Maandiko Matakatifu
Alma 42


Mlango wa 42

Maisha ya duniani ni wakati wa majaribio kumwezesha mtu kutubu na kumtumikia Mungu—Anguko limeleta kifo cha kimwili na cha kiroho kwa binadamu wote—Ukombozi huja kupitia toba—Mungu Mwenyewe hulipia dhambi za ulimwengu—Rehema ni kwa wale ambao wanatubu—Wengine wote wako chini ya hukumu ya Mungu—Rehema huja kwa sababu ya Upatanisho—Ni wale tu wenye toba ya kweli wanaokolewa. Karibia mwaka 74 K.K.

1 Na sasa, mwana wangu, naona kuna kitu kidogo zaidi ambacho kinakusumbua akili yako, ambacho huwezi kuelewa—ambacho kinahusu aunyoofu wa Mungu kwa kuadhibu wenye dhambi; kwani unajaribu kudhani kwamba si haki kwamba wenye dhambi watupiliwe kwenye hali ya taabu.

2 Sasa tazama, mwana wangu, nitakuelezea hiki kitu. Kwani tazama, baada ya Bwana Mungu akutuma wazazi wetu wa kwanza kutoka kwenye bustani ya bEdeni, kulima ardhi, kutoka ambapo walipelekwa—ndiyo, alimfukuza huyo mtu, na akaweka cmakerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huku na huko, kulinda dmti wa uzima

3 Sasa, tunaona kwamba yule mtu alikuwa kama Mungu, akijua wema na uovu; na ili asinyooshe mkono wake mbele, na achukue pia kwa mti wa uzima, na kula na kuishi milele, Bwana Mungu aliweka makerubi na upanga wa moto, ili asile tunda—

4 Na hivyo tunaona, kwamba kulikuwa na wakati ambao uliwekewa mwanadamu kutubu, ndiyo, awakati wa majaribio, wakati wa kutubu na kumtumikia Mungu.

5 Kwani tazama, kama Adamu angenyoosha mkono wake haraka, na kula kutoka kwa mti wa uzima, angeishi milele, kulingana na neno la Mungu, kukiwa hakuna nafasi ya toba; ndiyo, na pia neno la Mungu lingekuwa bure, na mpango mkuu wa wokovu ungezuiliwa.

6 Lakini tazama, ilipangiwa mwanadamu akufa—kwa hivyo, vile walitolewa mbali kutoka kwa mti wa uzima wangetolewa mbali kutoka uso wa dunia—na mwanadamu alipotea milele, ndiyo, binadamu bwakaanguka.

7 Na sasa, kwa hii unaona kwamba wazazi wetu wa kwanza awalitolewa mbali yote kimwili na kiroho kutoka kwa uwepo wa Bwana; na hivyo tunaona wakawa raia wa kufuata bkusudi lao.

8 Sasa tazama, haikuwa ya kufaa kwamba mwanadamu arudishwe kutoka kwa kifo chake cha mwili, kwani hiyo ingeangamiza ampango mkuu wa furaha.

9 Kwa hivyo, kwa vile roho haingekufa, na aanguko umeleta kwa wanadamu wote kifo cha roho na pia cha mwili, inaamanisha, walitolewa mbali na uwepo wa Bwana, ilikuwa ni lazima kwamba mwanadamu arudishwe kutoka kwenye kifo hiki cha roho.

10 Kwa hivyo, tangu walipokuwa wamekuwa na atamaa za kimwili, uasherati, na uibilisi, kwa basili, hii chali ya majaribio ilikuwa hali ya wao kujitayarisha; ikawa hali ya matayarisho.

11 Na sasa kumbuka, mwana wangu, kama haungekuwa mpango wa ukombozi, (kuwekwa kando) upesi vile walikufa roho zao zilikuwa ataabuni, ikiwa imetolewa kutoka kwa uwepo wa Bwana.

12 Na sasa, hapakuwa na njia ya kudai wanadamu kutoka hali hii ya kuanguka, ambayo mwanadamu alijiletea kwa sababu ya kutotii kwake;

13 Kwa hivyo, kulingana na haki, ampango wa ukombozi haungeletwa, tu kwa tabia ya btoba ya wanadamu katika hali hii ya majaribio, ndiyo, hali hii ya kujitayarisha; kwani isingekuwa masharti haya, rehema haingefaa isipokuwa iangamize kazi ya haki. Sasa kazi ya haki haiengeangamizwa; ikiwa hivyo, Mungu cangekoma kuwa Mungu.

14 Na hivyo tunaona kwamba binadamu wote awalianguka, na wakawa wameshikwa na bhaki; ndiyo, haki ya Mungu ambayo amewatolea milele watolewe kwenye uwepo wake.

