Maandiko
1 Nefi 5
iliyopita inayofuata

Mlango wa 5

Saria anamnungʼunikia Lehi—Wote wawili wanashangilia kurudi kwa wana wao—Wanatoa dhabihu—Mabamba ya shaba nyeupe yana maandiko ya Musa na manabii wengine—Mabamba yanamtambulisha Lehi kuwa uzao wa Yusufu—Lehi anatoa unabii kuhusu uzao wake na kuhifadhiwa kwa mabamba. Karibia mwaka 600–592 K.K.

1 Na ikawa kwamba baada ya sisi kufika nyikani kwa baba yetu, tazama, alijazwa na shangwe, na pia mama yangu, aSaria, alifurahi sana, kwani alikuwa ameomboleza kwa sababu yetu.

2 Kwani alikuwa amedhani kwamba tulikuwa tumeangamia nyikani; na pia alikuwa amemlalamikia baba yangu, akimwambia kwamba yeye ni mtu wa maono; na kusema: Tazama wewe umetuongoza kutoka nchi yetu ya urithi, na wana wangu hawapo tena, na tunaangamia nyikani.

3 Na kwa lugha ya aina hii mama yangu alimlalamikia baba yangu.

4 Na ikawa kwamba baba yangu akamzungumzia, na kusema: Najua kwamba mimi ni amtu wa maono; kwani kama nisingeona vitu vya Mungu katika bmaono nisingejua wema wa Mungu, lakini ningekaa huko Yerusalemu, na kuangamia pamoja na ndugu zangu.

5 Lakini tazama, nimepokea uthibitisho wa anchi ya ahadi, vitu ambavyo kwavyo ninafurahia; ndiyo, na bninajua kwamba Bwana atawakomboa wana wangu kutoka mikononi mwa Labani, na kuwaleta hapa kwetu nyikani.

6 Na kwa lugha ya aina hii baba yangu, Lehi, alimfariji mama yangu, Saria, kutuhusu, tulipokuwa tukisafiri kutoka nyikani hadi nchi ya Yerusalemu, kuchukua maandishi ya Wayahudi.

7 Na tulipokuwa tumerudi kwenye hema la baba yangu, tazama shangwe yao ilikuwa tele, na mama yangu akafarijika.

8 Na mama yangu akazungumza, akisema: Sasa najua kwa hakika kwamba Bwana aamemwamuru mume wangu kutorokea nyikani; ndiyo, na pia najua kwa hakika kwamba Bwana amewalinda wana wangu, na kuwakomboa kutoka mikononi mwa Labani, na kuwapatia uwezo wa bkutimiza kitu ambacho Bwana aliwaamuru. Na hii ndiyo lugha ambayo mama yangu alitumia.

9 Na ikawa kwamba walishangilia sana, na wakamtolea Bwana adhabihu za kuteketezwa kwa moto pamoja na sadaka; na bkumshukuru Mungu wa Israeli.

10 Na baada ya kumshukuru Mungu wa Israeli, baba yangu, Lehi, alichukua zile kumbukumbu ambazo zilikuwa zimechorwa kwenye amabamba ya shaba nyeupe, na aliyapekua tangu mwanzo.

11 Na akagundua kwamba yalikuwa na avitabu vitano vya Musa, ambavyo vilieleza historia ya kuumbwa kwa dunia, na pia kwa Adamu na Hawa, ambao ndiyo wazazi wetu wa kwanza;

12 Na pia amaandishi ya Wayahudi kutoka mwanzo, hadi mwanzo wa utawala wa Zedekia, mfalme wa Yuda;

13 Na pia unabii wa manabii watakatifu, tangu mwanzo, hadi mwanzoni mwa utawala wa aZedekia; na pia unabii mwingi ambao ulizungumzwa kutoka kinywa cha bYeremia.

14 Na ikawa kwamba baba yangu, Lehi, pia alipata kwenye amabamba ya shaba nyeupe nasaba ya babu zake; kwa hivyo akajua kwamba yeye ni wa kizazi cha Yusufu; ndiyo, hata yule bYusufu, ambaye alikuwa mwana wa cYakobo, ambaye daliuzwa Misri, na ambaye ealihifadhiwa kwa mkono wa Bwana, ili amhifadhi baba yake, Yakobo, na wote wa jamii yake wasiangamie kwa njaa.

15 Na awaliongozwa pia kutoka utumwani na kutoka nchi ya Misri, na yule Mungu ambaye alikuwa amewahifadhi.

16 Na hivyo baba yangu, Lehi, aligundua nasaba ya baba zake. Na Labani pia alikuwa kizazi cha aYusufu, ndipo yeye na baba zake wakaweka yale maandishi.

17 Na sasa baba yangu alipoona vitu hivi vyote, alijawa na Roho, na akaanza kutoa unabii kuhusu uzao wake—

18 Kwamba mabamba haya ya shaba nyeupe yanapaswa kupelekwa katika mataifa yote, makabila zote, lugha zote, na watu wote wa uzao wake.

19 Kwa hivyo, alisema kwamba mabamba haya ya shaba nyeupe yasiangamie akamwe; wala yasichakazwe na wakati. Na akatoa unabii wa vitu vingi kuhusu uzao wake.

20 Na ikawa kwamba mpaka hapo mimi na baba yangu tulikuwa tumeweka amri ambazo Bwana alikuwa ametuamuru.

21 Na tulikuwa tumepata yale maandishi ambayo Bwana alikuwa ametuamuru, na kuyachunguza na tukagundua kwamba yalikuwa ya kupendeza; ndiyo, hata yenye athamani kubwa kwetu sisi, kwani tungeweza bkuhifadhi amri za Bwana na kuwapa watoto wetu.

22 Kwa hivyo, ilikuwa ni hekima katika Bwana kwamba tuyabebe tulipokuwa, tukisafiri nyikani tukielekea nchi ya ahadi.