Vitabu vya Maelekezo na Miito
32. Toba na Mabaraza ya Uumini ya Kanisa


“32. Toba na Mabaraza ya Uumini ya Kanisa,” Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho (2020).

“32. Toba na Mabaraza ya Uumini ya Kanisa,” Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Picha
mwanamume na mwanamke wakisalimiana kwa mikono

32.

Toba na Mabaraza ya Uumini ya Kanisa

32.0

Utangulizi

Toba nyingi zinatokea kati ya mtu binafsi, Mungu, na wale walioathirika kwa dhambi za mtu huyo. Hata hivyo, wakati mwingine askofu au rais wa kigingi anahitaji kuwasaidia waumini wa Kanisa katika juhudi zao za kutubu.

Wakati wa kuwasaidia waumini kwenye toba, maaskofu, na marais wa vigingi ni wenye upendo na waangalifu. Wanafuata mfano wa Mwokozi, aliyewainua watu binafsi na kuwasaidia kuachana na dhambi na kumgeukia Mungu (ona Mathayo 9:10–13; Yohana 8:3–11).

Kama ilivyobainishwa hapa chini, sura hii imeratibiwa kuwaongoza viongozi kupitia maamuzi na matendo muhimu ya kumsaidia mtu kutubu dhambi nzito na kuwalinda wengine.

  • Jukumu la Kanisa katika kumsaidia Mtu Kutubu. Sehemu za 32.1–32.4 zinaelezea mafundisho ya Bwana ya toba na msamaha. Sehemu hizi pia zinaelezea malengo matatu ya vizuizi vya Uumini wa Kanisa au uondoaji. Kwa nyongeza, zinaelezea jukumu la maaskofu na marais wa vigingi katika kusaidia kwenye toba.

  • Kuamua Mpangilio kwa ajili ya Kumsaidia Mtu Atubu. Sehemu za 32.5–32.7 zinatoa miongozo kwa ajili ya kuamua ikiwa baraza la uumini au ushauri binafsi ni mpangilio wa kufaa kwa ajili ya kumsaidia mtu fulani kutubu.

  • Kusimamia Ushauri Binafsi. Sehemu ya 32.8 inatoa miongozo kwa ajili ya ushauri binafsi kutoka kwa askofu au rais wa kigingi. Pia inaelezea vizuizi vya uumini wa Kanisa visivyo rasmi.

  • Kusimamia Mabaraza ya Uumini ya Kanisa. Sehemu za 32.9–32.14 zinaelezea nani anawajibika kwa ajili ya mabaraza ya uumini, jinsi ya kuyaendesha, na maamuzi yanayowezekana. Matokeo ya maamuzi hayo pia yanaelezwa.

  • Kurejesha Haki za Uumini wa Kanisa. Sehemu za 32.15–32.17 zinaelezea jinsi mtu anavyoweza kurejeshewa haki za Uumini wa Kanisa kupitia toba.

Isipokuwa imeelekezwa vinginevyo, marejeleo kwa marais wa vigingi yanahusika pia kwa marais wa misheni. Marejeleo kwa maaskofu yanahusika pia kwa marais wa matawi.


JUKUMU LA KANISA KATIKA KUMSAIDIA MTU KUTUBU


32.1

Toba na Msamaha

Bwana alisema kwamba “hakuna kitu chochote kichafu kitakachorithi ufalme wa mbinguni” (Alma 11:37; ona pia 3 Nefi 27:19). Dhambi zetu zinatufanya wachafu—tusiostahili kuishi katika uwepo wa Baba Yetu wa Mbinguni. Pia zinatuletea uchungu katika maisha haya.

Sheria ya haki ya Mungu inahitaji matokeo wakati tunapofanya dhambi (ona Alma 42:14. 17–18). Hata hivyo, mpango Wake mkuu wa rehema “unaweza kutosheleza mahitaji ya haki, na kutuzingira [sisi] ndani ya mikono ya usalama” (Alma 34:16; ona pia Mosia 15:9).

Ili kutimiza mpango Wake wa rehema, Baba wa Mbinguni alimtuma Mwanae wa Pekee, Yesu Kristo, kulipia dhambi zetu (ona Alma 42:15). Yesu aliteseka adhabu ambayo sheria ya haki inaihitaji kwa ajili ya dhambi zetu (ona Mafundisho na Maagano 19:15–19; ona pia Alma 42:24–25). Kupitia dhabihu hii, wote Baba na Mwana walionesha Upendo Wao usiona na kikomo kwa ajili yetu (ona Yohana 3:16).

Wakati tunapotumia “imani kwa ajili ya toba,” Baba wa Mbinguni anatusamehe, akitoa huruma kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo (Alma 34:15; ona pia Alma 42:13). Wakati tunapokuwa tumesafishwa na kusamehewa, tunaweza hatimaye kuurithi ufalme wa Mungu (ona Isaya 1:18; Mafundisho na Maagano 58:42).

Toba ni zaidi ya kubadili tabia. Ni kukataa dhambi na kumgeukia Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Inaelekeza kwenye badiliko la moyo na akili (ona Mosia 5:2; Alma 5:12–14; Helamani 15:7). Kupitia toba, tunakuwa watu wapya, tuliopatanishwa na Mungu (ona 2 Wakorintho 5:17–18; Mosia 27:25–26).

Fursa ya kutubu ni mojawapo ya baraka kuu ambazo Baba wa Mbinguni ametupatia kupitia zawadi ya Mwanae.

32.2

Malengo ya Vizuizi vya Uumini wa Kanisa au Uondoaji

Wakati mtu anapokuwa amebatizwa, yeye anakuwa sehemu ya “nyumba ya Mungu” (Waefeso 2:19). Maagano ya ubatizo yanajumuisha ahadi ya kujitahidi kuishi kulingana na mafundisho na amri za Kristo. Wakati mtu anaposhindwa, mtu huyo anatumia imani katika Yesu Kristo na anatubu, akitegemea juu ya rehema Zake za kuimarisha na kusamehe.

Kama muumini akitenda dhambi nzito, askofu au rais wa kigingi anamsaidia atubu. Kama sehemu ya mchakato huu, anaweza kuhitaji kuzuia baadhi ya haki za Uumini wa Kanisa kwa muda. Katika baadhi ya hali, anaweza kuhitaji kuondoa uumini wa mtu kwa muda.

Kuzuia au kuondoa uumini wa mtu hakukusudii kuadhibu. Bali, vitendo hivi wakati mwingine ni lazima ili kumsaidia mtu atubu na kupata uzoefu wa badiliko la moyo. Pia vinatoa muda kwa mtu kujiandaa kiroho kufanya upya na kutunza maagano yake.

Askofu au rais wa kigingi anasimamia vizuizi vya uumini au uondoaji kama ilivyoainishwa katika 32.5–32.14. Vitendo hivi vinaambatana na masharti ya toba. Wakati mtu anapotubu kwa dhati, anaweza kurejeshewa haki za uumini wa Kanisa.

Wakati vizuizi vya uumini au uondoaji ni lazima, askofu au rais wa kigingi anafuata mwongozo wa Roho Mtakatifu na maelekezo katika sura hii. Anatenda katika roho ya upendo (ona 32.3).

Vizuizi vya uumini wa Kanisa ni vya kidini, sio vya kiraia au kihalifu. Vinaathiri tu msimamo wa mtu katika Kanisa. (Ona Mafundisho na Maagano 134:10.)

Malengo matatu ya vizuizi vya uumini au uondoaji ni kama ifuatavyo.

32.2.1

Husaidia Kuwalinda Wengine

Lengo la kwanza ni kusaidia kuwalinda wengine. Wakati mwingine mtu anakuwa tishio la kimwili au kiroho. Tabia za unyanyasaji, kudhuru kimwili, unyanyasaji wa kijinsia, unyanyasaji kwa kutumia vitu, udanganyifu, na ukengeufu ni baadhi ya njia ambazo kwazo hii inaweza kutokea. Kwa msukumo, askofu au rais wa kigingi anatenda ili kuwalinda wengine wakati mtu fulani anapokuwa tishio katika njia hizi na njia zingine hatari (ona Alma 5:59–60).

32.2.2

Humsaidia Mtu Kufikia Nguvu ya Ukombozi ya Yesu Kristo kupitia Toba

Lengo la pili ni kumsaidia mtu kufikia nguvu ya ukombozi ya Yesu Kristo kupitia toba. Kupitia mchakato huu, mtu anaweza tena kuwa safi na mwenye kustahili kupokea baraka zote za Mungu.

32.2.3

Hulinda Uadilifu wa Kanisa

Lengo la tatu ni kulinda uadilifu wa Kanisa. Kuzuia au kuondoa uumini wa mtu wa Kanisa inaweza kuwa lazima kama tabia yake kwa kipekee inaleta madhara kwa Kanisa (ona Alma 39:11). Uadilifu wa Kanisa haulindwi kwa kuficha au kupunguza uzito wa dhambi—bali kwa kuzishughulikia.

