Dhima
Dhamira ya Wasichana


Dhamira ya Wasichana

Dhamira ya Wasichana

Mimi ni binti mpendwa wa Wazazi wa Mbinguni, mwenye asili takatifu na takdiri ya milele.

Kama mfuasi wa Yesu Kristo, ninajitahidi kuwa kama Yeye. Ninatafuta na kufanyia kazi ufunuo binafsi na kuwatumikia wengine katika jina Lake takatifu.

Nitasimama kama shahidi wa Mungu wakati wote na katika vitu vyote na katika mahali kote.

Ninapojitahidi kustahili kwa ajili ya kuinuliwa, ninathamini zawadi ya toba na kutafuta kuwa bora kila siku. Kwa imani, nitaimarisha nyumba na familia yangu, kufanya na kushika maagano matakatifu, na kupokea ibada na baraka za hekalu takatifu.