Maandiko Matakatifu
3 Nefi 12


Mlango wa 12

Yesu awaita na kuwapa mamlaka wale wanafunzi kumi na wawili—Anatoa hotuba kwa Wanefi sawa sawa na Mahubiri ya Mlimani—Yeye anazungumzia sifa za Heri—Mafundisho Yake yanapita na yanatangulia juu ya sheria za Musa—Watu wanaamriwa kuwa wakamilifu kama vile Yeye na Baba Yake walivyo wakamilifu—Linganisha na Mathayo 5. Karibia mwaka 34 B.K.

1 Na ikawa kwamba wakati Yesu alikuwa amesema maneno haya kwa Nefi, na kwa wale ambao walipokuwa wameitwa, (sasa idadi ya wale ambao walikuwa wameitwa na kupokea uwezo na mamlaka ya kubatiza, ilikuwa akumi na wawili) na tazama, alinyoosha mkono wake mbele kwa umati, na kuwaambia kwa sauti kubwa akisema: bHeri ninyi ikiwa mtasikiliza maneno ya hawa kumi na wawili ambao cnimewachagua kutoka miongoni mwenu kuwahudumia, na kuwa watumishi wenu; na kwao nimewatolea uwezo kwamba wangewabatiza na maji; na baada ya hayo kwamba mmebatizwa na maji, tazama nitawabatiza kwa moto na Roho Mtakatifu; kwa hivyo heri ninyi ikiwa mtaamini katika mimi na mbatizwe, baada ya kuniona na kujua kwamba ni mimi.

2 Na tena wana heri nyingi wale ambao awataamini kwa maneno haya yenu kwa sababu mtashuhudia kwamba mmeniona, na kwamba mnajua kwamba ni mimi. Ndiyo, heri kwa wale ambao wataamini katika maneno yenu, na kujileta bchini kwenye unyenyekevu na kubatizwa, kwani watatembelewa cna moto na Roho Mtakatifu na watasamehewa dhambi zao.

3 Ndiyo, heri wale walio amaskini rohoni, ambao bwanakuja kwangu, kwani ufalme wa mbinguni ni wao.

4 Na tena heri wote walio na huzuni kwani watafarijika.

5 Na heri walio awapole kwani watarithi bdunia.

6 Na heri wale wote walio na anjaa na kuwa na bkiu kwa ajili ya chaki, kwani watashibishwa na Roho Mtakatifu.

7 Na heri walio na arehema kwani watapata rehema.

8 Na heri wote walio na moyo amweupe, kwani bwatamwona Mungu.

9 Na heri wote walio awapatanishi, kwani wataitwa bwatoto wa Mungu.

10 Na heri wale wote awanaodhulumiwa kwa ajili ya jina langu kwani ufalme wa mbinguni ni wao.

11 Na heri ninyi, wakati watu watawatukana na kuwadhulumu, na watasema aina yoyote ya uovu dhidi yenu bila ukweli kwa ajili yangu;

12 Kwani mtakuwa na shangwe kubwa na mtakuwa wachangamfu kupita kiasi, kwani athawabu yenu itakuwa kubwa mbinguni; kwani hivyo ndivyo walidhulumu hao manabii ambao walikuweko mbele yenu.

13 Amin, amin, nawaambia, ninawapatia muwe achumvi ya dunia; lakini ikiwa chumvi itapoteza ladha yake, dunia itatiwa chumvi na nini? Chumvi kutokea hapo haitakuwa na uzuri wowote lakini itatupwa na kukanyagwa na miguu ya watu.

14 Amin, amin, ninawaambia, ninawapatia muwe nuru ya watu hawa. Mji uliojengwa kwenye kilima hauwezi kufichwa.

15 Tazama, je, watu huwasha amshumaa na kuuweka chini ya pishi? La, lakini kwenye kinara cha mshumaa na humulika mwanga kwa wote walio ndani ya nyumba;

16 Kwa hivyo acha anuru yenu iangae mbele ya hawa watu, ili wapate kuyaona matendo yenu, na kumtukuza Baba yenu aliye mbinguni.

17 Msifikirie kwamba nimekuja kuharibu sheria au manabii. Sikuja kuharibu bali kutimiza;

18 Kwani amin ninawaambia, nukta moja wala chembe moja haijaondoka kutoka kwa asheria, lakini ndani yangu yote imetimizwa.

19 Na tazama, nimewapatia sheria na amri za Baba yangu, kwamba mtaamini ndani yangu, na kwamba mtatubu dhambi zenu, na mje kwangu na amoyo uliopondeka na roho iliyovunjika. Tazama, mnazo amri mbele yenu, na bsheria imetimizwa.