32.3

Jukumu la Waamuzi katika Israeli

Picha
askofu akizungumza na mtu

Maaskofu na Marais wa vigingi wanaitwa na kusimikwa kuwa waamuzi katika Israeli (ona Mafundisho na Maagano 107:72–74). Wanashikilia funguo za ukuhani kumwakilisha Bwana katika kuwasaidia waumini wa Kanisa watubu (ona Mafundisho na Maagano 13:1; 107:16–18).

Mara kwa mara maaskofu na marais wa vigingi wanasaidia kwenye toba kupitia ushauri binafsi. Msaada huu unaweza kujumuisha kuzuia kusiko rasmi baadhi ya haki za uumini wa Kanisa kwa muda. (Ona 32.8.)

Kwa baadhi ya dhambi nzito, viongozi wanasaidia kwenye toba kwa kufanya baraza la uumini (ona 32.6 na 32.9–32.14). Msaada huu unaweza kujumuisha uzuiaji rasmi wa baadhi ya haki za uumini wa Kanisa au uondoaji wa uumini wa mtu kwa muda (ona 32.11.3 na 32.11.4).

Maaskofu na marais wa vigingi huwasaidia waumuni wa Kanisa kuelewa kwamba Mungu anawapenda watoto Wake. Kwa sababu Anataka wawe na furaha na wapokee baraka, anajali pia kwa kiasi kikubwa kuhusu utii na toba yao.

Maaskofu na marais wa vigingi wana upendo na wanajali pale wanapowasaidia waumini watubu. Kuingilia kwa Mwokozi kwa mwanamke aliyeshikwa kwenye uzinzi ni mwongozo (ona Yohana 8:3–11). Ingawa Hakusema kuwa dhambi zake zimesamehewa, Yeye hakumhukumu mwanamke. Badala yake, Alimwambia “usifanya dhambi tena”—kutubu na kubadili maisha yake.

Viongozi hawa wanafundisha kwamba kuna “furaha … mbinguni kwa mwenye dhambi mmoja ambaye anatubu” (Luka 15:7). Wana subira, wanatoa msaada, na wako chanya. Wanastawisha tumaini. Wanafundisha na kushuhudia kwamba kwa sababu ya dhabihu ya upatanisho ya Mwokozi, wote wanaweza kutubu na kuwa safi.

Maaskofu na marais wa vigingi wanatafuta mwongozo kutoka kwa Roho kujua jinsi ya kumsaidia kila mtu atubu. Ni kwenye dhambi nzito pekee ndipo Kanisa limeweka kiwango cha hatua zipi viongozi wake wanapaswa kuchukua (ona 32.6 na 32.11). Hakuna hali mbili zinazoweza kuwa sawa. Ushauri ambao viongozi wanatoa na mchakato wa toba wanaouhimiza lazima uwe wenye mwongozo wa kiungu na unaweza kuwa tofauti kwa kila mtu.

Bwana anajua hali za kila mtu, uwezo, na ukomavu wa kiroho. Roho Mtakatifu atawasaidia viongozi kutambua jinsi ya kuwasaidia waumini kufanya mabadiliko ya lazima ili waweze kupona na kupinga jaribu la kurudia dhambi.

Kumsaidia mtu atubu, amrudie Mungu, na aweze kuponywa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo ni moja ya uzoefu wa furaha mno mtu anaoweza kuwa nao. Mafundisho na Maagano 18:10–13 inaeleza:

“Kumbuka thamani ya nafsi ni kubwa mbele za Mungu;

“Kwani, tazama, Bwana Mkombozi wako aliteseka hadi kifo katika mwili; kwa hiyo aliteseka maumivu ya watu wote, ili kwamba watu wote waweze kutubu na kuja kwake.

“Na yeye amefufuka tena kutoka kwa wafu, ili kwamba aweze kuwaleta watu wote kwake, kwa masharti ya toba.

“Na ni shangwe kubwa kiasi gani kwake katika nafsi ambayo hutubu!”

32.4

Kuungama, Usiri, na Kutoa Taarifa kwa mamlaka za Kiserikali

32.4.1

Kuungama

Toba inahitaji kwamba dhambi ziungamwe kwa Baba wa Mbinguni. Yesu Kristo alisema, “Kwa hili mnaweza kujua kama mtu ametubu dhambi zake—tazama, ataziungama na kuziacha” (Mafundisho na Maagano 58:43; ona pia Mosia 26:29).

Wakati waumini wa Kanisa wanafanya dhambi nzito, toba yao inajumuisha pia kuungama kwa askofu wao au rais wa kigingi. Kisha yeye anaweza kutumia funguo za injili ya toba kwa niaba yao (ona Mafundisho na Maagano 13:1; 84:26–27; 107:18, 20). Hii inawasaidia kupona na kurudi kwenye njia ya injili kupitia nguvu ya Upatanisho ya Mwokozi.

Lengo la kuungama ni kuwatia moyo waumini kujivua mzigo wenyewe ili waweze kikamilifu kutafuta msaada wa Bwana katika kubadilika na kupona. Kukuza “moyo uliovunjika na roho iliyopondeka” kunasaidiwa na kuungama (2 Nefi 2:7). Kuungama kwa hiari kunaonesha kwamba mtu anatamani kutubu.

Wakati muumini anapoungama, askofu au rais wa kigingi anafuata mwongozo kwa ajili ya kushauri katika 32.8. Kwa sala anatafuta mwongozo kuhusu mpangilio unaofaa kwa ajili ya kumsaidia muumini atubu (ona 32.5). Anafikiria kama baraza la uumini litasaidia. Kama sera ya Kanisa inahitaji baraza la uumini, anaelezea hili (ona 32.6 na 32.10).

Wakati mwingine muumini amemkosea mwenza wake au mtu mzima mwingine. Kama sehemu ya toba, anapaswa kwa kawaida kuungama kwa mtu yule na kutafuta msamaha. Kijana anayefanya dhambi nzito kwa kawaida anahimizwa kushauriana na wazazi wake.

32.4.2

Dhambi Nzito Ambazo Haziungamwi au Hazisemwi

Askofu au rais wa kigingi kwa kawaida hupata habari kuhusu dhambi nzito kupitia kuungama au kutoka kwa mtu mwingine. Anaweza pia kupata ushawishi kuhusu uwezekano wa dhambi nzito kupitia Roho Mtakatifu. Kama anahisi kushawishiwa na Roho kwamba mtu fulani anaweza kuwa anapambana na dhambi, anaweza kupanga mahojiano. Wakati wa mahojiano, anashiriki wasiwasi wake katika njia ya upole na heshima. Anaepuka toni yoyote ya kutuhumu.

Kama muumini anakana kufanya dhambi nzito ambayo askofu au rais wa kigingi ana taarifa ya kuithibitisha, baraza la uumini bado linaweza kukaa. Hata hivyo, ushawishi wa kiroho pekee hautoshi kufanya baraza (ona Mafundisho na Maagano 10:37). Kiongozi anaweza kukusanya taarifa za ziada kama zitahitajika. Anafuata miongozo katika 32.4.3 na 32.10.2.

32.4.3

Kukusanya taarifa

Kabla ya kufanya baraza la uumini, askofu au rais wa kigingi anakusanya taarifa nyingi iwezekanavyo kadiri ya anavyozihitaji. Taarifa kutoka kuungama kwa muumini mara nyingi zinatosha. Taarifa zinaweza pia kuja kutoka kwa mwanafamilia, kiongozi mwingine wa Kanisa, mhanga, au mshiriki katika dhambi.

Wakati wa kukusanya taarifa, askofu au rais wa kigingi anapaswa kutumia tu taratibu ambazo zinafaa kwa kiongozi wa ukuhani. Hapaswi kuweka lindo kwenye nyumba ya mtu au kumrekodi bila idhini yake. Wala hapaswi kutumia mifumo yoyote ambayo ni kinyume na sheria.

Tuhuma za uongo ni adimu lakini zinaweza kutokea. Viongozi wa Kanisa wanapaswa kuwa waangalifu wakati ambapo kuna taarifa chache kando na neno moja la mtu. Kwa mfano, muumini ambaye anatuhumiwa kwa uasherati anaweza kukana kosa. Maandiko yanaelezea kwamba “kila neno litathibitika dhidi yake kwa mashahidi wawili wa Kanisa” (Mafundisho na Maagano 42:80). “Mashahidi wawili” inamaanisha vyanzo viwili tofauti vya taarifa. Hii inaweza kujumuisha ufahamu wa mshiriki na baadhi ya vyanzo vingine vya kuaminika. Wakati mwingine kiongozi wa ukuhani anaweza kutaka kungoja kuchukua hatua mpaka taarifa zaidi zinapopatikana.

