Maandiko Matakatifu
Helamani 1


Kitabu cha Helamani

Historia ya Wanefi. Vita vyao na mabishano, na mafarakano yao. Na pia unabii wa manabii wengi watakatifu, kabla ya ujio wa Kristo, kulingana na maandishi ya Helamani, ambaye alikuwa mwana wa Helamani, na pia kulingana na maandishi ya wanawe, hata mpaka kuja kwa Kristo. Na pia wengi wa Walamani wanaongoka. Maelezo ya uongofu wao. Maelezo ya haki ya Walamani, na uovu na machukizo ya Wanefi, kulingana na maandishi ya Helamani na wanawe, hata mpaka ujio wa Kristo, ambacho kinaitwa kitabu cha Helamani, na kadhalika.

Mlango wa 1

Pahorani wa pili anakuwa mwamuzi mkuu na anauawa na Kishkumeni—Pakumeni anachukua kiti cha hukumu—Koriantumuri anaongoza majeshi ya Walamani, anateka Zarahemla, na anamuua Pakumeni—Moroniha anawashinda Walamani na kuteka tena Zarahemla, na Koriantumuri anauawa. Karibia mwaka 52–50 K.K.

1 Na sasa tazama, ikawa katika mwanzo wa mwaka wa arubaini wa utawala wa waamuzi juu ya watu wa Nefi, kulianza kuwa na taabu kubwa miongoni mwa watu wa Wanefi.

2 Kwani tazama, aPahorani alikuwa amefariki, na kwenda njia ya kawaida ya ulimwengu; kwa hivyo kulianza kuwa na ubishi kuhusu ni nani atakayechukua kiti cha hukumu miongoni mwa kaka, ambao walikuwa wana wa Pahorani.

3 Sasa haya ndiyo majina ya wale ambao walishindania kiti cha hukumu, ambao pia walisababisha watu kugombana: Pahorani, Paanki, na Pakumeni.

4 Sasa hawa sio wana wote wa Pahorani (kwani alikuwa na wengi), lakini hawa ndiyo wale ambao walishindania kiti cha hukumu; kwa hivyo, walianzisha migawanyiko mitatu miongoni mwa watu.

5 Walakini, ikawa kwamba Pahorani alichaguliwa kwa asauti ya watu kuwa mwamuzi mkuu na mtawala juu ya watu wa Nefi.

6 Na ikawa kwamba wakati Pakumeni alipoona kwamba hangepata kiti cha hukumu, alikubaliana na sauti ya watu.

7 Lakini tazama, Paanki, na sehemu ya watu ambao walitaka kwamba awe mtawala wao, walikasirika sana; kwa hivyo, alikuwa karibu kuwachochea hao watu kuasi dhidi ya ndugu zao.

8 Na ikawa kwamba vile alipokuwa karibu kufanya hivi, tazama, alikamatwa, na kujaribiwa kulingana na sauti ya watu, na kuhukumiwa kifo; kwani alikuwa ameasi na alitaka kuangamiza auhuru wa watu.

9 Sasa wakati wale watu ambao walitaka kwamba awe mtawala wao walipoona kwamba amehukumiwa kifo, kwa hivyo walikasirika, na tazama, walimtuma mtu mmoja kwa jina la Kishkumeni, kwenda kwa kiti cha hukumu cha Pahorani, na kumuua Pahorani wakati alipokuwa amekalia kiti cha hukumu.

10 Na akafukuzwa na watumishi wa Pahorani; lakini tazama, mwendo wa Kishkumeni ulikuwa wa kasi sana kwamba mtu yeyote hangemshika.

11 Na akarudi kwa wale ambao walimtuma, na wote wakaingia katika agano, ndiyo, wakiapa kwa Muumba wao asiye na mwisho, kwamba hawatamwambia yeyote kwamba Kishkumeni alikuwa amemuua Pahorani.

12 Kwa hivyo, Kishkumeni hakujulikana miongoni mwa watu wa Nefi, kwani alikuwa amejigeuza wakati ambao alimuua Pahorani. Na Kishkumeni na kundi lake, ambao walikuwa wamefanya agano naye, walijichanganya miongoni mwa watu, kwa njia kwamba hawangeweza kupatikana; lakini wale waliopatikana walihukumiwa akifo.

13 Na sasa tazama, Pakumeni alichaguliwa, kulingana na sauti ya watu, kuwa mwamuzi mkuu na mtawala juu ya watu, kutawala mahali pa kaka yake Pahorani; na ilikuwa kulingana na haki yake. Na hayo yote yalifanyika katika mwaka wa arubaini wa utawala wa waamuzi; na yalikuwa na mwisho.

14 Na ikawa katika mwaka wa arubaini na moja wa utawala wa waamuzi, kwamba Walamani walikuwa wamekusanya pamoja jeshi kubwa wasiohesabika la watu, na kuwahami kwa panga, na kwa vitara na kwa pinde, na kwa mishale, na kwa vyapeo, na kwa dirii, na kwa kila namna ya ngao ya kila aina.

15 Na walikuja tena ili waanzishe vita dhidi ya Wanefi. Na waliongozwa na mtu ambaye jina lake lilikuwa Koriantumuri; na alikuwa wa uzao wa Zarahemla; na alikuwa mwasi kutoka miongoni mwa Wanefi; na alikuwa mtu mkubwa na mwenye nguvu.

