Maandiko Matakatifu
Etheri 13


Mlango wa 13

Etheri anazungumzia Yerusalemu Mpya kujengwa katika Marekani na uzao wa Yusufu—Anatoa unabii, anatupwa nje, anaandika historia ya Wayaredi, na anatabiri kuangamizwa kwa Wayaredi—Vita vinaendelea kote nchini.

1 Na sasa mimi, Moroni, naendelea kumaliza maandishi yangu kuhusu uharibifu wa watu ambao nimekuwa nikiandika juu yao.

2 Kwani tazama, walikataa maneno yote ya Etheri; kwani aliwaambia kwa kweli vitu vyote, kutokea mwanzoni mwa binadamu; na kwamba wakati maji yalipokuwa ayamepungua kutoka juu ya uso wa nchi ilikuwa nchi iliyochaguliwa kuliko zingine zote, nchi iliyochaguliwa na Bwana; kwa hivyo Bwana alitaka kwamba watu wote bwangemtumikia, wale ambao wanaishi juu yake;

3 Na kwamba ilikuwa mahali pa aYerusalemu Mpya, ambayo bingekuja chini kutoka mbinguni, na utakatifu wa wakfu wa Bwana.

4 Tazama, Etheri aliona siku za Kristo, na alizungumza kuhusu aYerusalemu Mpya juu ya nchi hii.

5 Na alizungumza pia kuhusu nyumba ya Israeli, na aYerusalemu ambako bLehi angetokea—baada ya kuharibiwa kwake itajengwa tena, cmji mtakatifu wa Bwana; kwa hivyo, haingekuwa Yerusalemu mpya kwani ilikuwa wakati wa kale; lakini ingejengwa tena, na uwe mji mtakatifu wa Bwana; na ingejengwa kwa ajili ya nyumba ya Israeli—

6 Na kwamba aYerusalemu Mpya ingejengwa juu ya nchi hii, kwa ajili ya baki la uzao wa bYusufu, kwa vitu ambavyo kumekuwa na cmfano.

7 Kwani vile Yusufu alimleta baba yake chini katika nchi ya aMisri, hata hivyo alikufa huko; kwa hivyo, Bwana alileta baki la uzao wa Yusufu kutoka nchi ya Yerusalemu, kwamba angekuwa na huruma kwa uzao wa Yusufu kwamba bwasiangamie, hata vile alikuwa na huruma kwa baba ya Yusufu ili asiangamie.

8 Kwa hivyo, baki la nyumba ya Yusufu litajengwa juu ya anchi hii; na itakuwa nchi ya urithi wao; na watajenga mji mtakatifu kwa Bwana, kama Yerusalemu ya kale; na bhawatachanganywa tena, mpaka mwisho utakapofika wakati dunia itakapoisha.

9 Na kutakuwa na mbingu ampya na dunia mpya; na zitakuwa kama za kale ijapokuwa ya kale imepita mbali, na vitu vyote vimekuwa vipya.

10 Na ndipo kutatokea Yerusalemu Mpya; na heri wanaoishi ndani yake, kwani ni hao ambao mavazi yao ni asafi kupitia kwa damu ya Mwanakondoo; na ni hao hao ambao wamehesabiwa miongoni mwa baki la uzao wa Yusufu, ambao walikuwa wa nyumba ya Israeli.

11 Na hapo pia kutatokea Yerusalemu ya kale; na wakazi wake, wamebarikiwa, kwani wameoshwa kwenye damu ya Mwanakondoo; ni hawa ambao walitawanywa na akukusanywa kutoka pande nne za dunia, na kutoka katika nchi za bkaskazini, na ni washiriki wa lile agano ambalo Mungu alifanya na baba yao, cIbrahimu.

12 Na wakati vitu hivi vitakapokuja, huletwa kutimizwa andiko ambalo linasema, wako wale walio wa akwanza, watakaokuwa wa mwisho; na wako wale waliokuwa wa mwisho, ambao watakuwa wa kwanza.

13 Na nilikuwa karibu kuandika zaidi, lakini nimekatazwa; lakini kuu na wa ajabu ulikuwa unabii wa Etheri; lakini walimdhania kuwa bure, na wakamtupa nje; na alijificha kwenye pango la mwamba wakati wa mchana, na wakati wa usiku alienda akiangalia vitu ambavyo vitawajia watu.

