Maandiko Matakatifu
2 Nefi 21


Mlango wa 21

Shina la Yese (Kristo) litahukumu kwa haki—Elimu ya Mungu itafunika dunia katika Milenia—Bwana atainua bendera na kukusanya Israeli—Linganisha Isaya 11. Karibia mwaka 559–545 K.K.

1 Na patatokea mbele afimbo kutoka bShina la cYese, na tawi litamea kutoka mizizi yake.

2 Na aRoho wa Bwana itakuwa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya mashauri na uwezo, roho ya elimu na ya kumcha Bwana;

3 Na atamsababisha aweze kufahamu kwa haraka katika kumcha Bwana; na ahatahukumu kulingana na maono ya macho yake, wala kukemea kulingana na kusikia kwa masikio yake.

4 Lakini kwa ahaki atahukumu walio maskini, na bakemee kwa adili walio cwanyenyekevu wa dunia; na ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua walio waovu.

5 Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa amafigo yake.

6 Pia mbwa-mwitu ataishi na mwanakondoo, na chui atalala na mwana mbuzi, na ndama na mwana simba na ngʼombe mnono pamoja; na mtoto mchanga atawaongoza.

7 Na ngʼombe na dubu watakula pamoja; watoto wao watalala chini pamoja; na simba atakula majani kama ngʼombe.

8 Na mtoto anayenyonya atacheza kwenye tundu la anyoka, na mtoto aliyeachishwa kunyonya atatia mkono wake kwenye pango la bfira.

9 aHawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu wote mtakatifu, kwani dunia yote itajaa belimu ya Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari.

10 Na katika asiku ile kutakuwa na bmzizi wa Yese, ambao utasimama kama bendera ya watu; na cWayunani dwatautafuta; na pumziko lake litakuwa takatifu.

11 Na itakuwa kwamba katika siku ile Bwana atanyoosha mkono wake tena mara ya apili kurudisha baki la watu wake litakalobaki, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari.

12 Na atawainulia mataifa abendera, na kuwakusanya watu wa Israeli bwaliofukuzwa, na ckuwakusanya pamoja wale waliotawanywa wa Yuda kutoka pembe nne za dunia.

13 Na awivu wa Efraimu pia utaondoka, na maadui wa Yuda watatengwa; bEfraimu hatamwonea wivu cYuda, na Yuda hatamuudhi Efraimu.

14 Lakini wao awatashambulia juu ya mabega ya Wafilisti kuelekea upande wa magharibi; watawapora wale kutoka mashariki pamoja; watainyooshea Edomu na Moabu mkono wao; na watoto wa Amoni watawatii.

15 Na Bwana aatauangamiza ulimi wa bahari ya Misri; na kwa upepo wake mkali atatingisha mkono wake juu ya mto, na kuugawanya uwe vijito saba, na kuwavusha watu kwa miguu mikavu.

16 Na kutakuwa abarabara kuu kwa baki la watu wake waliosalia, kutoka Ashuru, kama vile ilivyokuwa katika Israeli katika siku ile waliyotoka nje ya nchi ya Misri.