Maandiko Matakatifu
1 Nefi 11


Mlango wa 11

Nefi anaona Roho wa Bwana na anaonyeshwa kwa ono mti wa uzima—Anamuona mama wa Mwana wa Mungu na kufahamu kuhusu ufadhili wa Mungu—Anaona ubatizo, huduma, na kusulibiwa kwa Mwanakondoo wa Mungu—Pia anaona mwito na huduma ya Mitume Kumi na Wawili wa Mwanakondoo. Karibia mwaka 600–592 K.K.

1 Kwani ikawa baada ya kutamani kujua vitu ambavyo baba yangu aliona, na nikiamini kwamba Bwana anaweza kunijulisha haya kwangu, nikiwa nimekaa anikiwaza moyoni mwangu bnilinyakuliwa na Roho wa Bwana, ndiyo, hadi kwenye cmlima mrefu zaidi, ambao sijawahi kuona hapo awali kamwe, na ambao juu yake sijawahi kukanyagisha mguu wangu kamwe hapo awali.

2 Na Roho akaniambia: Tazama, ni nini unachotamani?

3 Na nilisema: Natamani kuona vitu ambavyo baba yangu aaliona.

4 Na Roho akaniambia: Unaamini kwamba baba yako aliuona amti ambao ameuzungumzia?

5 Na nikasema: Ndiyo, wewe unajua kwamba aninaamini maneno yote ya baba yangu.

6 Na baada ya mimi kuzungumza maneno haya, Roho akapaza sauti, na kusema: Hosana kwa Bwana, Mungu aliye juu sana; kwani yeye ndiye Mungu juu ya aardhi yote, ndiyo, hata juu ya yote. Na umebarikiwa ewe, Nefi, kwa sababu bunamwamini Mwana wa Mungu aliye juu sana; kwa hivyo, wewe utaona vitu ulivyotamani.

7 Na tazama utapewa kitu hiki kama aishara, kwamba baada ya kuona mti ambao ulizaa tunda ambalo baba yako alionja, wewe utaona pia mtu akiteremka kutoka mbinguni, na wewe utashuhudia; na baada ya kumwona wewe butashuhudia kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.

8 Na ikawa kwamba Roho akaniambia: Tazama! Na nikatazama na kuona amti; na ulikuwa kama ule mti ambao baba yangu aliuona; na urembo wake ulikuwa hauna kipimo, ndiyo, zaidi ya urembo wote; na bweupe wake ulizidi weupe wa theluji ivumayo.

9 Na ikawa baada ya kuona huu mti, nikamwambia Roho: Nimeona kuwa umenionyesha mti aulioadimika zaidi ya yote.

10 Na akaniambia: Nini unachotamani?

11 Na nikamwambia: Kufahamu amaana yake—kwani nilimzungumzia kama mwanadamu; kwani niliona kuwa alikuwa kwa bmfano wa mwanadamu; walakini, nilijua kwamba ni Roho wa Bwana; na akanizungumzia kama mwanadamu anavyozungumzia na mwingine.

12 Na ikawa kwamba akaniambia: Tazama! Na nikatazama ili nimwone, na sikumwona; kwani alikuwa ameenda kutoka machoni mwangu.

13 Na ikawa kwamba nilitazama na nikaona mji mkuu wa Yerusalemu, na pia miji mingine. Na nikaona mji wa aNazareti; na katika mji wa Nazareti nikamwona bbikira, na alikuwa mrembo na mweupe.

14 Na ikawa kwamba niliona ambingu zikifunguka; na malaika akateremka na kusimama mbele yangu; na akaniambia: nini unachokiona, Nefi?

15 Na nikamwambia: Ni bikira, ambaye ni mrembo na mtakatifu zaidi ya bikira wengine wote.

16 Na akaniambia: Je wajua ufadhili wa Mungu?

17 Na nikamwambia: Najua kwamba anawapenda watoto wake; walakini, sijui maana ya vitu vyote.

18 Na akaniambia: Tazama, abikira unayemwona ni bmama wa Mwana wa Mungu, katika kimwili.

19 Na ikawa kwamba niliona alinyakuliwa na Roho; na baada ya kunyakuliwa na aRoho kwa muda, malaika akanizungumizia, akisema: Tazama!

20 Na nikatazama na kumwona yule bikira tena, akimbeba amtoto mikononi mwake.

21 Na malaika akaniambia: Tazama aMwanakondoo wa Mungu, ndiyo, hata bMwana wa cBaba wa Milele! Je, unajua maana ya ule dmti ambao baba yako aliuona?