Wakati kiongozi wa Kanisa anapokusanya taarifa kwa ajili ya baraza la uumini, anapaswa mara moja kuacha ikiwa ana habari kwamba utekelezaji wa sheria unashughulikia kumpeleleza muumini. Hii inafanywa kuepuka uwezekano wa madai kwamba kiongozi anaweza kuwa amezuia haki. Kwa ushauri wa kisheria kuhusu hali hizi ndani ya Marekani na Kanada, rais wa kigingi anawasiliana na ofisi ya Kanisa ya Ushauri Mkuu:

1-800-453-3860, mkondo 2‑6301

1-801-240-6301

Nje ya Marekani na Kanada, rais wa kigingi anawasiliana na mshauri wa sheria wa eneo kwenye ofisi ya eneo.

Kwa kawaida baraza la uumini halikai kufikiria tabia inayochunguzwa na mahakama ya mashitaka ya madai au jinai mpaka mahakama inapokuwa imefikia hukumu ya mwisho. Katika baadhi ya hali inaweza kufaa pia kuchelewesha baraza la uumini mpaka kipindi cha sheria cha kukata rufaa kinapokuwa kimekwisha au rufaa imekataliwa.

32.4.4

Usiri

Maaskofu, marais wa vigingi, na washauri wao wana jukumu takatifu la kulinda taarifa zote za siri walizopewa. Taarifa hii inaweza kuja katika mahojiano, ushauri, na kuungama. Jukumu lilelile la usiri linatumika kwa wote wanaoshiriki katika mabaraza ya uumini. Usiri ni muhimu kwa sababu waumini wanaweza wasiungame dhambi au kutafuta mwongozo kama kile wanachoshiriki hakitawekwa siri. Utoaji wa siri unasaliti uaminifu wa waumini na unawasababishia kupoteza imani kwa viongozi wao.

Uthabiti kwenye jukumu lao la usiri, askofu, rais wa kigingi, au washauri wao wanaweza tu kushiriki taarifa kama hizo kama ifuatavyo:

  • Wanahitaji kushauriana na rais wa kigingi wa muumini, rais wa misheni, au askofu kuhusu kuitisha baraza la uumini au masuala yanayohusiana. Rais wa kigingi anaweza pia kushauriana na Sabini wa eneo lake. Kama itahitajika, Sabini wa Eneo anamuelekeza rais wa kigingi kwa Urais wa Eneo. Rais wa kigingi ndiye pekee anayeamua ikiwa baraza linapaswa kuitishwa au matokeo yake.

  • Mtu anahamia kata mpya (au kiongozi wa ukuhani anapumzishwa) wakati hatua za uumini au masuala mengine mazito yanangojea maamuzi. Katika hali hizi, kiongozi anamfahamisha askofu mpya au rais wa kigingi kuhusu mambo ya kushughulikia au hatua zinazongojea maamuzi (ona 32.14.7). Pia anamtaarifu kiongozi ikiwa muumini anaweza kuleta tishio kwa wengine.

  • Askofu au rais wa kigingi anapata taarifa kwamba muumini wa Kanisa anaishi nje ya kata au kigingi anaweza kuwa amehusika katika dhambi nzito. Katika hali kama hiyo, kwa siri anawasiliana na askofu wa muumini yule.

  • Ni lazima kufichua taarifa wakati wa baraza la uumini. Taarifa zote zilizokusanywa na zilizotolewa kama sehemu ya baraza la uumini ni siri.

  • Muumini anachagua kutoa ruhusa kwa ajili ya kiongozi kushiriki taarifa na watu maalumu. Hawa wanaweza kujumuisha wazazi, viongozi wa Kanisa, au wengine wanaoweza kutoa msaada. Kiongozi hashiriki taarifa zaidi ya ruhusa muumuni aliyoitoa.

  • Inaweza kuwa muhimu kushiriki taarifa chache kuhusu uamuzi wa baraza la uumini (ona 32.12.2).

Katika hali zote zingine, kiongozi anapaswa kurejelea kwenye 32.4.5. Hali hizi zinajumuisha wakati sheria inapoweza kuhitaji kwamba jinai, kama unyanyasaji wa mtoto, liripotiwe kwenye mamlaka ya serikali.

Kuwasaidia viongozi katika kuwalinda wengine na kutii sheria, Kanisa linatoa msaada kutoka kwa wataalamu waliopata mafunzo. Ili kupokea mwongozo huu, viongozi mara moja wanapiga simu kwenye msaada wa Kanisa dhidi ya unyanyasaji kule unakopatikana (ona 32.4.5 na 38.6.2.1) Mahali ambapo haupo, rais wa kigingi anawasiliana na mshauri wa sheria wa eneo kwenye ofisi ya eneo.

Katika hali moja pekee askofu au rais wa kigingi anapaswa kufichua taarifa ya siri bila kwanza kuomba mwongozo kama huo. Hapo ni pale ambapo ufichuzi ni lazima ili kuzuia madhara yanayotishia uhai au uharibifu mkubwa na hakuna muda wa kuomba mwongozo. Katika hali kama hizo, jukumu la kuwalinda wengine ni muhimu zaidi kuliko jukumu la usiri. Viongozi wanapaswa kuwasiliana na mamlaka za kiraia mara moja.

Kama viongozi wanatunza muhtasari au wanawasiliana wao kwa wao kielekroniki, wanalinda kuingiliwa kwa taarifa hii. Pia wanafuta au kuharibu taarifa wakati wanapokuwa hawaihitaji tena. Hawashiriki bila ulazima taarifa binafsi.

Mamlaka za kiraia zinaweza kupinga usiri unaotakiwa wa kiongozi wa ukuhani. Kama hii inatokea ndani ya Marekani na Kanada, rais wa kigingi anaomba ushauri wa kisheria kutoka ofisi ya Kanisa ya Ushauri Mkuu:

1-800-453-3860, mkondo 2‑6301

1-801-240-6301

Nje ya Marekani na Kanada, rais wa kigingi anawasiliana na mshauri wa sheria wa eneo kwenye ofisi ya eneo.

32.4.5

Kutoa Taarifa kwa Mamlaka za Serikali

Toba ya baadhi ya dhambi zinahitaji mtu kutoa taarifa kwa mamlaka za serikali kama amevunja sheria ya kiraia. Maaskofu na marais wa vigingi wanawahimiza waumini kufuata sheria na kutoa taarifa kwa mambo kama hayo. Pia wanawashauri waumini kupata ushauri stadi wa kisheria wakati wa kutoa taarifa. Sera za Kanisa ni kutii sheria.

Katika sehemu nyingi, viongozi wa ukuhani wanatakiwa kisheria kutoa taarifa ya baadhi ya tabia za kihalifu ambazo wanazifahamu. Kwa mfano, baadhi ya majimbo na nchi zinahitaji kwamba unyanyasaji wa mtoto utolewe taarifa kwenye mamlaka za utekelezji wa sheria.

Katika baadhi ya nchi, Kanisa limeanzisha msaada wa kisheria wa siri wa unyanyasaji ili kuwasaidia maaskofu na marais wa vigingi. Viongozi hawa wanapaswa mara moja kuita msaada wa kisheria kuhusu kila hali ambayo mtu anaweza kuwa amenyanyaswa (ona 38.6.2.1). Unapatikana saa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki.

Katika nchi ambazo hazina msaada wa kisheria, askofu anayepata habari ya unyanyasaji anapaswa kuwasiliana na rais wake wa kigingi, ambaye anapaswa kuomba mwongozo kutoka kwa mshauri wa kisheria wa eneo kwenye ofisi ya eneo.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kutoa taarifa ya unyanyasaji, ona 38.6.2.1 na 38.6.2,7.


KUAMUA MAZINGIRA KWA AJILI YA KUMSAIDIA MTU ATUBU


32.5

Mazingira kwa ajili ya Kumsaidia Mtu Atubu

Baada ya kujua kwamba muumini ametenda dhambi nzito, askofu au rais wa kigingi anachukua hatua kuwalinda wengine. Pia anaomba mwongozo wa Roho Mtakatifu katika kuamua mpangilio kwa ajili ya kumsaidia mtu yule kutubu na kumkaribia zaidi Mwokozi.

32.5.1

Muhtasari wa Mazingira

Jedwali linalofuata linaorodhesha mipangilio mitatu kwa ajili ya kumsaidia mtu atubu. Pia linatoa muhtasari baadhi ya mambo ya kuzingatia kwa viongozi wakati wa kuamua mpangilio gani wa kuutumia.

Mazingira kwa ajili ya Kumsaidia Mtu Atubu

Mazingira

Baadhi ya Mambo ya Kuzingatia (ona pia 32.7)

Mazingira

Baraza la Uumini la Kigingi

Baadhi ya Mambo ya Kuzingatia (ona pia 32.7)

  • Kwa waumini waliopokea endaumenti ya hekaluni.

