Maandiko Matakatifu
2 Nefi 33


Mlango wa 33

Maneno ya Nefi ni ya kweli—Yanamshuhudia Kristo—Wale ambao wanamwamini Kristo wataamini maneno ya Nefi, ambayo yatasimama kama shahidi mbele ya baraza la hukumu. Karibia mwaka 559–545 K.K.

1 Na sasa mimi, Nefi, siwezi kuandika vitu vyote ambavyo vilifundishwa miongoni mwa watu wangu; wala mimi sio ashujaa kwa kuandika, kama nilivyo katika mazungumzo; kwani mwanadamu banapozungumza kwa uwezo wa Roho Mtakatifu uwezo wa Roho Mtakatifu huyapeleka katika mioyo ya watoto wa watu.

2 Lakini tazama, kuna wengi awanaoshupaza mioyo yao dhidi ya Roho Mtakatifu, kwamba hana nafasi ndani yao; kwa hivyo, wanatupa vitu vingi ambavyo vimeandikwa na kuvichukua kama vitu visivyofaa.

3 Lakini mimi, Nefi, nimeandika yale ambayo nimeandika, na kuyachukua kuwa yenye athamani kuu, na zaidi kwa watu wangu. Kwani bnawaombea siku zote kwa mchana, na macho yangu huitia mto maji usiku, kwa sababu yao; na ninamlilia Mungu wangu kwa imani, na ninajua kwamba atasikia kilio changu.

4 Na ninajua kwamba Bwana Mungu ataweka wakfu sala zangu kwa faidha ya watu wangu. Na maneno ambayo nimeandika kwa unyonge yatatiwa anguvu kwao; kwani binawashawishi kutenda mema; inawafahamisha wao kuhusu babu zao; na inazungumza kuhusu Yesu, na kuwashawishi kumwamini, na kuvumilia hadi mwisho, ambao ni uzima wa cmilele.

5 Na inazungumza kwa aukali dhidi ya dhambi, kulingana na vile ukweli ulivyo bwazi; kwa hivyo, hakuna mtu yeyote atakayekasirikia maneno ambayo nimeandika ila tu awe na roho ya ibilisi.

6 Nafurahia kwa uwazi; nafurahia ukweli; namfurahia Yesu wangu, kwani aameikomboa nafsi yangu kutoka jehanamu.

7 Nina ahisani kwa watu wangu, na imani kuu katika Kristo kwamba nitakutana na nafsi nyingi zisizokuwa na mawaa katika kiti chake cha hukumu.

8 Nina hisani kwa Myahudi—nasema aMyahudi, kwa sababu nina maana kwamba nilitoka huko.

9 Na pia nina hisani kwa aWayunani. Lakini tazama, siwezi kuwatumainia ila tu wao bwapatanishwe na Kristo, na kuingia katika lile lango cjembamba, na dwatembee katika njia ile eiliyosonga inayoelekeza uzima wa milele, na waendelee katika njia hiyo hadi mwisho wa siku ya majaribio.

10 Na sasa, ndugu zangu wapendwa, na pia Myahudi, na ninyi nyote mlio pande zote za ulimwengu, sikilizeni maneno haya na mwamini katika Kristo; na kama hamwamini katika maneno haya aaminini katika Kristo. Na kama mtamwamini Kristo mtaamini katika bmaneno haya, kwani ni cmaneno ya Kristo, na ameyapatia kwangu; na dyanafundisha wanadamu wote kwamba wafanye mema.

11 Na kama sio maneno ya Kristo, amueni ninyi—kwani Kristo atawaonyesha, kwa auwezo na utukufu mkuu, kwamba ni maneno yake, katika siku ya mwisho; na wewe na mimi btutasimama uso kwa uso kwenye baraza lake; na utajua kwamba nimeamriwa na yeye kuandika vitu hivi, ingawa mimi ni mnyonge.

12 Na ninamuomba Baba kwa jina la Kristo kwamba wengi wetu, kama sio wote, waokolewe katika aufalme wake siku ile kuu ya mwisho.

13 Na sasa, ndugu zangu wapendwa, wale wote ambao ni wa nyumba ya Israeli, na nyote hadi mwisho wa ulimwengu, nawazungumzia kama sauti ainayolia kutoka mavumbini: Kwa herini hadi siku ile kuu itakapofika.

14 Na wewe usiyekubali kupokea wema wa Mungu, na kuheshimu maneno ya Wayahudi, na pia amaneno yangu, na bmaneno yatakayotoka kutoka kinywa cha Mwanakondoo wa Mungu, tazama, nakupigia kwaheri isiyo na mwisho, kwani maneno haya cyatakuhukumu siku ya mwisho.

15 Kwani yale ambayo ninayatia muhuri duniani, yataletwa dhidi yako katika baraza la ahukumu; kwani Bwana ameniamuru hivi, na ni lazima nitii. Amina.