Maandiko Matakatifu
Alma 1


Kitabu cha Alma
Mwana wa Alma

Historia ya Alma, ambaye alikuwa mwana wa Alma, mwamuzi mkuu wa kwanza juu ya watu wa Nefi, na pia kuhani mkuu wa Kanisa. Historia kuhusu utawala wa waamuzi, na vita na mabishano miongoni mwa wale watu. Na pia historia ya vita miongoni mwa Wanefi na Walamani, kulingana na maandishi ya Alma, mwamuzi mkuu wa kwanza.

Mlango wa 1

Nehori anafundisha mafundisho ya uwongo, anaanzisha kanisa, anaanzisha ukuhani wa uongo, na anamuua Gideoni—Nehori anauawa kwa sababu ya hatia zake—Ukuhani wa uongo na mateso yanaenea miongoni mwa watu—Makuhani wanajilisha, watu wanawajalia wale walio masikini, na Kanisa linafanikiwa. Karibia mwaka 91–88 K.K.

1 Sasa ikawa kwamba katika mwaka wa kwanza wa utawala wa waamuzi juu ya watu wa Nefi, tangu wakati huu na kuendelea mbele, mfalme Mosia akiwa aameelekea njia ya ulimwengu wote, akiwa amepigana vita vyema, akiwa ametembea wima mbele ya Mungu, akiwa hajaacha yeyote kutawala badala yake; walakini alikuwa ameanzisha bsheria, na zilikubaliwa na watu; kwa hivyo iliwabidi kuishi kulingana na sheria alizokuwa ameweka.

2 Na ikawa kwamba katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Alma katika kiti cha hukumu, kulikuwa na amtu mmoja ambaye aliletwa mbele yake ili ahukumiwe, mtu aliyekuwa mkubwa, na alifahamika kwa sababu ya nguvu zake nyingi.

3 Na alikuwa ameenda miongoni mwa watu, akiwa amewahubiria yale ambayo aaliita neno la Mungu, bakipinga kanisa; akiwatangazia watu kwamba inafaa kila kuhani na kila mwalimu awe cmashuhuri; na dhaifai wafanye kazi kwa mikono yao, lakini kwamba inafaa walishwe na watu.

4 Na alishuhudia kwa watu pia kwamba wanadamu wote wataokolewa katika siku ya mwisho, na kwamba haistahili waogope au kubabaika, lakini kwamba wainue vichwa vyao na washangilie; kwani Bwana alikuwa ameumba wanadamu wote, na pia kuwakomboa wanadamu wote; na, mwishowe, wanadamu wote watapokea uzima wa milele.

5 Na ikawa kwamba alifundisha vitu hivi sana hata kwamba wengi waliamini maneno yake, wengi sana hata wakaanza kumlisha na kumpatia pesa.

6 Na akaanza kujiinua kwa kiburi cha moyo wake, na kuvaa mavazi ya thamani nyingi, ndiyo, na hata akaanza kuanzisha akanisa kulingana na mafundisho yake.

7 Na ikawa kwamba alipokuwa akienda, kuhubiria wale walioamini neno lake, alikutana na mtu ambaye alikuwa wa kanisa la Mungu, ndiyo, hata mmoja wa walimu wao; na akaanza kubishana na yeye kwa ukali, ili awapotoshe watu wa kanisa; lakini yule mtu alimpinga, na kumuonya kwa amaneno ya Mungu.

8 Sasa jina la yule mtu lilikuwa aGideoni; na ni yeye ndiye aliyekuwa chombo mikononi mwa Mungu cha kuwakomboa watu wa Limhi kutoka utumwani.

9 Sasa, kwa sababu Gideoni alimpinga kwa maneno ya Mungu alimkasirikia Gideoni, na akauchomoa upanga wake na akaanza kumjeruhi. Sasa Gideoni alikuwa amelemewa kwa umri mkuu, kwa hivyo hakuweza kuvumilia mapigo yake, kwa hivyo aaliuawa kwa upanga.

10 Na mtu aliyemuua alichukuliwa na watu wa kanisa, na kuletwa mbele ya Alma, akuhukumiwa kulingana na kosa alilotenda.

11 Na ikawa kwamba alisimama mbele ya Alma na kujitetea kwa ujasiri mwingi.

12 Lakini Alma akamwambia: Tazama, hii ndiyo mara ya kwanza kwamba aukuhani wa uongo umeletwa miongoni mwa watu hawa. Na tazama, hatia yako sio tu ya ukuhani wa uongo, lakini umejaribu kuulazimisha kwa upanga; na kama ukuhani wa uongo utalazimishwa miongoni mwa watu hawa utathibitisha maangamizo yao kabisa.

13 Na wewe umemwaga damu ya mtu mwenye haki, ndiyo, mtu ambaye ametenda wema mwingi miongoni mwa watu hawa; na kama tutakuachilia basi damu yake itatujia kulipiza akisasi.

14 Kwa hivyo aumehukumiwa kufa, kulingana na sheria ambayo tulipewa na Mosia, mfalme wetu wa mwisho; na imekubaliwa na watu hawa; kwa hivyo lazima watu hawa waishi kulingana na sheria hiyo.

15 Na ikawa kwamba walimchukua; na jina lake lilikuwa aNehori; na wakambeba na kumpeleka juu ya kilima Manti, na hapo akalazimishwa, kwa usahihi zaidi akakubali, kati ya mbingu na ardhi, kwamba yale ambayo alikuwa amefundisha watu yalikuwa kinyume cha neno la Mungu; na hapo akapata bkifo cha aibu.