20 Kwa hivyo njooni kwangu na mwokolewe; kwani amin nawaambia kwamba isipokuwa mtii amri zangu ambazo nimewaamuru wakati huu, kwa njia yoyote hamtaingia katika ufalme wa mbinguni.

21 Mmesikia kwamba ilisemekana na wale wa wakati wa kale, na pia imeandikwa mbele yenu, kwamba ausiue, na yeyote atakayeua atakuwa hatarini mwa hukumu ya Mungu;

22 Lakini ninawaambia kwamba, yeyote aliye na hasira na ndugu yake atakuwa hatarini ya hukumu yake. Na yeyote atakayesema kwa ndugu yake, Raka, atakuwa hatarini na baraza; na yeyote atakayesema, Wewe mjinga, atakuwa hatarini na moto wa jehanamu.

23 Kwa hivyo ikiwa utakuja kwangu, au utatamani kuja kwangu, na ukumbuke kwamba ndugu yako anacho kitu dhidi yako—

24 Nenda njia yako kwa ndugu yako, na kwanza aondoa tofauti na ndugu yako, na hapo uje kwangu, na moyo wa lengo moja na nitakupokea.

25 Kubaliana na adui yako haraka, wakati uko katika njia moja na yeye, asije akupate wakati wowote na kukutupa gerezani.

26 Amin, amin, nakwambia hutatoka humo kamwe mpaka utakapolipa senti ya mwisho. Na wakati ungali upo gerezani unaweza kulipa hata asenti moja? Amin, amin, nakwambia, La.

27 Tazama, imeandikwa na wale wa kale, kwamba usifanye auzinzi.

28 Lakini ninawaambia kwamba, yeyote ambaye anamchungulia mwanamke akumtamani, huwa tayari amezini moyoni mwake.

29 Tazama, ninakupatia amri ili usikubali vitu hivi kuingia amoyoni mwako.

30 Kwani inawafaa kwamba mjizuie wenyewe hivi vitu, ambapo mtajitwika amsalaba wenu, kuliko kwamba mtupwe jehanamu.

31 Imeandikwa kwamba yeyote atakayempatia mke wake talaka, ampe cheti cha atalaka.

32 Amin, amin, nawaambia, kwamba yeyote atakayempatia mke wake atalaka, isipokuwa kwa sababu ya buasherati, humsababisha kutenda cuzinzi na yeyote atakayemwoa yule ambaye amepewa talaka anatenda uzinzi.

33 Na tena imeandikwa, na wale wa kale kwamba hutaapa uwongo mwenyewe, lakini utadhihirisha kwa Bwana aviapo vyako;

34 Lakini amin, amin ninawaambia, ausiape kabisa; wala kwa mbingu, kwani ni kiti cha enzi cha Mungu;

35 Wala kwa dunia, kwani ndipo mahali pa kuweka miguu yake;

36 Wala hutaapa kwa kichwa chako, kwani huwezi kutengeneza unywele wako mmoja kuwa mweusi au mweupe;

37 Lakini acha maongezi yenu yawe Ndiyo, ndiyo; La, la; kwani chochote kilicho zaidi ya haya ni ovu.

38 Na tazama, imeandikwa, jicho kwa ajicho, na jino kwa jino;

39 Lakini ninawaambia kwamba ahamtashindana na uovu, lakini yeyote atakayekupiga katika shavu la kulia, bmgeuzie upande mwingine pia;

40 Na ikiwa mtu yeyote atakushtaki mahakamani na achukue koti lako, mwachie achukue joho lako pia;

41 Na yeyote atakayekulazimisha kwenda maili moja, nenda na yeye mbili.

42 aMpatie akuombaye, na atakayekukopa kwako usimfukuze.

43 Na tazama, imeandikwa pia na wale wa kale kwamba, utampenda jirani yako na umchukie adui wako;

44 Lakini tazama ninawaambia, wapendeni amaadui zenu, wabariki wanao walaani, wafanyie mazuri wale ambao wanawachukia, na bmuwaombee wale ambao wanawatumia kwa madharau na kuwadhulumu;

45 Ili muwe watoto wa Baba yenu aliye mbinguni; kwani yeye husababisha jua kungʼaa kwa waovu na kwa wenye haki.

46 Kwa hivyo vitu ambavyo vilikuwa vya kale, ambavyo vilikuwa chini ya sheria, vyote vimetimia.

47 Vitu vya akale vimeachwa na vitu vyote vimekuwa vipya.

48 Kwa hivyo ningependa kwamba mngekuwa awakamilifu hata kama nilivyo, au Baba yenu ambaye yuko mbinguni ni mkamilifu.