  • Linatakiwa kama mwanamume au mwanamke aliyepata endaumenti ataondolewa uumini wake kwa ajili ya dhambi yoyote nzito au vitendo vilivyowasilishwa katika 32.6.1, 32.6.2, au 36.6.3.

Mazingira

Baraza la Uumini la Kata

Baadhi ya Mambo ya Kuzingatia (ona pia 32.7)

  • Kwa ajili ya muumini yoyote.

  • Linatakiwa kwa dhambi nzito iliyozungumziwa katika 32.6.1.

  • Linaweza kuwa la lazima kwa dhambi nzito na vitendo vilivyozungumziwa katika 32.6.2 na 32.6.3.

  • Halitoshi kama mwanamume au mwanamke aliyepata endaumenti ataondolewa uumini wake wa Kanisa kwa sababu ya dhambi yoyote nzito au vitendo vilivyozungumziwa katika 32.6.1, 32.6.2, au 36.6.3.

Mazingira

Ushauri Binafsi (ona 32.8)

Baadhi ya Mambo ya Kuzingatia (ona pia 32.7)

  • Kwa ajili ya muumini yoyote.

  • Unaweza kujumuisha vizuizi vya uumini wa Kanisa visivyo rasmi.

  • Unaweza usitoshe kwa dhambi nzito au vitendo ambavyo baraza la uumini litasaidia katika mchakato wa toba (ona 32.6.2 na 32.6.3).

  • Hautoshi kwa dhambi nzito zinazohitaji baraza la uumini (ona 32.6.1).

  • Halitoshi kama mwanamume au mwanamke aliyepata endaumenti ataondolewa uumini wake wa Kanisa kwa sababu ya dhambi yoyote nzito au vitendo vilivyozungumziwa katika 32.6.1, 32.6.2, au 36.6.3.

Ushauri binafsi na vizuizi visivyo rasmi kutoka kwa askofu au rais wa kigingi wakati mwingine havitoshi kumsaidia mtu kutubu dhambi nzito. Bwana ametoa mabaraza ya uumini kumsaidia mwamuzi katika Israeli katika hali hizi. (Ona Kutoka 18:12–27; Mosia 26:29–36; Mafundisho na Maagano 42:80–83; 102.) Kwa baadhi ya dhambi nzito, baraza linahitajika kwa sera ya Kanisa (ona 32.6.1). Kukiuka maagano ya hekaluni kunaongeza uwezekano wa baraza la uumini kuwa la lazima (ona 32.7.4).

Katika kata, washauri wa askofu wanasaidia katika mabaraza ya uumini. Katika kigingi, washauri wa rais wa kigingi wanasaidia. Katika baadhi ya mabaraza ya uumini kwenye kigingi, baraza kuu pia linashiriki (ona 32.9.2). Katika baraza la uumini, uaskofu au urais wa kigingi hukutana na mtu kwa moyo wa upendo.

32.5.2

Kuamua Mazingira na Muda

Wakati wa kuamua yapi kati ya mazingira haya yatamsaidia vizuri mtu kutubu, viongozi wanaomba mwongozo wa Roho Mtakatifu. Pia wanafikiria vipengele vifuatavyo:

  • Uzito wa dhambi na sera ya Kanisa kuhusu kama baraza linahitajika (ona 32.6)

  • Hali ya mtu (ona 32.7)

Askofu anashauriana na rais wa kigingi kuhusu hali maalumu. Lazima apate kibali kutoka rais wa kigingi kabla ya kufanya baraza la uumini.

Kuhusu mambo magumu, rais wa kigingi anaweza kuomba ushauri kutoka kwa Sabini wa Eneo lake. Rais wa kigingi lazima ashauriane na Urais wa Eneo juu ya mambo yaliyoainishwa katika 32.6.3. Hata hivyo, Rais wa kigingi pekee ndiye anaamua kama baraza linapaswa kuitwa ili kushughulikia tabia. Kama baraza linakutana, rais wa kigingi au askofu anaamua matokeo.

Kama askofu au rais wa kigingi anaamua kwamba ushauri binafsi unatosha, anafuata mwongozo katika 32.8. Kama anaamua kwamba baraza la uumini linahitajika, au kama sera ya Kanisa inahitaji baraza, yule anayeliongoza anafuata taratibu katika 32.9–32.14.

Kabla ya kufanya baraza, askofu au rais wa kigingi anaweza kuamua kwamba vizuizi vile visivyo rasmi vya uumini vitakuwa vyenye kufaa kwa muda. Anafanya baraza wakati itakapokuwa vyema kutia moyo toba ya kweli ya muumini. Hata hivyo, anapaswa kutochelewesha baraza kama ni lazima ili kuwalinda wengine.

32.6

Uzito wa Dhambi na Sera za Kanisa

Uzito wa dhambi ni zingatio muhimu katika kuamua mazingira ambayo (1) yatasaidia kuwalinda wengine na (2) kumsaidia mtu atubu. Bwana alisema kwamba “hawezi kuiangalia dhambi na kuivumilia hata kidogo” (Mafundisho na Maagano 1:31; ona pia Mosia 26:29). Watumishi Wake hawapaswi kupuuzia ushahidi wa dhambi nzito.

Dhambi nzito ni makosa ya makusudi dhidi ya sheria za Mungu. Aina za dhambi nzito zimeorodheshwa hapa chini.

Sehemu zifuatazo zinaelezea lini baraza la uumini linatakiwa, lini linaweza kuwa la lazima, na lini sio la lazima

32.6.1

Lini Baraza la Uumini Linatakiwa

Askofu au rais wa kigingi lazima aitishe baraza la uumini wakati taarifa zinapoonesha kwamba muumini anaweza kuwa amefanya dhambi yoyote kati ya zile zilizoelezwa katika sehemu hii. Kwa dhambi hizi, baraza linahitajika bila kujali kipimo cha kupevuka kiroho cha muumini na uelewa wa injili.

Ona 32.11 kwa ajili ya uwezekano wa matokeo ya mabaraza ambayo yameitishwa kwa ajili ya dhambi zilizoorodheshwa katika sehemu hii. Vizuizi visivyo rasmi vya uumini sio vya hiari kwa mabaraza haya.

32.6.1.1

Vitendo vya kutumia nguvu na unyanyasaji

Mauaji. Baraza la uumini linahitajika kama muumini anamuua mtu. Kama ilivyotumika hapa, mauaji ni kuutoa uhai wa binadamu kwa makusudi, bila haki. Kuondolewa uumini wa Kanisa wa mtu kunahitajika.

Mauaji hayajumuishi vitendo vya polisi au kijeshi wakiwa kazini. Utoaji mimba hauchukuliwi kama mauaji katika muktadha huu. Kama kifo kilisababishwa na ajali au kujilinda mwenyewe au kuwalinda wengine, utoaji wa uhai wa binadamu unaweza usifafanuliwe kama mauaji. Hii inaweza pia kuwa kweli katika hali zingine, kama vile wakati mtu ana uwezo mdogo wa kiakili.

Ubakaji. Baraza la uumini linahitajika kwa ajili ya ubakaji. Kama lilivyotumika hapa, ubakaji ni kujamiiana kwa kutumia nguvu au kujamiiana na mtu fulani ambaye hawezi kukubali kisheria kutokana na uwezo mdogo kiakili au kimwili. Kama ilivyotumika hapa, ubakaji haujumuishi kujamiiana kwa kukubaliana kati ya watoto wawili ambao wanakaribiana kiumri.

Kutiwa Hatiani kwa Unyanyasaji wa Kijinsia. Baraza la uumini linahitajika kama muumini ametiwa hatiani kwa unyanyasaji wa kijinsia.

Unyanyasaji wa Watoto au Vijana. Baraza la uumini linahitajika kama muumini ananyanyasa mtoto au kijana kama ilivyoelezwa katika 38.6.2.3.

Unyanyasaji wa Mume au Mke au Mtu Mzima Mwingine. Kuna wigo tofauti wa uzito katika tabia ya unyanyasaji. Ona 38.6.2.4 kwa wakati gani baraza la uumini linahitajika kwa ajili ya unyanyasaji wa mume au mke au mtu mzima mwingine.

Tabia ya Unyanyasaji wa Nguvu. Baraza la uumini linahitajika kama mtu mzima mara kwa mara anawadhuru watu kimwili kupitia tabia ya nguvu na ni tishio kwa wengine.

32.6.1.2

Uasherati

Kujamiiana kwa maharimu (kujamiiana kwa ndugu wa karibu). Baraza la uumini linahitajika kwa ajili ya kujamiiana kwa maharimu kama iliyofafanuliwa katika 38.6.10. Kuondolewa uumini wa Kanisa wa mtu takribani mara zote kunahitajika.

