3 Nefi 5
iliyopita inayofuata

Mlango wa 5

Wanefi wanatubu na kuacha dhambi zao—Mormoni anaandika historia ya watu wake na kutangaza neno lisilo na mwisho kwao—Israeli itakusanywa kutoka kwenye tawanyiko lake. Karibia mwaka 22–26 B.K.

1 Na sasa tazama, hakukuwa hata nafsi moja miongoni mwa watu wote wa Wanefi ambayo ilikuwa na shaka hata kidogo katika maneno ya manabii watakatifu ambao walizungumza; kwani walijua kwamba ilikuwa muhimu kwamba yatimizwe.

2 Na walijua kwamba ni muhimu kwamba Kristo alikuwa amekuja, kwa sababu ya ishara nyingi ambazo zilikuwa zimetolewa kulingana na maneno ya manabii; na kwa sababu ya vitu ambavyo vilikuwa vimetimizwa kitambo walijua kwamba ilikuwa muhimu kwamba vitu vyote vitimizwe kulingana na yale ambayo yalikuwa yamezungumzwa.

3 Kwa hivyo waliacha dhambi zao zote, na machukizo yao, na ukahaba wao, na walimtumikia Mungu kwa bidii yote mchana na usiku.

4 Na sasa ikawa kwamba wakati walikuwa wamechukua wanyangʼanyi wote kama wafungwa, mpaka kwamba hakuna aliyetoroka ambaye hakuuawa, waliwatupa wafungwa wao gerezani, na wakasababisha neno la Mungu kuhubiriwa kwao; na kadiri wengi walipotubu dhambi zao na kufanya agano kwamba hawataua tena waliachiliwa ahuru.

5 Lakini kadiri kulipokuwa na wengi ambao hawakufanya agano, na ambao waliendelea na mauaji ya siri mioyoni mwao, ndiyo, vile wengi walipatikana wakitoa vitisho kwa ndugu zao walihukumiwa na kuadhibiwa kulingana na sheria.

6 Na hivyo walimaliza yale maovu yote, na siri, na mashirika ya machukizo, ambamo kwake kulikuwa na maovu mengi sana, na kutendeka kwa mauaji mengi.

7 Na hivyo mwaka wa aishirini na mbili ulikuwa umepita, na mwaka wa ishirini na tatu pia, na wa ishirini na nne, na wa ishirini na tano; na hivyo miaka ishirini na tano ilipita.

8 Na vitu vingi vilikuwa vimetendeka ambavyo, kwa maoni ya watu kadhaa, vilikuwa vikubwa na vya kushangaza; walakini, vyote haviwezi kuandikwa kwenye kitabu hiki; ndiyo, kitabu hiki hakiwezi kutosha hata sehemu moja ya amia ya yale yaliyofanyika miongoni mwa watu wengi hivyo kwa muda wa miaka ishirini na tano.

9 Lakini tazama kuna amaandishi ambayo yana mambo yote ya hawa watu; na taarifa fupi zaidi na ya kweli ilitolewa na Nefi.

10 Kwa hivyo nimetengeneza maandishi yangu ya vitu hivi kulingana na kumbukumbu ya Nefi, ambayo ilichorwa kwenye mabamba ambayo yaliitwa mabamba ya Nefi.

11 Na tazama, ninatengeneza maandishi kwenye mabamba ambayo nimeunda kwa mikono yangu mwenyewe.

12 Na tazama, ninaitwa aMormoni, nikiitwa kufuatana na bnchi ya Mormoni, nchi ambamo Alma alianzisha kanisa miongoni mwa watu, ndiyo, kanisa la kwanza ambalo lilianzishwa miongoni mwao baada ya uhalifu wao.

13 Tazama, mimi ni mwanafunzi wa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Nimeitwa na yeye kutangaza neno lake miongoni mwa watu wake, ili wawe na maisha yasiyo na mwisho.

14 Na imekuwa muhimu kwamba mimi, kwa kutii mapenzi ya Mungu, kwamba sala za wale ambao wameenda mbele, ambao walikuwa watakatifu, sharti itatimizwa kulingana na imani yao, niandike amaandishi ya vitu hivi ambavyo vimefanywa—

15 Ndiyo, maandishi madogo ya yale mambo ambayo yamefanyika kutoka wakati ambao Lehi aliondoka Yerusalemu, hata chini mpaka wakati huu.

16 Kwa hivyo nitatengeneza maandishi yangu kutoka kwa kumbukumbu ambazo zilitolewa na wale ambao walikuwa mbele yangu, hadi mwanzo wa maisha yangu;

17 Na ndipo nafanya amaandishi haya ya vitu ambavyo nimeona kwa macho yangu.

18 Na ninajua maandishi ninayoandika kuwa ya haki na ya kweli; walakini kuna vitu vingi ambavyo, kwa sababu ya lugha yetu, hatuwezi akuviandika.

19 Na sasa ninamaliza kuzungumza, juu yangu mwenyewe, na nitaendelea kutoa historia yangu ya vitu ambavyo vimefanyika mbele yangu.

20 Mimi ni Mormoni, na ni wa kizazi cha Lehi kamili. Ninayo sababu ya kumsifu Mungu wangu na Mwokozi wangu Yesu Kristo, kwamba aliwaleta babu zetu kutoka nchi ya Yerusalemu, (na ahakuna yeyote aliyeijua isipokuwa yeye tu na wale ambao aliwaleta kutoka nchi hiyo) na kwamba amenipatia mimi na watu wangu elimu nyingi katika wokovu wa nafsi zetu.

21 Kwa kweli ameibariki anyumba ya bYakobo, na amekuwa na churuma kwa uzao wa Yusufu.

22 Na aikiwa vile uzao wa Lehi umetii amri zake amewabariki na kuwasaidia kufanikiwa kulingana na neno lake.

23 Ndiyo, na kwa kweli ataleta abaki la uzao wa Yusufu bkuwaelemisha kuhusu Bwana Mungu wao.

24 Na kwa kweli kadiri Bwana anavyoishi, aatakusanya ndani kutoka katika pembe nne za dunia baki lote la uzao wa Yakobo, ambao wametawanyika ugenini kote usoni mwa nchi.

25 Na vile amefanya agano na nyumba yote ya Yakobo, hivyo hivyo agano ambalo amefanya na nyumba ya Yakobo litatimizwa kwa wakati wake mwenyewe, kwa akurudisha nyumba yote ya Yakobo kwenye ujuzi wa agano ambalo amefanya nao.

26 Na hapo ndipo awatajua Mkombozi wao, ambaye ni Yesu Kristo, Mwana wa Mungu; na ndipo watakusanywa kutoka pembe nne za dunia hadi kwenye nchi zao, kutoka ambapo walitawanywa; ndiyo, kadiri Bwana aishivyo ndivyo itakavyokuwa. Amina.