14 Na vile alivyoishi kwenye pango la mwamba aliandika maandishi haya yaliyosalia, akitazama uharibifu ambao uliwajia watu, wakati wa usiku.

15 Na ikawa kwamba katika mwaka huo huo ambamo alitupwa nje kutoka miongoni mwa watu vita vikubwa vilianza miongoni mwa watu, kwani kulikuwa na wengi walioasi, ambao walikuwa watu wenye nguvu, na walitafuta kumwangamiza Koriantumuri kwa mipango yao ya siri na maovu, ambayo yamezungumziwa.

16 Na sasa Koriantumuri, akiwa amesoma, mwenyewe, katika ustadi wote wa vita na ujanja wote wa ulimwengu, kwa hivyo alifanya vita na wale waliotaka kumwangamiza.

17 Lakini hakutubu, wala wanawe wenye sura nzuri na mabinti zake; wala wana na mabinti za Kohori waliokuwa na sura nzuri; wala wana na mabinti za Korihori ambao walikuwa na sura nzuri; na kwa kifupi, hakukuwa na wana na mabinti waliokuwa na sura nzuri juu ya uso wa dunia nzima ambao walitubu dhambi zao.

18 Kwa hivyo, ikawa kwamba katika mwaka wa kwanza ambamo Etheri aliishi kwenye pango la mwamba, kulikuwa na watu wengi waliouawa kwa upanga wa wale wa akundi ovu la siri, likipigana dhidi ya Koriantumuri ili wangepata ufalme.

19 Na ikawa kwamba wana wa Koriantumuri walipigana sana na walitokwa na damu sana.

20 Na katika mwaka wa pili neno la Bwana lilimjia Etheri, kwamba aende na amtabirie aKoriantumuri kwamba, ikiwa angetubu, na nyumba yake yote, Bwana angempatia ufalme wake na kuwaachilia watu—

21 La sivyo wangeangamizwa, na nyumba yake yote isipokuwa yeye. Na angeishi tu kushuhudia utimizaji wa unabii ambao umezungumziwa kuhusu watu awengine kupokea nchi kwa urithi wao; na Koriantumuri angezikwa na hao; na kila mtu angeangamizwa isipokuwa bKoriantumuri.

22 Na ikawa kwamba Koriantumuri hakutubu, wala nyumba yake, wala watu; na vita havikuisha; na walitaka kumuua Etheri, lakini alitoroka kutoka kwao na kujificha tena kwenye pango la ule mwamba.

23 Na ikawa kwamba kulitokea mtu ambaye aliitwa Sharedi, na alifanya vita na Koriantumuri; na alimshinda, mpaka kwamba katika mwaka wa tatu alimweka kwenye utumwa.

24 Na wana wa Koriantumuri, katika mwaka wa nne, walimshinda Sharedi, na kumrudisha baba yao kwenye ufalme.

25 Sasa kulianza kuwa na vita juu ya uso wa nchi yote, kila mtu na kundi lake akipigania kile alichotaka.

26 Na kulikuwa na wanyangʼanyi, na kwa kifupi, kila aina ya uovu juu ya uso wa nchi yote.

27 Na ikawa kwamba Koriantumuri alimkasirikia sana Sharedi, na akamwendea na jeshi lake kupigana; na walikutana kwa hasira kubwa, na walikutania kwenye bonde la Gilgali; na vita vikawa vikali sana.

28 Na ikawa kwamba Sharedi alipigana dhidi yake kwa muda wa siku tatu. Na ikawa kwamba Koriantumuri alimshinda, na kumfukuza mpaka alipofikia mahali tambarare pa Heshloni.

29 Na ikawa kwamba Sharedi alimfanyia vita tena juu ya tambarare; na tazama, alimshinda Koriantumuri, na kumrudisha nyuma tena hadi kwenye bonde la Gilgali.

30 Na Koriantumuri alifanya vita na Sharedi tena kwenye bonde la Gilgali, ambamo kwake alimshinda Sharedi na kumuua.

31 Na Sharedi alimjeruhi Koriantumuri katika paja lake, kwamba hangepigana tena kwa muda wa miaka miwili, wakati ambamo watu wote juu ya uso wa nchi walikuwa wanamwaga damu, na hakukuwa na yeyote ambaye angewazuia.