Maandiko Matakatifu
Alma 28


Mlango wa 28

Walamani wanashindwa kwenye vita vya kutisha—Maelfu na maelfu wauawa—Waovu wanahukumiwa wawe katika hali ya masumbuko ya milele; wenye wema wanapokea furaha isiyo na mwisho. Karibia mwaka 77–76 K.K.

1 Na ikawa kwamba baada ya watu wa Amoni kuimarishwa kwenye nchi ya Yershoni, na kanisa pia kuanzishwa kwenye nchi ya aYershoni, na majeshi ya Wanefi kuwekwa kila mahali kwenye nchi ya Yershoni, ndiyo, kwenye mipaka yote kuzunguka nchi ya Zarahemla; tazama majeshi ya Walamani yalikuwa yamewaandama ndugu zao hadi kwenye nyika.

2 Na hivyo kulikuwa na vita vya kutisha; ndiyo, hata vita kama hivyo havikuwa vimeonekana kamwe miongoni mwa watu wote nchini kutoka Lehi alipotoka Yerusalemu; ndiyo, na maelfu na maelfu ya Walamani waliuawa na kutawanywa kila mahali.

3 Ndiyo, na pia kulikuwa na mauaji ya ajabu miongoni mwa watu wa Nefi; lakini, Walamani awalifukuzwa na kutawanywa, na watu wa Nefi walirudi tena kwa nchi yao.

4 Na sasa huu ulikuwa wakati ambao kulikuwa na huzuni na vilio vilivyosikika kote nchini, miongoni mwa watu wa Nefi—

5 Ndiyo, vilio vya wajane wakiomboleza mabwana zao, na pia baba wakiomboleza wana wao; na binti kwa kaka, ndiyo, kaka kwa baba; na hivyo vilio vya kuombeleza vilisikika miongoni mwao wote, wakiomboleza jamaa zao ambao waliuawa.

6 Na sasa hii ilikuwa siku ya huzuni; ndiyo, wakati wa unadhiri, na wakati wa akufunga na kusali.

7 Na hivyo mwaka wa kumi na tano wa utawala wa waamuzi juu ya watu wa Nefi ukaisha;

8 Na hii ni historia ya Amoni na ndugu zake, matembezi yao kwenye nchi ya Nefi, kuumia kwao nchini, masikitiko yao, na mateso yao, na shangwe yao isiyo na akipimo, na makaribisho na ulinzi kutoka kwa ndugu zao kwenye nchi ya Yershoni. Na sasa Bwana, Mkombozi wa watu wote, aibariki nafsi zao milele.

9 Na hii ni historia ya vita na mabishano miongoni mwa Wanefi, na pia vita baina ya Wanefi na Walamani; na mwaka wa kumi na tano wa utawala wa waamuzi umeisha.

10 Na kutoka mwaka wa kwanza mpaka wa kumi na tano umeleta maangamizo ya maelfu ya maisha; ndiyo, umeleta vitendo vibaya vya umwagaji wa damu.

11 Na miili ya wengi imelazwa ardhini, wakati miili ya maelfu ainaoza kwa chunguchungu juu ya ardhi; ndiyo, na maelfu wengi bwanaomboleza kwa kupoteza jamii yao, kwa ajili wana sababu ya kuogopa, kulingana na ahadi za Bwana, kwamba wanadhainiwa masharti ya taabu ya daima.

12 Wakati maelfu wengi wa wengine kwa kweli wanaomboleza jamii yao, lakini wanafurahi na kushangilia kwa matumaini, na hata wanajua, kulingana na aahadi za Bwana, kwamba wanainuliwa na kuishi kwa mkono wa kulia wa Mungu, kwa hali ya furaha daima.

13 Na hivyo tunaona vile akutokuwa sawa kwingi kwa watu kwa sababu ya dhambi na makosa, na nguvu za ibilisi, ambayo huja kwa bmipango ya udanganyifu ambayo amefikiria kutega mioyo ya watu.

14 Na hivyo tunaona mwito mkuu wa uangalifu kwa watu kufanya kazi kwenye ashamba la mizabibu la Bwana; na hivyo tunaona sababu kuu ya huzuni, na pia ya kufurahi—huzuni kwa sababu ya vifo na uharibifu miongoni mwa watu, na shangwe kwa sababu ya bmwangaza wa Kristo ambao ni uzima.