Ponografia ya Watoto. Baraza la uumini linahitajika kama mtu anahusika katika ponografia ya watoto kama ilivyoainishwa katika 38.6.6.

Ndoa ya mitala. Baraza la uumini linahitajika kama mtu kwa kujua anafunga ndoa ya mitala. Baadhi ya ndoa za mitala zinaweza kutokea kwa siri, kwa mume na mke kutojua kuhusu mmoja au zaidi ya waume na wake wengine. Kuondoa uumini wa Kanisa wa mtu kunahitajika ikiwa mtu kwa kujua anaingia kwenye ndoa ya mitala.

Tabia ya Unyanyasaji wa Nguvu Kijinsia. Baraza la uumini linahitajika kama mtu mzima mara kwa mara anawadhuru watu kijinsia na ni tishio kwa wengine.

32.6.1.3

Vitendo vya Ulaghai

Tabia ya Unyanyasaji wa Nguvu Kifedha. Baraza la uumini linahitajika kama mtu mzima ana historia ya kwa makusudi na mara kwa mara kuwadhuru watu kifedha na ni tishio kwa wengine (ona 38.6.2.4). Hii inajumuisha ulaghai wa uwekezaji na shughili zinazofanana na hizo. Upotevu wa kifedha usiokusudiwa kutokana na hali za kiuchumi haufikiriwi kama ni ulaghai. Kama madai mahakamani yanahusika, viongozi wa ukuhani wanaweza kuamua kusubiri mpaka matokeo ya mwisho.

32.6.1.4

Ukiukwaji wa Uaminifu

Dhambi Nzito Wakati Unashikilia Nafasi Maarufu ya Kanisa. Baraza la uumini linahitajika kama muumini anafanya dhambi nzito akiwa anashikilia nafasi maarufu. Hawa hujumuisha, Kiongozi Mkuu mwenye Mamlaka, Afisa Mkuu wa Kanisa, Sabini wa Eneo, rais wa hekalu au matroni, rais wa misheni, au mwenza wake, rais wa kigingi, patriaki, au askofu. Hii haiwahusu marais wa matawi. Hata hivyo, haki za uumini wa Kanisa wa rais wa tawi zinaweza kuzuiliwa au kuondolewa sawa na ilivyo kwa waumini wengine.

32.6.1.5

Baadhi ya Vitendo Vingine

Kupatikana na hatia ya Jinai. Baraza la uumini linahitajika katika hali nyingi wakati mtu anatiwa hatiani kwa jinai.

32.6.2

Wakati Baraza la Uumini linapoweza kuwa la Lazima

Baraza la Uumini linapoweza kuwa la lazima katika mifano ifuatayo.

32.6.2.1

Vitendo vya kutumia nguvu na unyanyasaji

Bwana aliamuru, Usiue … , wala kufanya kitu chochote kama hicho” (Mafundisho na Maagano 59:6; italiki zimeongezwa). Vitendo vya kutumia nguvu na unyanyasaji ambavyo kwavyo baraza la uumini linaweza kuwa la lazima vinajumuisha (lakini havikomi kwa) hivyo vilivyoorodheshwa hapo chini.

Jaribio la Kuua. Kwa makusudi kujaribu kuua mtu.

Unyanyasaji wa Kijinsia, ikijumuisha Mashambulizi na Usumbufu. Unyanyasaji wa Kijinsia unajumuisha matendo ya aina mbalimbali (ona 38.6). Baraza la uumini linaweza kuwa la lazima kwa ajili ya mtu ambaye amemshambulia kijinsia au amemnyanyasa mtu. Ona 38.6.18.3 kwa ajili ya wakati baraza linapohitajika.

Unyanyasaji wa Mume au Mke au Mtu Mzima Mwingine. Kuna wigo tofauti wa uzito katika tabia ya unyanyasaji (ona 38.6.2.4). Baraza la uumini linaweza kuwa la lazima kwa ajili ya mtu ambaye amemnyanyasa mume au mke au mtu mzima mwingine. Ona 38.6.2.4 kwa ajili ya wakati baraza linapohitajika.

32.6.2.2

Uasherati na Uzinzi

Sheria ya Bwana ya usafi wa kimwili ni kujinyima mahusiano ya kingono nje ya ndoa kati ya mwanamume na mwanamke kulingana na sheria ya Mungu (ona Kutoka 20:14; Mafundisho na Maagano 63:16.). Baraza la uumini linaweza kuwa la lazima kwa ajili ya uesharati na uzinzi kama ilivyoelezwa katika 38.6.5. Ona 32.6.1.2 kwa ajili ya wakati baraza linapohitajika.

32.6.2.3

Vitendo vya Ulaghai

Amri Kumi zinafundisha, “Usiibe” au “kutoa ushahidi wa uongo” (Kutoka 20:15–16). Baraza la uumini linaweza kuwa la lazima kwa ajili ya vitendo kama vile unyang’anyi, wizi wa kuvunja nyumba, wizi, ubadhirifu, kosa la kusema uongo, na ulaghai. Ona 38.8.2 kwa ajili ya ulaghai wa kindugu. Ona 32.6.1.3 kwa ajili ya wakati baraza linapohitajika kwa ajili ya vitendo vya ulaghai.

32.6.2.4

Ukiukwaji wa Uaminifu

Baraza la Uumini linaweza kuwa la lazima ikiwa muumini:

  • Ametenda dhambi nzito wakati anashikilia nafasi ya mamlaka au kuaminika katika Kanisa au jamii.

  • Ametenda dhambi nzito ambayo inajulikana sana.

Ona 32.6.1.4 kwa ajili ya wakati baraza linapohitajika.

32.6.2.5

Baadhi ya vitendo vingine

Mfalme Benjamini alifundisha, “Siwezi kuwaelezea vitu vyote ambavyo vinaweza kuwasababisha kutenda dhambi; kwani kuna njia nyingi na mbinu, nyingi sana hata kwamba siwezi kuzihesabu” (Mosia 4:29). Baraza linaweza kuwa la lazima ikiwa mtu:

  • Anaonesha mwelekeo wa kufanya dhambi nzito (ona Mafundisho na Maagano 82:7).

  • Kwa makusudi anatelekeza wajibu wa familia, pamoja na kutolipa msaada wa mtoto na masurufu.

  • Kuuza mihadarati (dawa za kulevya).

  • Anafanya vitendo vingine vizito vya jinai.

Baraza la uumini linaweza kuwa la lazima ikiwa muumini anakubaliana na, anafanya, anapanga kwa ajili ya, analipia kwa ajili ya, au anahimiza utoaji mimba. Ona 38.6.1 kwa ajili ya mwongozo.

Wakati Baraza la Uumini Linapotakiwa au Linapoweza Kuwa la Lazima

Aina ya Dhambi

Baraza la Uumini Linatakiwa (ona 32.6.1)

Baraza la Uumini Linaweza Kuwa la Lazima (ona 32.6.2)

Aina ya Dhambi

Vitendo vya kutumia nguvu na unyanyasaji

Baraza la Uumini Linatakiwa (ona 32.6.1)

  • Mauaji

  • Ubakaji

  • Kutiwa hatiani kwa unyanyasaji wa kijinsia

  • Unyanyasaji wa watoto au vijana

  • Tabia ya unyanyasaji wa kutumia nguvu.

Baraza la Uumini Linaweza Kuwa la Lazima (ona 32.6.2)

  • Jaribio la kuua.

  • Unyanyasaji wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na shambulio na usumbufu (ona 38.6.18.3 kwa wakati baraza linapohitajika)

  • Unyanyasaji wa mume au mke au mtu mzima (ona 38.6.2.4 kwa wakati baraza linapohitajika.

Aina ya Dhambi

Uasherati

Baraza la Uumini Linatakiwa (ona 32.6.1)

  • Kujamiiana kwa maharimu (kujamiiana kwa ndugu wa karibu)

  • Ponografia ya Watoto

  • Ndoa ya mitala

  • Tabia ya Unyanyasaji wa kijinsia.

Baraza la Uumini Linaweza Kuwa la Lazima (ona 32.6.2)

  • Uasherati, kujamiiana, na mahusiano ya jinsia moja.

