Maandiko
1 Nefi 9


Mlango wa 9

Nefi anaandika aina mbili za historia—Kila kimoja kinaitwa mabamba ya Nefi—Mabamba makubwa yanayo maandishi ya historia ya kiulimwengu; mabamba ndogo yanayo asili ya vitu vitakatifu. Karibia mwaka 600–592 K.K.

1 Na baba yangu aliona vitu hivi vyote, na kusikia, na kuvizungumza, alipokuwa kwenye hema, katika abonde la Lemueli, na pia vitu vingi zaidi, ambavyo haviwezi kuandikwa kwenye mabamba haya.

2 Na sasa, kama nilivyosema kuhusu mabamba haya, tazama sio yale mabamba ambayo nimeyaandika historia kamili ya watu wangu; kwani amabamba ambayo nimeandika historia kamili ya watu wangu nimeyaita kwa jina la Nefi; kwa hivyo, yanaitwa mabamba ya Nefi, kufuatana na jina langu; na pia mabamba haya yanaitwa mabamba ya Nefi.

3 Walakini, nimepokea amri ya Bwana kwamba niyatengeneze mabamba haya kwa akusudi muhimu kwamba kuweko na historia iliyochorwa ya bhuduma ya watu wangu.

4 Kwenye yale mabamba mengine ichorwe historia ya utawala wa wafalme, na vita na mabishano ya watu wangu; kwa hivyo mabamba haya sehemu kubwa ni ya huduma; na yale amabamba mengine sehemu kubwa ni ya utawala wa wafalme na vita na pia mabishano ya watu wangu.

5 Kwa hivyo, Bwana ameniamuru kuandika mabamba haya kwa kusudi lake lenye ahekima, ambalo kusudi mimi silijui.

6 Lakini Bwana aanavijua vitu vyote kuanzia mwanzoni; kwa hivyo, anatayarisha njia ya kutimiza kazi zake zote miongoni mwa watoto wa watu; kwani tazama, ana buwezo wote wa kutimiza maneno yake yote. Na hivyo ndivyo ilivyo. Amina.