Maandiko Matakatifu
2 Nefi 13


Mlango wa 13

Yuda na Yerusalemu zitaadhibiwa kwa sababu ya maasi yao—Bwana hutetea na huhukumu watu Wake—Mabinti wa Sayuni wanalaaniwa na kusumbuliwa kwa sababu ya kupenda anasa—Linganisha Isaya 3. Karibia mwaka 559–545 K.K.

1 Kwani tazama, Bwana, Bwana wa Majeshi, huondoa kutoka Yerusalemu, na Yuda, kijiti na bakora, bakora yote ya mkate, na kijiti chote cha maji—

2 Mwanadamu aliye shujaa, na mwanadamu aliye wa vita, mwamuzi, na nabii, na aliye na hekima, na mzee;

3 Kapteni wa wanajeshi hamsini, na yule anayeheshimika, na mshauri, na mganga mwerevu, na mzungumzaji shujaa.

4 Na nitawapatia watoto kuwa wafalme wao, na watoto wachanga watawatawala.

5 Na watu watadhulumiwa, kila mmoja na mwingine, na kila mmoja na jirani yake; watoto watajivunia wazee, na mshenzi kwa anayeheshimika.

6 Wakati mtu atamkumbatia kaka yake wa nyumba ya baba yake, na kusema: Wewe unayo mavazi, kuwa kiongozi wetu, na usikubali haya amaangamizo kushukia kwa mkono wako—

7 Katika siku ile ataapa, akisema: Mimi sitakuwa amponyaji; kwani nyumbani mwangu hamna mkate wala mavazi; msinifanye kiongozi wa watu.

8 Kwani Yerusalemu aimeangamizwa, na Yuda bimeanguka, kwa sababu ndimi zao na matendo yao yamekuwa kinyume cha Bwana, kwa kuchokoza utukufu wa macho yake.

9 Umbo la nyuso zao linashuhudia dhidi yao, na kutangaza kwamba dhambi yao ni kama ya aSodoma, na hawawezi kuificha. Ole kwa nafsi zao, kwani wamejilipiza kwa uovu!

10 Waambieni walio haki kwamba wako asalama; kwani watakula matunda ya matendo yao.

11 Ole kwa wale walio waovu, kwani wataangamia; kwani malipo ya mikono yao yatakuwa juu yao!

12 Na watu wangu, wanadhulumiwa na watoto, na kutawaliwa na wanawake. Ee watu wangu, wale awanaowaongoza wanawasababisha kukosa na kuangamiza njia ya mapito yenu.

13 Bwana husimama akuwatetea, na husimama kuhukumu watu.

14 Bwana atawahukumu wazee wa watu wake na wana wa awafalme wao; kwani bmmekula shamba la cmizabibu na dmali ya emaskini nyumbani mwenu.

15 Mnamaanisha nini? Mnawapiga watu wangu kuwa vipande, na kusaga nyuso za maskini, asema Bwana Mungu wa Majeshi.

16 Zaidi ya hayo, Bwana asema: Kwa sababu mabinti za Sayuni wanaringa, na kutembea na shingo mbele na macho ya tamaa, na mwendo wa akiburi, na kuliza sauti ya njuga kwa miguu yao—

17 Kwa hivyo Bwana atachapa kipaji cha mabinti za Sayuni, kwa kigaga, na Bwana aatagundua sehemu zao za siri.

18 Na katika siku ile Bwana ataondoa urembo wa pambo zao, na akofia zao zilizoshonwa, na ushanga na bduara ya mviringo kama mwezi.

19 Mikufu na bangili, na abuibui za vito;

20 Kofia, na mavazi ya miguu, na vitambaa vya kichwa, na marashi, na vipuli vya masikio;

21 Na pete, na vipuli vya pua;

22 Na amavazi mengi mazuri, na kanzu, na shali, na vibeti;

23 Na avioo, na kitani dhaifu, na shela, na setiri.

24 Na itakuwa kwamba, badala ya kunukia utamu kutakuwa na uvundo; na badala ya mshipi, akiraka; na badala ya nywele, upara; na badala ya bnguo nzuri, mshipi wa gunia; ckuchomeka badala ya urembo.

25 Wanaume wako wataanguka kwa upanga na mashujaa wako kwa vita.

26 Na milango yake italia na kuomboleza; na atakuwa na ukiwa, na atakaa ardhini.

      • EBR ufungaji (wa jeraha); m.y., siwezi kutatua matatizo yako.

      • MY kutembea kwa hatua fupi, za haraka haraka katika namna ya uongo.

      • EBR fichua; msemo unaomaanisha “kuwaabisha.”

      • Yawezekana wavu wa kufungia nywele. Wataalamu hawakubaliana mara zote kuhusu asili ya mapambo ya kike yaliyoorodheshwa katika aya ya 18–23.

      • MY mapambo yaliyo na umbo kama la mwezi mwandamo.

      • EBR shela.

      • EBR mavazi ya kupendeza.

      • AU mavazi yenye kuangaza.

      • EBR nguo chakavu.

      • AU joho.

      • AU mhuri (ishara ya utumwa).