16 Walakini, hii haikukomesha kuenea kwa ukuhani wa uongo katika nchi; kwani kulikuwa na wengi ambao walipenda vitu vya ulimwengu visivyo na faida, na wakaendelea kuhubiri mafundisho ya uwongo; na walitenda haya ili wapate autajiri na heshima.

17 Walakini, hawakuthubutu akudanganya, kama ingejulikana, kwa kuogopa sheria, kwani waongo waliadhibiwa; kwa hivyo walidai kwamba walikuwa wanahubiri kulingana na imani yao; na sasa sheria haikuwa na uwezo wowote juu ya bimani ya mtu yeyote.

18 Na hawakuthubutu akuiba, kwani waliogopa sheria, kwani kama hao waliadhibiwa; wala hawakupora, wala kuua, kwani yule baliyeua alihukumiwa ckifo.

19 Lakini ikawa kwamba yeyote ambaye hakuwa wa kanisa la Mungu alianza kuwatesa wale ambao walikuwa wa kanisa la Mungu, na waliokuwa wamejivika jina la Kristo.

20 Ndiyo, waliwatesa, na kuwasumbua kwa maneno ya kila aina, na haya yalikuwa ni kwa sababu ya unyenyekevu wao; kwa sababu hawakuwa na majivuno katika macho yao wenyewe, na kwa sababu walifundishana neno la Mungu, wao kwa wao, bila kutozana apesa na bila gharama.

21 Sasa kulikuwa na sheria kali miongoni mwa watu wa kanisa, kwamba kusiwe na mtu yeyote, miongoni mwa washiriki wa kanisa, atakayeinuka na akuwatesa wale ambao sio washiriki wa kanisa, na kwamba kusiwe na mateso miongoni mwao.

22 Walakini, kulikuwa na wengi miongoni mwao ambao walianza kuwa na kiburi, na kuanza kubishana vikali na wapinzani wao, hata wakapigana kwa ngumi; ndiyo, walipigana kwa ngumi wao kwa wao.

23 Sasa hii ilikuwa katika mwaka wa pili wa utawala wa Alma, na ilikuwa ni chanzo cha mateso mengi kwa kanisa; ndiyo, ilikuwa ni chanzo cha majaribio mengi kwa kanisa.

24 Kwani mioyo ya wengi ilishupazwa na majina yao ayalifutwa, hata kwamba hawakukumbukwa tena miongoni mwa watu wa Mungu. Na pia wengi bwalijiondoa kutoka miongoni mwao.

25 Sasa hili lilikuwa ni jaribio kuu kwa wale ambao walikuwa wamesimama imara katika imani; walakini, walikuwa wameimarishwa na hawangeondolewa katika kutii amri za Mungu, na walivumilia kwa asubira mateso yale waliyotundikwa.

26 Na wakati makuhani walipoacha akazi zao ili watoe neno la Mungu kwa watu, watu nao pia waliacha kazi zao ili wasikie neno la Mungu. Na makuhani walipomaliza kuwafundisha neno la Mungu wote walirudia kazi zao kwa bidii; na kuhani, hakujiinua zaidi ya wale ambao walimsikiliza, kwani mhubiri hakuwa bora zaidi kuliko wale ambao walimsikiliza, wala mwalimu hakuwa bora kuliko mwanafunzi; na hivyo wote walikuwa sawa, na wote walifanya kazi, kila mtu bkulingana na nguvu zake.

27 Na awalipeana mali yao, kulingana na uwezo wao, kwa bmasikini, na waliohitaji, na wagonjwa, na walioteswa; na hawakuvaa mavazi ya thamani kubwa, lakini walikuwa wasafi na wa kuvutia.

28 Na hivyo waliimarisha mambo ya kanisa; na hivyo wakaanza kuwa na amani bila kikomo tena, ingawa walikuwa wamepata mateso mengi.

29 Na sasa, kwa sababu ya uthabiti wa kanisa walianza akutajirika sana, wakipokea kwa utele vitu vyote walivyohitaji—utele katika mifugo na wanyama, na vinono vya kila aina, na pia utele wa nafaka, na wa dhahabu, na wa fedha, na wa vitu vya thamani, na utele wa bhariri na kitani nzuri, na kila aina ya nguo ya kuvutia.

30 Na hivyo, hata katika hali yao ya akufanikiwa, hawakumfukuza yeyote aliyekuwa buchi, au walio na njaa, au walio na kiu, au wale ambao walikuwa wagonjwa, au wale ambao hawakuwa wamelishwa; na hawakuweka mioyo yao katika utajiri; kwa hivyo walikuwa wakarimu kwa wote, wote wazee kwa vijana, wote watumwa na walio huru, wote wanaume kwa wanawake, washiriki wa kanisa na wale wasio washiriki wa kanisa, bila ckuwabagua wale wote walio na shida.

31 Na hivyo walifanikiwa na wakawa matajiri zaidi ya wale ambao hawakuwa washiriki wa kanisa.

32 Kwani wale ambao hawakuwa washiriki wa kanisa walijishughulisha na uchawi, na kuabudu asanamu au buvivu, na ckusengenyana, na dwivu na kuzusha mzozo; wakivaa mavazi yaliyo ghali; ewakijiinua kwa kiburi machoni mwao; kutesana, kusema uwongo, kuiba, kupora, kufanya ukahaba, na kuua, na kila aina ya uovu; walakini, sheria ilitimizwa kwa wale wote ambao waliivunja, kwa vyovyote ilivyowezekana.

33 Na ikawa kwamba kwa kutimiza amri juu yao, kila mtu akiteseka kulingana na yale ambayo alitenda, wakawa watulivu zaidi, na hawakutenda uovu wowote ikiwa ungegunduliwa; kwa hivyo, kulikuwa na amani kuu miongoni mwa watu wa Nefi hadi mwaka wa tano wa utawala wa waamuzi.