  • Kukaa kinyumba, muungano wa kiraia na kuingia ubia wa kuishi pamoja, na ndoa ya jinsia moja

  • Matumizi makubwa au ya kulazimisha ya ponografia ambayo yamesababisha madhara kwa ndoa ya muumini au familia

Aina ya Dhambi

Vitendo vya Ulaghai

Baraza la Uumini Linatakiwa (ona 32.6.1)

  • Tabia ya Unyanyasaji wa Kifedha, kama vile ulaghai na shughuli zinazofanana

Baraza la Uumini Linaweza Kuwa la Lazima (ona 32.6.2)

  • Unyang’anyi, wizi wa kuvunja nyumba, wizi, au ubadhirifu

  • Kosa la kusema uongo chini ya kiapo

Aina ya Dhambi

Ukiukwaji wa Uaminifu

Baraza la Uumini Linatakiwa (ona 32.6.1)

  • Dhambi nzito wakati unashikilia nafasi maarufu ya Kanisa

Baraza la Uumini Linaweza Kuwa la Lazima (ona 32.6.2)

  • Dhambi nzito wakati anashikilia nafasi ya mamlaka au kuaminika katika Kanisa au jamii.

  • Dhambi nzito ambayo inajulikana sana

Aina ya Dhambi

Baadhi ya vitendo vingine

Baraza la Uumini Linatakiwa (ona 32.6.1)

  • Kupatikana na hatia kwa jinai zote

Baraza la Uumini Linaweza Kuwa la Lazima (ona 32.6.2)

  • Kutoa Mimba

  • Tabia ya dhambi nzito

  • Kutelekeza kwa makusudi wajibu wa familia, ikiwa ni pamoja na kutolipa msaada wa mtoto na masurufu.

  • Kuuza mihadarati (dawa za kulevya).

  • Vitendo vingine vizito vya jinai.

32.6.3

Wakati Rais wa Kigingi Anaposhauriana na Urais wa Eneo kuhusu kama Baraza la Uumini au Hatua Nyingine Ni lazima

Baadhi ya mambo yanahitaji kiwango cha ziada cha umakini na mwongozo. Kujua jinsi ya kusaidia vyema, rais wa kigingi lazima ashauriane na Urais wa Eneo kuhusu hali katika sehemu hii. Hata hivyo, Rais wa kigingi pekee ndiye anaamua kama baraza linapaswa kuitwa ili kushughulikia tabia. Kama baraza linakutana, rais wa kigingi au askofu anaamua matokeo.

Kama baraza la uumini linakutana kwa ajili ya moja ya mambo yaliyoainishwa katika sehemu hii, maamuzi ya baraza lazima “yabaki katika Msimamo Mzuri,” “vizuizi Rasmi vya Uumini,” au “uondoaji uumini,” Idhini ya Urais wa Kwanza inatakiwa kuondoa vizuizi rasmi au kumrudisha mtu ndani ya Kanisa (ona 32.16.1 nambari 9).

32.6.3.1

Vitendo vingine

Kama baraza la uumini halikutani, hatua nyingine inaweza kujumuisha:

  • Vizuizi visivyo rasmi (ona 32.8.3).

  • Ufafanuzi wa kumbukumbu ya uumini (ona 32.14.5)

  • Vizuizi vya ibada, ambavyo vinamzuia mtu kupokea au kutumia ukuhani au kupokea au kutumia kibali cha hekaluni.

Rais wa Kigingi anashauriana na Urais wa Eneo kabla ya mojawapo ya hatua hizi kuchukuliwa

32.6.3.2

Ukengeufu

Masuala ya ukengeufu mara nyingi yanaathari zaidi ya mipaka ya kata au kigingi. Yanahitaji kushughulikiwa haraka ili kuwalinda wengine.

Askofu anashauriana na rais wa kigingi kama anahisi kwamba kitendo cha muumini kinaweza kuwa ukengeufu. Askofu au rais wa kigingi anaweza kuweka vikwazo visivyo rasmi vya uumini kwa muumini (ona 32.8.3). Rais wa kigingi mara moja anashauriana na Urais wa Eneo. Hata hivyo, ni rais wa kigingi pekee anayeamua kama baraza la uumini au hatua nyingine ni lazima.

Kama lilivyotumika hapa, ukengeufu unamaanisha muumini kushiriki katika moja ya mambo yafuatayo:

  • Mara kwa mara kufanya kwa uwazi na kwa kudhamiria kuleta upinzani hadhrani kwa Kanisa, mafundisho yake, sera zake, au viongozi wake

  • Kuendelea kufundisha kama mafundisho ya Kanisa kile kisicho mafundisho ya Kanisa baada ya kusahihishwa na askofu au rais wa kigingi.

  • Kuonesha kwa makusudi mwelekeo wa kufanya mambo ili kudhoofisha imani na uhudhuriaji wa waumini wa Kanisa

  • Kuendelea kufuata mafundisho ya madhehebu yaliyokengeuka baada ya kusahihishwa na askofu au rais wa kigingi

  • Kujiunga rasmi na kanisa lingine na kushawishi mafundisho yake (Kutohudhuria kabisa katika Kanisa au kuhudhuria kanisa lingine kwa upekee wake hakujumuishi ukengeufu. Hata hivyo, kama muumini anajiunga rasmi na kanisa lingine na anatetea mafundisho yake, uondoaji wa uumini wake unaweza kuwa lazima.)

Mwokozi aliwafundisha Wanefi kwamba wanapaswa kuendelea kumhudumia mtu aliyefanya dhambi. “Lakini kama hatubu hatahesabiwa miongoni mwa watu wangu, ili asiwaharibu watu wangu” (3 Nefi 18:31).

32.6.3.3

Ubadhirifu wa Fedha za Kanisa

Kama mtu anafanya ubadhirifu wa fedha za Kanisa au anaiba mali za thamani za Kanisa, rais wa kigingi anashauriana na Urais wa Eneo kuhusu kama baraza la uumini au hatua nyingine inaweza kuwa lazima. Viongozi wanazingatia:

  • Kiasi kilichofanyiwa ubadhirifu au kuibwa.

  • Kama malipizo yametokea.

  • Kiwango cha majuto cha mtu.

Kwa ujumla, kama muumini wa Kanisa anafanya ubadhirifu wa fedha za Kanisa au anaiba mali za thamani za Kanisa, rekodi yake ya uumini itafafanuliwa. Wakati toba inakuwa imekamilika, rais wa kigingi anaweza kuomba uondoaji wa ufafanuzi (ona 32.14.5).

32.6.3.4

Watu Binafsi waliobadilisha jinsia

Maaskofu na marais wa vigingi wanaofanya kazi pamoja na watu wanaotambulika kama waliobadilisha jinsia wanapaswa kufuata miongozo katika 38.6.23.

32.6.4

Wakati Baraza la Uumini Kwa Kawaida Si La Lazima

Baraza la Uumini kwa kawaida si la lazima katika mifano ifuatayo.

32.6.4.1

Kushindwa Kukubaliana na Baadhi ya viwango vya Kanisa

Baraza la uumini halikutani kwa vitendo vilivyoorodheshwa hapo chini. Hata hivyo, tilia maanani upekee katika kipengele cha mwisho.

  • Kutohudhuria Kanisani

  • Kutokutimiza majukumu ya Kanisa

  • Kutolipa zaka

  • Dhambi za kushindwa kutimiza majukumu

  • Punyeto

  • Kutokutii Neno la Hekima

  • Kutumia ponografia, isipokuwa kwa ponografia ya watoto (kama ilivyoainishwa katika 38.6.6.) au matumizi makubwa au ya lazima ya ponografia ambayo yamesababisha madhara makubwa kwa ndoa ya muumini au familia (kama ilivyoainishwa katika 38.6.13).

32.6.4.2

Kuanguka kwa Biashara au Kutolipwa kwa Madeni

Viongozi hawapaswi kutumia mabaraza ya uumini kuamua migogoro ya biashara. Kuanguka kwa biashara na kutolipwa kwa madeni sio sababu za kuwa na mkutano wa baraza la uumini. Hata hivyo, baraza lazima likae kwa ajili ya shughuli za udanganyifu mkubwa au udanganyifu mwingine mkubwa wa matumizi ya fedha (ona 32.6.1.3)

32.6.4.3

Migogoro ya Kiraia

Mabaraza ya Uumini hayakai kusuluhisha migogoro ya kiraia (ona Mafundisho na Maagano 134:11).

32.7

Hali za mtu

Bwana alisema, “Mkono wangu wa rehema umenyoshwa kwenu, na yeyote atakayekuja, nitampokea; na heri ni wao ambao huja kwangu” (3 Nefi 9:14). Hali za mtu ni zingatio muhimu katika kuamua:

  • Mazingira yanayofaa kwa ajili ya kumsaidia yeye kutubu dhambi nzito (ona 32.5 na 42.6).

  • Maamuzi yaliyofanywa katika ushauri binafsi au baraza la uumini (ona 32.8 na 32.11).

Maaskofu na marais wa vigingi wanatafuta mawazo na mapenzi ya Bwana kwa kila hali. Wanazingatia vipengele vifuatavyo katika kuamua mazingira gani ya kutumia na nini matokeo yake yatakuwa. Vipengele hivi haviamuru uamuzi fulani. Bali, kuna misaada kwa maamuzi ambayo viongozi wanafanya kwa sala na kadiri wanavyoongozwa na Roho.

