Maandiko Matakatifu
3 Nefi 8


Mlango wa 8

Dhoruba, matetemeko, moto, vimbunga, na mchafuko wa ardhi ulishuhudia kusulubiwa kwa Kristo—Watu wengi wanaangamizwa—Giza linafunika nchi kwa muda wa siku tatu—Wale wanaosalia wanahuzunika kwa sababu ya majaliwa yao. Karibia mwaka 33–34 B.K.

1 Na sasa ikawa kwamba kulingana na maandishi yetu, na tunajua maandishi yetu kuwa ya kweli, kwani tazama, alikuwa mtu wa haki ambaye aliandika maandishi haya—kwani kweli alifanya amiujiza mingi katika bjina la Yesu; na hapakuweko na mtu yeyote ambaye angefanya miujiza katika jina la Yesu isipokuwa awe ameoshwa kila chembe kutokana na uovu wake.

2 Na sasa ikawa, kama hakukuwa na kosa lililotendwa na huyu mtu katika kuhesabu majira yetu, mwaka wa athelathini na tatu ulikuwa umepita.

3 Na watu walianza kuangalia kwa bidii kwa ishara ambayo ilitolewa na nabii Samweli, Mlamani, ndiyo, kwa wakati ambao kungekuwa na agiza kwa muda wa siku tatu usoni mwa nchi.

4 Na kulianza kuwa na mashaka makuu na ugomvi miongoni mwa watu, ingawaje aishara nyingi zilikuwa zimetolewa.

5 Na ikawa katika mwaka wa thelathini na nne, katika mwezi wa kwanza siku ya nne ya mwezi, kulitokea dhoruba kubwa, ambayo haijawahi kujulikana katika nchi yote.

6 Na kulikuwa pia tufani kubwa na ya kutisha; na kukawa na aradi ya kutisha, mpaka kwamba bilitingisha dunia yote kama karibu kupasuka mbalimbali.

7 Na kulikuwa na umeme wa nguvu sana, ambao haujajulikana katika nchi yote.

8 Na amji wa Zarahemla ulianza kuwaka moto.

9 Na mji wa Moroni ulizama kwenye kilindi cha bahari, na wakazi wake walitota.

10 Na ardhi ilifunika mji wa Moroniha, kwamba katika mahali pa mji kulitokea mlima mkubwa.

11 Na kulikuwa na uharibifu mkuu na wa kutisha katika nchi ya upande wa kusini.

12 Lakini tazama, kulikuwa na uharibifu mkubwa zaidi na wa kutisha katika nchi ya upande wa kaskazini; kwani tazama, sura ya nchi yote ilibadilika, kwa sababu ya tufani na kimbunga, na radi na umeme, na tetemeko kubwa la nchi yote.

13 Na barabara akuu zilibomoka, na barabara laini ziliharibika, na mahali pengi laini palikwaruzwa.

14 Na miji mingi iliyojulikana ailizama, na mingi ikachomwa, na mingi ilitingishwa mpaka majengo yao yakaanguka ardhini, na wakazi wa miji waliuawa, na mahali paliwachwa penye ukiwa.

15 Na kulikuwa na miji ambayo ilibaki; lakini uharibifu kwayo ulikuwa mkubwa sana, na kulikuwa na wengi ndani ya miji ambao waliuawa.

16 Na kulikuwa na wengine ambao walichukuliwa na vimbunga; na mahali walipoenda hakuna mtu anayejua, isipokuwa wanajua kwamba walipelekwa mbali.

17 Na hivyo uso wa ardhi yote uligeuzwa, kwa sababu ya tufani, na radi, na umeme, na kutingishika kwa nchi.

18 Na tazama, amiamba ilipasuka punde mbili; ilivunjika juu ya uso wa ardhi yote, mpaka kwamba ilipatikana katika vipande, kwa nyufa na mianya, juu ya uso wa nchi yote.

19 Na ikawa kwamba wakati radi, na umeme, na vimbunga, na tufani, na tetemeko la nchi vilipokwisha—kwani tazama, ulidumu muda wa masaa amatatu; na watu wengine walisema kwamba muda ulikuwa mrefu kuliko huo; walakini vitu hivi vyote vikubwa na vya kutisha vilifanyika katika muda wa masaa matatu—na kisha tazama, kulikuwa na giza juu ya nchi.

20 Na ikawa kwamba kulikuwa na giza jeusi juu ya uso wa nchi, mpaka kwamba wakazi wake ambao walikuwa hawajakufa waliweza akuhisi bukungu wa giza;

21 Na hakungekuwa na mwanga kwa sababu ya giza, wala mshumaa, wala mienge; wala hakungewashwa moto na miti yao mizuri na iliyokauka sana, ili hakungekuwa na mwanga kabisa;

22 Na hakukuonekana mwanga wowote, wala moto, wala mwanga kidogo, wala jua, wala mwezi, wala nyota, kwani ukungu wa giza ulikuwa mwingi sana ambao ulikuwa juu ya uso wa nchi.

23 Na ikawa kwamba ulidumu kwa muda wa siku atatu kwamba hakukuwa na mwanga ambao ulionekana; na kulikuwa na maombolezo makubwa na kulia kwa hasira na kilio miongoni mwa watu wote bila kikomo; ndiyo, kulikuwa na kugumia kwingi kwa watu, kwa sababu ya giza na uharibifu mkubwa ambao uliwajia.

24 Na sehemu moja walisikika wakilia wakisema: Ee kwamba kama tulikuwa tumetubu kabla ya siku hii kubwa na kutisha, na ndipo ndugu zetu wangehurumiwa, na hawangechomwa katika ule mji mkuu wa aZarahemla.

25 Na mahali pengine walisikika wakilia wakisema: Ee tunatamani kama tungekuwa tumetubu mbele ya hii siku kubwa ya kutisha, na kuwa hatungeua na kupiga manabii kwa mawe, na kuwatupa nje; hapo mama zetu na mabinti zetu warembo, na watoto wetu wangehurumiwa, na hawangezikwa katika mji wa Moroniha. Na hivyo vilio vya watu vilikuwa vikubwa na vya kuhofisha.