22 Na nikamjibu, nikasema: Ndiyo, ni aupendo wa Mungu, ambao umejimimina mioyoni mwa watoto wa watu, kwa hivyo, ni wa kupendeza zaidi ya vitu vyote.

23 Na akanizungumzia, na kusema: Ndiyo, na inafurahisha moyo kwa ashangwe.

24 Na baada ya kusema maneno haya, akaniambia: Tazama! Na nikatazama, na nikamwona Mwana wa Mungu aakienda miongoni mwa watoto wa watu; na nikawaona wengi wakiinama mbele ya miguu yake na kumuabudu.

25 Na ikawa kwamba niliona ile afimbo ya chuma, ambayo baba yangu aliiona, ilikuwa neno la Mungu, na ilielekea hadi kwenye chemchemi ya bmaji ya uhai, au kwenye cmti wa uzima; maji ambayo ni kielelezo cha upendo wa Mungu; na pia nikaona kwamba ule mti wa uzima ulikuwa pia kielelezo cha upendo wa Mungu.

26 Na malaika akaniambia tena: Angalia na uone aufadhili wa Mungu!

27 Na nikatazama na akuona Mkombozi wa ulimwengu, ambaye baba yangu alikuwa amenena kumhusu; na pia nikaona bnabii atakayemtayarishia njia mbele yake. Na Mwanakondoo wa Mungu akamwendea na cakabatizwa naye; na baada ya kubatizwa, nikaona mbingu zikifunguka, na Roho Mtakatifu akishuka kutoka mbinguni na kutua juu yake kwa mfano wa dnjiwa.

28 Na nikaona kwamba alienda na kuwahudumia watu, kwa auwezo na utukufu mkuu; na umati ukakusanyika kumsikiliza; na nikaona kwamba walimfukuza kutoka miongoni mwao.

29 Na pia nikaona wengine akumi na wawili wakimfuata. Na ikawa kwamba walichukuliwa na Roho kutoka machoni mwangu, na sikuwaona.

30 Na ikawa kwamba malaika akanizungumzia tena, akisema: Angalia! Na nikaangalia, na kuona mbingu zikifunguka tena, na nikaona amalaika wakiwashukia watoto wa watu; na kuwahudumia.

31 Na akanizungumzia tena, akasema: Angalia! Na nikaangalia, na nikamwona Mwanakondoo wa Mungu akienda miongoni mwa watoto wa watu. Na nikaona umati wa watu waliokuwa wagonjwa, na ambao walikuwa wakiugua kutokana na aina zote za magonjwa, pamoja na aibilisi na bpepo wachafu; na malaika akazungumza na kunionyesha hivi vitu vyote. Na cwakaponywa kwa nguvu za Mwanakondoo wa Mungu; na ibilisi pamoja na pepo wachafu wakafukuzwa.

32 Na ikawa kwamba malaika akanizungumzia tena, akisema: Angalia! Na nikaangalia na nikamwona Mwanakondoo wa Mungu, kwamba alikamatwa na watu; ndiyo, Mwana wa Mungu asiye na mwisho aalihukumiwa na ulimwengu; na niliona na kuyashuhudia.

33 Na mimi, Nefi, nikaona kwamba aliinuliwa juu ya amsalaba na bkuuawa kwa dhambi za ulimwengu.

34 Na baada ya yeye kusulubiwa nikaona umati wa dunia, ukiwa umekusanyika pamoja kupigana dhidi ya mitume wa Mwanakondoo; kwani hivi ndivyo wale kumi na wawili waliitwa na malaika wa Bwana.

35 Na umati wa dunia ulikusanyika pamoja; na nikaona kwamba walikuwa kwenye ajengo kubwa na pana, kama jengo lile baba yangu aliloliona. Na malaika wa Bwana akanizungumzia tena, akisema: Tazama ulimwengu na hekima yake; ndiyo, tazama nyumba ya Israeli imekusanyika pamoja kupinga mitume kumi na wawili wa Mwanakondoo.

36 Na ikawa kwamba niliona na ninashuhudia, kwamba lile jengo kuu na pana lilikuwa ni akiburi cha ulimwengu; na lilianguka, na muanguko wake ulikuwa mkuu zaidi. Na malaika wa Bwana akanizungumizia tena, akisema: Hivyo ndivyo mataifa yote, makabila yote, lugha zote, na watu wote, ambao wanawapinga wale mitume kumi na wawili wa Mwanakondoo wataangamizwa.