32.7.1

Ukubwa wa Dhambi

Uzito wa dhambi unapimwa kwa ukubwa wake. Hii inaweza kujumuisha idadi na marudio ya dhambi zilizofanywa, ukubwa wa madhara yanayotokea kutokana nazo, na idadi ya watu walioumizwa nazo.

32.7.2

Mapendeleo ya Mhanga

Viongozi wanazingatia mapendeleo ya wahanga na watu wengine. Hii inaweza kujumuisha mume au mke wa mtu na wanafamilia wengine. Viongozi pia wanazingatia ukubwa wa madhara.

32.7.3

Ushahidi wa Toba

Mwongozo wa Kiroho unahitajika kubaini kama mtu ametubu kwa dhati. Toba kama hiyo inaoneshwa zaidi kwa kuaminika na vitendo adilifu baada ya muda fulani kuliko kwa huzuni wakati wa usaili mmoja. Vipengele vya kuzingatia vinajumuisha:

  • Uimara wa imani katika Yesu Kristo.

  • Uhalisia wa kuungama.

  • Kina cha huzuni kwa ajili ya dhambi.

  • Masahihisho kwa watu walioumia.

  • Kukubaliana na Masharti ya kisheria.

  • Mafanikio katika kuiacha dhambi.

  • Uaminifu katika kutii amri tangu dhambi hiyo.

  • Uaminifu kwa viongozi wa Kanisa na watu wengine

  • Utayari wa kufuata ushauri wa viongozi wa Kanisa.

Picha
mwanamke akisali

32.7.4

Ukiukwaji wa Maagano ya Hekaluni

Bwana alitangaza, “Kwani yule aliyepewa vingi kwake huyo vitatakiwa vingi” (Mafundisho na Maagano 82:3). Mtu ambaye amepokea endaumenti ya hekaluni amefanya maagano kuishi kiwango cha juu. Kukiuka maagano haya kunaongeza uzito wa dhambi. Kunaongeza uwezekano wa baraza la uumini kuwa la lazima.

32.7.5

Nafasi ya Kuaminiwa au Mamlaka

Uzito wa dhambi unaongezeka kama mtu imeifanya akiwa katika nafasi ya kuaminiwa au mamlaka, kama vile mzazi, kiongozi, au mwalimu.

32.7.6

Urudiaji

Tabia ya kurudia dhambi ileile nzito inaweza kuonesha tabia ya kina iliyokita mizizi au uraibu ambao unazuia maendeleo kuelekea toba ya kweli. Kwa nyongeza kwenye vizuizi vya uumini ambavyo vinaweza kuwa vya lazima, programu za kupata nafuu ya uraibu na ushauri wa kitaalamu vinaweza kuwa vyenye msaada (ona 32.8.2).

32.7.7

Umri, Kupevuka, na Uzoefu

Viongozi wanazingatia umri, kupevuka, na uzoefu pale wanapomshauri muumini au kuamua matokeo ya baraza la uumini. Upole mara nyingi unafaa kwa ajili ya wale ambao hawajapevuka katika injili. Kwa mfano, upole unaweza kufaa kwa ajili ya waumini wenye umri mdogo wanaoshiriki katika tabia isiyo adilifu kama wanaacha dhambi na kuonesha toba ya kweli. Hata hivyo, hatua kubwa zaidi zinaweza kuhitajika kama wataendelea katika tabia hiyo.

32.7.8

Uwezo wa Kiakili

Ugonjwa wa akili, uraibu, au upungufu wa uwezo wa akili haumpi uhalali mtu aliyefanya dhambi nzito. Hata hivyo, hivi ni vipengele vya kuzingatia. Kama sehemu ya kumsaidia mtu kutubu, viongozi wanaomba mwongozo wa Bwana kuhusu uelewa wa mtu wa kanuni za injili na kiwango cha uwajibikaji.

32.7.9

Kuungama kwa Hiari

Kuungama kwa hiari na huzuni ya kimungu kwa ajili ya matendo ya mtu inaonesha tamanio la kutubu.

32.7.10

Muda kati ya Dhambi na Kuungama

Kuungama ni sehemu ya kutubu na hakupaswi kucheleweshwa. Wakati mwingine dhambi inafuatiwa na kipindi kirefu cha masahihisho na kuishi kwa uaminifu. Kama muumini anaungama dhambi na hakuirudia, hiyo inaweza kuonesha kwamba yeye ameiacha. Katika mfano huo, kuungama kunaweza kukamilisha badala ya kuanzisha mchakato wa toba.


KUTOA USHAURI BINAFSI


32.8

Ushauri Binafsi na Vizuizi visivyo Rasmi vya Uumini

Ushauri binafsi mara nyingi unatosha kusaidia kuwalinda wengine na kumsaidia mtu kupata nguvu ya ukombozi ya upatanisho wa Yesu Kristo kupitia toba. Ushauri kama huo unaweza pia kuwasaidia waumini kujilinda dhidi ya dhambi nzito. Katika ushauri binafsi, viongozi wanaweza pia kutoa vizuizi visivyo rasmi vya uumini ili kumsaidia muumini afanye toba ya dhambi nzito (ona 32.8.3).

Dhambi nzito hazipaswi kuchukuliwa kirahisi (ona Mafundisho na Maagano 1:31). Kukiuka maagano ya hekaluni kunaongeza uwezekano wa baraza la uumini kuwa la lazima (ona 32.7.4).

Miongozo ya kusaidia viongozi wajue ni wakati gani kushauri na vizuizi visivyo rasmi vinaweza kutosha imeorodheshwa hapo chini (ona pia 32.7):

  • Mtu hajafanya dhambi ambayo ingehitaji baraza la uumini (ona 32.6.1).

  • Mtu ameungama kwa hiari na ametubu kwa dhati.

  • Mtu anatubu juu ya dhambi kubwa ambayo hajawahi kuifanya hapo awali.

  • Dhambi ya mtu yule haijakiuka maagano ya hekaluni.

  • Mtu ana hali muhimu ya kupunguza uzito wa dhambi.

32.8.1

Ushauri Binafsi

Miongozo ifuatayo inatumika wakati askofu au rais wa kigingi anamshauri muumini ili kumsaidia atubu.

  • Omba tu taarifa za kutosha kuamua (1) mtazamo wa muumini kwenye tabia ya kutenda dhambi na (2) asili, marudio, na muda wa tabia. Usiombe maelezo zaidi ya yale yaliyo ya lazima ili kuelewa hali. Usiulize maswali ambayo yanatokea kutokana na udadisi binafsi.

  • Uliza jinsi tabia ilivyowaathiri wengine.

  • Lenga kwenye hali chanya ambazo zinaongeza uongofu wa muumini na kujitolea kwa Bwana. Mtie moyo muumini kuchukua hatua maalumu ili kuleta mabadiliko ya tabia na mabadiliko ya moyo kwa ajili ya kutubu. Mwalike kuwa karibu na Mwokozi, akitafuta nguvu Yake na kuhisi upendo Wake wa ukombozi.

  • Himiza shughuli za kuinua kama vile kusali, kujifunza maandiko, na kuhudhuria mikutano ya Kanisa. Fundisha kwamba historia ya familia na kazi ya hekalu vinaweza kupunguza ushawishi wa adui. Himiza kuwahudumia wengine na kushiriki injili.

  • Himiza ufanywaji wa masahihisho kwa wale waliopata madhara ya dhambi na uombaji msamaha.

  • Himiza kujitenga mbali na ushawishi mbaya. Saidia waumini kuchukua hatua za kiulinzi ili kupinga majaribu maalum.

  • Tambua kwamba wewe ni kiongozi wa Kanisa la Kristo, sio mshauri wa kitaalamu. Kwa nyongeza kwenye ushauri unaoutoa, baadhi ya waumini watafaidika kutokana na ushauri wa kitabia. Baadhi wanateseka kutokana na ugonjwa wa akili. Kama inavyohitajika, washauri waumini kuomba msaada kutoka wataalamu wenye sifa zinazostahili za kitabibu na afya ya akili.

  • Kuwa mwenye kuomba na tafuta mwongozo kutoka kwa Roho kabla ya kutoa vizuizi visivyo rasmi. Baadhi ya waumini wanaweza kunufaika kutokana na kutumia fursa za uumini wa Kanisa kwa kushiriki kikamilifu kuliko kuzuiliwa.

  • Fuatilia ili kuhimiza, kuimarisha nguvu za kiroho, na kusimamia maendeleo.

Baada ya muumini kuungama kwa askofu au rais wa kigingi, ushauri wa kufuatilia unaweza kutokea katika njia kadhaa. Kiongozi mwenyewe anaweza kuutoa. Au, kwa ruhusa ya muumini, anaweza kumpanga mmoja wa washauri wake kuutoa.