16 Kwa hivyo, mfalme wa Walamani, ambaye jina lake lilikuwa Tubalothi, ambaye alikuwa mwana wa aAmoroni, alidhani kwamba Koriantumuri, akiwa na nguvu nyingi, angeweza kusimama dhidi ya Wanefi, na nguvu zake na pia hekima yake kuu, mpaka kwamba kwa kumtuma yeye mbele angepata uwezo juu ya Wanefi—

17 Kwa hivyo aliwachochea kuwa na hasira, na akakusanya pamoja majeshi yake, na kumweka Koriantumuri kuwa kiongozi wao, na kuwasababisha kwenda chini kwenye nchi ya Zarahemla kupigana dhidi ya Wanefi.

18 Na ikawa kwamba kwa sababu ya ubishi mwingi na taabu nyingi serikalini, kwamba hawakuwa wameweka walinzi wa kutosha katika nchi ya Zarahemla; kwani walikuwa wamefikiri kwamba Walamani hawangekuja hadi katikati ya nchi yao kushambulia huo mji mkubwa wa Zarahemla.

19 Lakini ikawa kwamba Koriantumuri alitembea mbele ya jeshi lake kubwa, na kuwafikia wakazi wa mji, na mwendo wao ulikuwa wa kasi sana kiasi kwamba hapakuweko na nafasi ya Wanefi kukusanya majeshi yao pamoja.

20 Kwa hivyo Koriantumuri aliua walinzi wa lango la mji, na akaenda mbele na jeshi lake lote hadi kwenye mji, na wakamuua yeyote aliyewapinga, mpaka kwamba wakamiliki mji wote.

21 Na ikawa kwamba Pakumeni, ambaye alikuwa mwamuzi mkuu, alitoroka mbele ya Koriantumuri, hata akafikia kuta za mji. Na ikawa kwamba Koriantumuri alimpiga kwenye ukuta, mpaka akafa. Na hivyo siku za Pakumeni zikaisha.

22 Na sasa wakati Koriantumuri alipoona kwamba amemiliki mji wa Zarahemla, na kuona kwamba Wanefi wamewatoroka, na wameuawa, na wamekamatwa, na wametupwa gerezani, na kwamba amepata uwezo juu ya mji wenye nguvu sana katika nchi yote, moyo wake ulipata ujasiri mpaka kwamba alikuwa karibu kwenda dhidi ya nchi yote.

23 Na sasa hakukawia kwenye nchi ya Zarahemla, lakini alienda na jeshi kubwa, hata na kuelekea kwenye mji wa Neema; kwani nia yake ilikuwa kwenda mbele na kupata njia yake kwa kutumia upanga, ili aweze kupata sehemu za kaskazini ya nchi.

24 Na, akidhani kwamba nguvu zao kubwa zilikuwa katikati ya nchi, kwa hivyo alienda mbele, bila kuwapatia nafasi ya kujikusanya wenyewe pamoja isipokuwa tu kwa vikundi vidogo; na kwa njia hii waliwashukia na kuwatupa chini ardhini.

25 Lakini tazama, huu mwendo wa Koriantumuri kupita katikati ya nchi ulimpa Moroniha faida kubwa juu yao, ingawa idadi kubwa ya Wanefi waliouawa.

26 Kwani tazama, Moroniha alikuwa amedhani kwamba Walamani hawangethubutu kuja katikati ya nchi, lakini kwamba wangeshambulia miji iliyo karibu na mipaka vile walivyokuwa wamefanya hapo awali; kwa hivyo Moroniha alikuwa ameamuru kwamba majeshi yao yenye nguvu yalinde sehemu hizo karibu na kando ya mipaka.

27 Lakini tazama, Walamani hawakuogopa kulingana na kusudi lake, lakini walikuwa wamekuja katikati ya nchi, na walikuwa wamekamata mji mkuu ambao ulikuwa Zarahemla, na walikuwa wanapitia katika sehemu nyingi kubwa za nchi, wakiwaua watu na mauaji makubwa, wote wanaume, wanawake, na watoto, wakimiliki miji mingi na ngome nyingi.

28 Lakini Moroniha alipogundua hii, mara moja alimtuma Lehi na jeshi kuwazunguka na kuwazuia kabla ya kufika nchi ya Neema.

29 Na hivyo ndivyo alivyofanya; na aliwazuia kabla ya hao kufikia nchi ya Neema, na akakabiliana nao, mpaka kwamba wakaanza kurudi nyuma kuelekea nchi ya Zarahemla.

30 Na ikawa kwamba Moroniha aliwazuia kukimbia, na akakabiliana nao, mpaka kwamba kukawa na vita vya kumwaga damu nyingi; ndiyo, wengi waliuawa, na miongoni mwa idadi ya waliouawa aKoriantumuri alipatikana miongoni mwao.

31 Na sasa, tazama, Walamani hawakuweza kurudi nyuma upande wowote, upande wa kaskazini, wala kusini, wala mashariki, wala magharibi, kwani walizungukwa kila upande na Wanefi.

32 Na hivyo Koriantumuri alikuwa amewatumbukiza Walamani katikati ya Wanefi, mpaka kwamba walikuwa chini ya uwezo wa Wanefi, na yeye mwenyewe akauawa, na Walamani wakajisalimisha kwa Wanefi.

33 Na ikawa kwamba Moroniha alichukua tena mji wa Zarahemla, na kuamuru kwamba Walamani ambao walikuwa wameshikiliwa mahabusu wakubaliwe kutoka nchini kwa amani.

34 Na hivyo ukaisha mwaka wa arubaini na moja wa utawala wa waamuzi.