15 Na sasa, mpango wa rehema haungetimizwa isipokuwa upatanisho ufanywe; kwa hivyo Mungu mwenyewe ahulipia dhambi za ulimwengu, kutimiza mpango wa brehema, kuwezesha mahitaji ya chaki, kwamba Mungu angekuwa dmkamilifu, na Mungu mwenye haki, na Mungu wa huruma pia.

16 Sasa, toba haingewajia watu isipokuwa kuwe na adhabu, ambayo pia ilikuwa ya amilele kama vile uhai wa roho ulivyo, umepandikishwa kinyume na mpango wa furaha, ambao ulikuwa wa milele kama vile uhai wa roho ulivyo.

17 Sasa, mtu anaweza kutubu namna gani isipokuwa atende dhambi? Ni vipi angetenda adhambi ikiwa hapakuweko na bsheria? Kungekuwaje sheria kusipokuwa na adhabu?

18 Sasa, kulikuwa na adhabu iliyobandikwa, na sheria ya haki ikatolewa, ambayo ilileta majuto ya adhamiri kwa watu.

19 Sasa, kama sheria haingetolewa—ikiwa mtu aataua sharti auawe—je, angeogopa kwamba angekufa ikiwa angeua?

20 Na pia, kama hakungekuwa na sheria kutolewa dhidi ya dhambi watu hawangeogopa kutenda dhambi.

21 Na kama sheria ahaingetolewa, wakati watu wanatenda dhambi, haki ingefanya nini au rehema, kwani hawangekuwa na madai juu ya kiumbe?

22 Lakini sheria imetolewa, na adhabu kuwekwa, na atoba kukubaliwa; toba ambayo, rehema hudai; la sivyo, kazi ya haki ingedai kiumbe na kutimiza sheria, na sheria kutoa adhabu; kama sio hivyo matendo ya haki yangeangamizwa, na Mungu kukoma kuwa Mungu.

23 Lakini Mungu hakomi kuwa Mungu, na arehema hudai wanaotubu, na rehema huja kwa sababu ya upatanisho; na bupatanisho huleta cufufuo wa wafu; na ufufuo wa wafu dhuwarudisha watu kwenye uwepo wa Mungu; na hivyo wanarudishwa kwenye uwepo wake, ekuhukumiwa kulingana na matendo yao, kulingana na sheria na haki.

24 Kwani tazama, haki hutekeleza madai yake yote, na pia huruma hudai yote yaliyo yake; na hivyo, hakuna ila tu waliotubu kwa ukweli watakaokolewa.

25 Ni nini, unadhani kwamba rehema inaweza kuibia ahaki? Ninakwambia, Hapana; hata chembe kimoja. Ikiwa hivyo, Mungu atakoma kuwa Mungu.

26 Na hivyo Mungu hutimiza akusudi lake kubwa na la milele, ambalo lilitayarishwa bkutokea msingi wa dunia. Na hivyo huja wokovu na ukombozi wa binadamu, na pia maangamizo yao na taabu.

27 Kwa hivyo, Ee mwana wangu, ayeyote atakeyekuja angekuja na kunywa maji ya uzima bure; yeyote atakayekataa kuja hivyo hatashurutishwa kuja; lakini katika siku ya mwisho bitarudishwa kwake kulingana na cvitendo vyake.

28 Ikiwa anatamani kufanya auovu, na hajatubu katika siku zake, tazama, uovu utafanywa kwake, kulingana na kurudishwa kwa Mungu.

29 Na sasa, mwana wangu, nataka kwamba usiache vitu hivi vikusumbue mara nyingine, na ni dhambi zako tu zikusumbue, pamoja na taabu hiyo ambayo itakuleta wewe katika toba.

30 Ee mwana wangu, nataka kwamba usikane haki ya Mungu mara nyingine. Usijaribu kujisamehe mwenyewe hata kwa njia ndogo kwa sababu ya dhambi zako, kwa kukataa haki ya Mungu; lakini uache haki ya Mungu, na rehema yake, na uvumilivu wake uvume ndani ya moyo wako; na acha ikulete chini kwenye mavumbi ndani ya aunyenyekevu.

31 Na sasa, Ee mwana wangu, umeitwa na Mungu kuhubiri neno kwa hawa watu. Na sasa, mwana wangu, nenda njia zako, tangaza neno kwa ukweli na busara, kwamba uzilete roho kwenye toba, kwamba mpango mkuu wa rehema ungekuwa na madai juu yao. Na Mungu akupatie hata kulingana na maneno yangu. Amina.