Maandiko Matakatifu
3 Nefi 29


Mlango wa 29

Ujio wa Kitabu cha Mormoni ni ishara kwamba Bwana ameanza kukusanya Israeli na kutimiza maagano Yake—Wale ambao wanakana mafunuo Yake ya siku za mwisho na zawadi watalaaniwa. Karibia mwaka 34–35 B.K.

1 Na sasa tazama, nawaambia kwamba wakati Bwana atakapoona sawa katika hekima yake, kwamba maneno haya ayatawajia Wayunani kulingana na neno lake, ndipo mtajua kwamba bagano ambalo Baba amefanya na wana wa Israeli, kuhusu kurudi kwao kwenye nchi zao za urithi, kitambo imeanza kutimizwa.

2 Na mtajua kwamba maneno ya Bwana, ambayo yamezungumzwa na manabii watakatifu, yote yatatimizwa; na hamtahitajika kusema kwamba Bwana aanachelewesha kuja kwake kwa wana wa Israeli.

3 Na hamtakikani kuwaza katika mioyo yenu kwamba maneno ambayo yamezungumzwa ni ya bure, kwani tazama, Bwana atakumbuka agano lake ambalo amefanya kwa watu wake wa nyumba ya Israeli.

4 Na wakati mtakapoona maneno haya yakitokea miongoni mwenu, hamtahitaji tena kudharau mwenendo wa Bwana, kwani aupanga wake wa bhaki uko ndani ya mkono wake wa kulia; na tazama, katika siku ile, ikiwa mtakataa kwa madharau, vitendo vyake, ndipo atasababisha kwamba haraka mtapitwa.

5 aOle kwake ambaye bhukataa vitendo vya Bwana; ndiyo, ole kwake ambaye catakataa Kristo na matendo yake!

6 Ndiyo, aole kwa yule ambaye atakataa mafunuo ya Bwana, na ambaye atasema kuwa Bwana hafanyi kazi tena kwa kufunua au unabii, au kwa bkarama, au kwa lugha au kwa kuponya, au kwa uwezo wa Roho Mtakatifu!

7 Ndiyo, na ole kwa yule atakayesema katika ile siku, kupata afaida, kwamba bhakuwezi kufanyika miujiza na Yesu Kristo; kwani yule atakayefanya hivi atakuwa cmwana wa upotevu, ambaye kwake hakukuwa na huruma kulingana na neno la Kristo!

8 Ndiyo, na hamhitaji tena akufyonya, wala bkudharau, wala kuchezea cWayahudi, wala baki lolote la nyumba ya Israeli; kwani tazama, Bwana hukumbuka agano lake kwao, na atawafanyia kulingana na yale ambayo ameapa.

9 Kwa hivyo hampaswi kudhani kwamba mnaweza kugeuza mkono wa kulia wa Bwana hadi kushoto, ili asifanye hukumu yake kwa kutimiza lile agano ambalo amefanya kwa nyumba ya Israeli.