Maandiko Matakatifu
1 Nefi 10


Mlango wa 10

Lehi abashiri kwamba Wayahudi watatekwa mateka na Wababilonia—Anasimulia kuja kwa Masiya, Mwokozi, na Mkombozi, miongoni mwa Wayahudi—Lehi pia anasimulia kuhusu kuja kwa yule atakaye mbatiza Mwanakondoo wa Mungu—Lehi anasimulia kifo na ufufuko wa Masiya—Analinganisha kutawanyika na kukusanyika kwa Israeli na mzeituni—Nefi anazungumza kuhusu Mwana wa Mungu, kipawa cha Roho Mtakatifu, na haja ya haki. Karibia mwaka 600–592 K.K.

1 Na sasa mimi, Nefi, ninaendelea kuandika historia kuhusu matendo yangu kwenye amabamba haya, pamoja na utawala na huduma yangu; kwa hivyo, ili niendelee na historia yangu, lazima nizungumze machache kuhusu vitu vya baba yangu, na pia kaka zangu.

2 Kwani tazama, ikawa kwamba baada ya baba yangu kumaliza kuzungumza maneno ya andoto yake, na pia kuwasihi waendelee kwenye jitihada, aliwazungumuzia kuhusu Wayahudi—

3 Kwamba baada yao kuangamizwa, hata ule mji mkuu aYerusalemu, na wengi bkupelekwa uhamishoni cBabilonia, kulingana na nyakati za Bwana, dwatarejea tena, ndiyo, hata kurejeshwa kutoka uhamishoni; na baada ya kutolewa uhamishoni watamiliki tena nchi yao ya urithi.

4 Ndiyo, hata baada ya miaka amia sita tangu baba yangu atoke Yerusalemu, Bwana Mungu atainua bnabii miongoni mwa Wayahudi—hata cMasiya, au, kwa maneno mengine, Mwokozi wa ulimwengu.

5 Na pia akazungumzia kuhusu manabii, jinsi wengi wao walivyokuwa awameshuhudia vitu hivi, kuhusu Masiya ambaye alikuwa amemzungumzia, au huyu Mkombozi wa ulimwengu.

6 Kwa hivyo, wanadamu wote walikuwa wamepotea na wako katika hali ya akuanguka, na watakuwa hivyo hata milele wasipomtegemea huyu Mkombozi.

7 Na alizungumza pia kuhusu anabii ambaye angemtangulia Masiya, ili kumtayarishia Bwana njia yake—

8 Ndiyo, hata ataondoka mbele na kutangaza nyikani: aItayarisheni njia ya Bwana, na yanyoosheni mapito yake; kwani miongoni mwenu amesimama yeye msiyemjua; na yeye ni mkuu kunishinda, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake. Na baba yangu alizungumza mengi kuhusu kitu hiki.

9 Na baba yangu akasema atabatiza katika aBethabara, ngʼambo ya Yordani; na pia akasema kuwa batabatiza kwa maji; hata kwamba atambatiza Masiya kwa maji.

10 Na baada ya kumbatiza Masiya kwa maji, itambidi kuona na kushuhudia kwamba alimbatiza aMwanakondoo wa Mungu, ambaye ataondoa dhambi za ulimwengu.

11 Na ikawa kwamba baada ya baba yangu kuzungumza maneno haya aliwazungumzia kaka zangu kuhusu injili ambayo itahubiriwa miongoni mwa Wayahudi, na pia kuhusu akufifia kwa Wayahudi katika bkutoamini. Na baada ya ckumuua Masiya, ajaye, na baada ya kuuwawa datafufuka kutoka kwa wafu, na ajidhihirishe, kupitia nguvu za eRoho Mtakatifu, kwa Wayunani.

12 Ndiyo, baba yangu hata alizungumza mengi kuhusu Wayunani, na pia kuhusu nyumba ya Israeli, kwamba watalinganishwa na amzeituni, ambao matawi yake yatakatwa na bkutawanywa kote kote usoni mwa dunia.

13 Kwa hivyo, akasema ni lazima sote tuongozwe pamoja hadi kwenye anchi ya ahadi, ili maneno ya Bwana yatimizwe, kuwa tutawanywe kote usoni mwa dunia.

14 Na baada ya nyumba ya Israeli kutawanyika awatakusanyika tena pamoja; au, kwa usemi mwingine, baada ya bWayunani kupokea utimilifu wa Injili, matawi ya asili ya cmzeituni, au mabaki ya nyumba ya Israeli, yatapandikizwa, au kumfahamu Masiya wa ukweli, Bwana wao na Mkombozi wao.

15 Na baba yangu alitumia maneno haya kwa kuwatolea kaka zangu unabii, na kuwazungumzia na pia vitu vingi mno ambavyo siandiki kwenye kitabu hiki; kwani nimeandika mengi yaliyonipasa kwa kile kitabu changu akingine.

16 Na vitu hivi vyote, ambavyo nimezungumza, vilifanyika wakati baba yangu akiishi kwenye hema, katika bonde la Lemueli.

17 Na ikawa kwamba, baada ya mimi, Nefi nikiwa nimesikia amaneno yote ya baba yangu, kuhusu yale mambo aliyokuwa ameyaona katika bono, na pia mambo yale aliyozungumza kwa nguvu za Roho Mtakatifu, nguvu alizopokea kwa imani katika Mwana wa Mungu—na Mwana wa Mungu alikuwa ndiye cMasiya ajaye—mimi, Nefi, nikatamani pia nipate kuona, na kusikia, na kujua juu ya mambo haya, kwa nguvu za dRoho Mtakatifu, ambayo ni karama ya Mungu kwa wote wale ambao humtafuta kwa ebidii, sio tu katika nyakati fzilizopita, lakini pia katika nyakati ambapo atajionyesha mwenyewe kwa watoto wa watu.

18 Kwani yeye ni ayule yule jana, leo, na milele; na njia imetayarishiwa wanadamu wote tangu msingi wa ulimwengu, ikiwa itakuwa kwamba watatubu na kuja kwake.

19 Kwani atafutaye kwa bidii atapata; na watafunguliwa asiri za Mungu, kwa nguvu ya bRoho Mtakatifu, kama ilivyokuwa katika nyakati hizi na nyakati za kale, na vile vile hizo nyakati za kale, na pia nyakati zijazo; kwa hivyo, cmpangilio wa Bwana ni mpangilio imara milele.

20 Kwa hivyo kumbuka, Ewe mwanadamu, autahukumiwa kwa yale yote utendayo.

21 Kwa hivyo, kama uliteua kutenda maovu katika nyakati za amajaribio yako, basi utapatwa bmchafu mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu; na hakuna kitu kichafu chaweza kuishi na Mungu; kwa hivyo, lazima utupiliwe mbali milele.

22 Na Roho Mtakatifu ananipatia mamlaka kuzungumza vitu hivi, na nisiyazuie.