Maandiko Matakatifu
Alma 45


Historia ya watu wa Nefi, na vita vyao na mafarakano yao, katika siku za Helamani, kulingana na maandishi ya Helamani, ambayo aliweka katika siku zake.

Yenye milango ya 45 hadi 62.

Mlango wa 45

Helamani anaamini maneno ya Alma—Alma anatabiri kuangamizwa kwa Wanefi—Anabariki na kulaani nchi—Inaonekana Alma alichukuliwa juu na Roho, kama vile Musa—Mfarakano unatokea kanisani. Karibia mwaka 73 K.K.

1 Tazama, sasa ikawa kwamba watu wa Nefi walikuwa na furaha sana, kwa sababu Bwana alikuwa amewaokoa tena kutoka mikono ya maadui wao; kwa hivyo walitoa shukrani kwa Bwana Mungu wao; ndiyo, na awalifunga sana, na kuomba sana na wakamwabudu Mungu kwa shangwe kuu.

2 Na ikawa katika mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa waamuzi juu ya watu wa Nefi, kwamba Alma alimjia mwana wake Helamani na kumwambia: Unaamini wewe maneno ambayo nilikuzungumzia kuhusu yale amaandiko ambayo yamehifadhiwa?

3 Na Helamani akasema kwake: Ndiyo, naamini.

4 Na Alma akasema tena: Unaamini katika Yesu Kristo, atakayekuja?

5 Na akasema: Ndiyo, ninaamini maneno yote ambayo umesema.

6 Na Alma akasema kwake tena: aUtaweka amri zangu?

7 Na akasema: Ndiyo, nitatii amri zako kwa moyo wangu wote.

8 Na Alma akamwambia: Umebarikiwa wewe; na Bwana aatakufanikisha katika nchi hii.

9 Lakini tazama, nitakutolea aunabii mdogo; lakini yale ambayo nita kwako usifanye yajulikane; ndiyo, yale nitakayotabiri kwako hayatafanywa yasijulikane, hata mpaka utabiri utakavyotimizwa; kwa hivyo andika maneno ambayo nitasema.

10 Na haya ndiyo maneno: Tazama, ninaona kwamba watu hawa, Wanefi, kulingana na roho ya ufunuo ambayo iko ndani yangu, katika miaka amia nne kutoka wakati ambao Yesu Kristo atajidhihirisha kwao, watafifia kwa bkutoamini.

11 Ndiyo, na ndipo wataona vita na maradhi ya kuambukiza, ndiyo, njaa na umwagaji wa damu, hata mpaka watu wa Nefi awatakapomalizika

12 Ndiyo, na itafanyika kwa sababu watafifia katika kutoamini na kuangukia kazi za gizani, na auzinzi, na aina yote ya uovu; ndiyo, nakwambia, kwamba kwa sababu watakosa dhidi ya mwangaza ulio mkubwa na hekima, ndiyo, nakwambia, kwamba kutokea siku hiyo, hata kizazi cha nne hakitapita kabla ya huu uovu kutokea.

13 Na wakati ile siku kuu itakapowadia, tazama, wakati unawadia mapema kwamba wale ambao wako sasa, au uzao wa wale ambao wamehesabiwa miongoni mwa watu wa Nefi, ahawatahesabiwa tena miongoni mwa watu wa Nefi.

14 Lakini yeyote atakayebaki, na haangamizwi katika ile siku kuu na ya kuogopesha, aatahesabiwa miongoni mwa Walamani, na atakuwa kama wao, wote, isipokuwa wachache ambao wataitwa wanafunzi wa Bwana; na hao Walamani watawawinda mpaka wakati bwatakapomalizika. Na sasa, kwa sababu ya uovu, huu unabii utatimizwa.

15 Na sasa ikawa kwamba baada ya Alma kusema vitu hivi kwa Helamani, alimbariki, na pia wanawe wengine; na pia akabariki ardhi kwa wale walio ahaki.

16 Na akasema: Hivyo ndivyo asemavyo Bwana Mungu—Nchi aitalaaniwa, ndiyo, nchi hii, kwa kila taifa, kabila, lugha, na watu, kwa uangamizo, ambao wanafanya uovu, wakati watakapoiva kabisa kwa uovu; na vile nimesema ndivyo itakavyokuwa; kwani hii ni laana na bbaraka ya Mungu juu ya nchi, kwani Bwana hawezi kuangalia dhambi na kuivumilia hata ckidogo.

17 Na sasa, wakati Alma alipokuwa amesema maneno haya alibariki akanisa, ndiyo, wale wote ambao watasimama imara katika imani kutokea wakati huo na kuendelea.

18 Na wakati Alma alipofanya haya aliondoka kutoka nchi ya Zarahemla, kama anayeenda katika nchi ya Meleki. Na ikawa kwamba hakusikika tena; hatujui kulingana kifo chake au kuzikwa kwake.

19 Tazama, haya tunajua, kwamba alikuwa mtu wenye haki; na msemo ukaenea kanisani kwamba alichukuliwa na Roho, au akuzikwa kwa mkono wa Bwana, kama vile Musa. Lakini tazama, maandiko yanasema kuwa Bwana alimchukua Musa kumrudisha kwake mwenyewe; na tunadhani kwamba pia amempokea Alma katika roho, kwake mwenyewe; kwa hivyo, kwa sababu hii hatujui chochote kuhusu kifo chake wala mazishi yake.

20 Na sasa ikawa katika mwanzo wa mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa waamuzi juu ya watu wa Nefi, kwamba Helamani alienda miongoni mwa watu kuwatangazia neno.

21 Kwani tazama, kwa sababu ya vita vyao na Walamani na mafarakano mengi madogo na vurugu ambazo zilikuwa miongoni mwa watu, ilikuwa ni lazima kwamba aneno la Mungu litangazwe kwao, ndiyo, na kwamba maagizo yafanywe kokote kanisani.

22 Kwa hivyo, Helamani na ndugu zake walienda mbele na kuanzisha kanisa tena katika nchi, ndiyo, katika kila mji kote katika nchi ambao ulikuwa umemilikiwa na watu wa Nefi. Na ikawa kwamba waliteua makuhani na walimu kote nchini, juu ya makanisa yote.

23 Na sasa ikawa kwamba baada ya Helamani na ndugu zake kuteua makuhani na walimu juu ya makanisa kwamba kukatokea amfarakano miongoni mwao, na hawakusikiliza maneno ya Helamani na ndugu zake;

24 Bali walianza kuwa na kiburi, wakijiinua kwa mioyo yao, kwa sababu ya autajiri wao mwingi; kwa hivyo walikuwa matajiri kwenye fikira bzao, na hawakusikiliza maneno yao, kutembea wima mbele ya Mungu.