Kwa makubaliano ya muumini, askofu au rais wa kigingi anaweza kuwapangia washiriki wa akidi ya wazee au Muungano wa Usaidizi kusaidia katika njia maalumu. Kwa vijana, anaweza kuwapangia urais wa Wasichana au washauri wa akidi ya Ukuhani wa Haruni kusaidia. Wale ambao wamepangiwa kusaidia wamepewa haki ya kupata msukumo ili kukamilisha jukumu hilo (ona 4.2.6).

Mtu fulani anapopangiwa kusaidia kwa ushauri wa kufuatilia, kiongozi anatoa taarifa ya lazima inayotosha tu kumsaidia muumini. Mtu aliyepangiwa lazima adumushe usiri. Yeye pia anamtaarifu askofu juu ya maendeleo na mahitaji ya muumini.

32.8.2

Kuwasaidia Watu wenye Uraibu

Ushauri binafsi wakati mwingine unahusisha kuwasaidia waumini watubu dhambi zao zenye uhusiano na, au zilizosababishwa na uraibu. Uraibu huu unaweza kujumuisha vitu au mlolongo mpana wa tabia. Uraibu unaleta madhara kwa watu binafsi, ndoa, na familia. Maaskofu wanaweza kuwashauri waumini kuomba msaada kutoka programu za Kanisa za kupata ahueni ya uraibu na kutoka kwa wataalamu wenye sifa zinazostahili za kitabibu na afya ya akili.

Uraibu unaojulikana sana unaoongezeka ni matumizi ya ponografia. Iwe ni uraibu au tabia ya mara moja, matumizi ya ponografia ya aina yoyote yana madhara. Kuyatumia humfukuza Roho Mtakatifu. Yanadhoofisha uwezo wa kuvuta nguvu ambazo zinakuja kutokana na kutunza maagamo. Yanaleta pia madhara kwenye mahusiano ya thamani.

Ushauri binafsi na vizuizi vya uumini visivyo rasmi kwa kawaida vinatosha kwa ajili ya kumsaidia mtu atubu kutokana na kutumia ponografia. Mabaraza la Uumini kwa kawaida hayakai. Kwa upekee, ona 38.6.6 na 38.6.13. Ushauri wa kitaalamu unaweza kusaidia.

Marais wa vigingi na maaskofu wanawasaidia wanafamilia kama inavyohitajika. Wazazi wangeweza kujumuishwa wakati wa kuwashauri vijana kuhusu matumizi ya ponografia. Mwenza anaweza kujumuishwa wakati wa kumshauri mwana ndoa.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kuwashauri waumini wanaohusika na ponografia, ona 38.6.13.

32.8.3

Vizuizi vya Uumini Visivyo Rasmi

Kwa nyongeza kwenye kutia moyo vitendo chanya wakati anaposhauri, askofu au rais wa kigingi anaweza isivyo rasmi kuzuia baadhi ya fursa za uumini wa Kanisa kwa muda fulani. Vikitolewa kwa busara, vizuizi hivi vinaweza kusaidia kwenye toba na maendeleo ya kiroho. Vinafikiriwa visivyo rasmi kwa sababu havikuandikwa kwenye kumbukumbu za uumini.

Vizuizi visivyo rasmi vinaweza kwisha baada ya wiki chache, miezi kadhaa, au kwa muda mrefu kama ni lazima kwa mtu kutubu kikamilifu. Katika hali zisizo za kawaida, muda unaweza kuwa mrefu zaidi ya mwaka mmoja.

Viongozi wanaomba mwongozo wa Roho kuhusu vizuizi gani vitamsaidia vizuri zaidi mtu kutubu. Hivi vinajumuisha (lakini havikomei hapo) kusimamisha fursa ya kuhudumia katika wito wa Kanisa, kutumia ukuhani, au kuingia hekaluni. Kiongozi anaweza pia kumzuia mtu kuhubiri, kutoa somo, au sala katika mipangilio ya Kanisa. Kama kiongozi anasimamisha fursa ya kuingia hekaluni, anafuta kibali cha hekaluni katika Leader and Resources (LCR).

Kushiriki sakramenti ni sehemu muhimu ya kutubu. Haipaswi kuwa zuio la kwanza kutolewa kwa mtu anayetubu aliye na moyo uliovunjika na roho iliyopondeka. Hata hivyo, kama mtu amefanya dhambi nzito, kiongozi anaweza kusimamisha fursa hii kwa muda.

Viongozi kwa kawaida hawamwambii mtu mwingine yoyote kuhusu vizuizi visivyo rasmi isipokuwa kama kuna haja ya kujua (ona 32.12.2).

Askofu au rais wa kigingi anaweza kuondoa vizuizi visivyo rasmi kama anavyoongozwa na Roho wakati mtu anapoonesha maendeleo kwenye toba ya kweli. Kama muumini anaendelea katika mpangilio wa dhambi, inaweza kuwa yenye kusaidia au kulazimu kuitisha baraza la uumini.

Picha
mwanamke akiomba

KUSIMAMIA MABARAZA YA UUMINI YA KANISA


Mabaraza ya uumini ya Kanisa yanafanywa wakati askofu au rais wa kigingi wanapoamua kwamba yatakuwa yenye kusaidia au wakati yanapohitajika kwenye sera za Kanisa (ona 32.6). Yanafanywa kwenye ngazi ya kata, kigingi, tawi, au misheni. Sehemu hii inatoa taarifa kuhusu jinsi ya kuyasimamia.

32.9

Ushiriki na Majukumu

Jedwali lifuatalo linaonesha nani kwa kawaida anashiriki katika mabaraza ya uumini.

Washiriki katika Mabaraza ya Uumini

Baraza la Uumini la Kata

Washiriki katika Mabaraza ya Uumini

  • Mtu ambaye baraza linakutana kwa ajili yake

  • Askofu na washauri wake

  • Karani wa kata

  • Rais wa Akidi ya wazee au rais wa Muungano wa Usaidizi (hiari; ona 32.10.1)

Baraza la Uumini la Kigingi

Washiriki katika Mabaraza ya Uumini

  • Mtu ambaye baraza linakutana kwa ajili yake

  • Rais wa kigingi na washauri wake

  • Karani wa kigingi

  • Washauri wakuu (katika hali zenye ukomo kama ilivyoelezwa katika 32.9.2)

  • Askofu wa mtu ambaye baraza linakutana kwa ajili yake (hiari; ona 32.9.3)

  • Rais wa Akidi ya wazee au rais wa Muungano wa Usaidizi (hiari; ona 32.10.1)

32.9.1

Rais wa Kigingi

Rais wa kigingi:

  • Ana mamlaka juu ya mabaraza ya uumini katika kigingi; hata hivyo, mengi ya mabaraza haya yanaitishwa na maaskofu.

  • Lazima atoe kibali kabla ya askofu kuitisha baraza la uumini.

  • Anaitisha baraza la uumini la kigingi kama mwanamume au mwanamke ambaye amepokea endaumenti ya hekaluni yuko hatarini kuondolewa uumini wake wa Kanisa.

  • Anaweza kuitisha baraza kama muumini anakata rufaa dhidi ya uamuzi wa baraza la uumini la kata.

  • Lazima atoe kibali kabla ya pendekezo la baraza la uumini la kata la kuondoa uumini wa mtu asiye na endaumenti haujafika mwisho.

32.9.2

Baraza Kuu

Washiriki wa baraza kuu kwa kawaida hawashiriki katika mabaraza ya uumini ya kigingi. Hata hivyo, baraza kuu linaweza kushiriki katika hali ngumu (ona Mafundisho na Maagano 102:2). Kwa mfano, urais wa kigingi unaweza kualika baraza kuu kushiriki wakati:

  • Kuna ukweli unaokanwa.

  • Wataongeza thamani na usawa.

  • Muumini anapoomba ushiriki wao.

  • Mshiriki wa urais wa kigingi au familia yake inahusika (ona 32.9.7).

32.9.3

Askofu (au Rais wa Tawi katika Kigingi)

Askofu:

  • Ana mamlaka juu ya mabaraza ya uumini ya kata.

  • Anashauriana na rais wa kigingi na anapata kibali chake kabla ya kuitisha baraza.

  • Anaweza asiitishe baraza kama mwanamume au mwanamke aliyepokea endaumenti ya hekaluni yuko hatarini kuondolewa uumini wake wa Kanisa. Baraza la uumini la kigingi lazima liitishwe katika hali hizo.

  • Anaweza kualikwa kuhudhuria baraza la uumini la kigingi kwa ajili ya muumini wa kata ambaye uumini wake unarejewa. Mahudhurio yake lazima yapate kibali cha rais wa kigingi na mtu mwenyewe.

Baraza la uumini la kata au tawi linaweza kupendekeza uondoaji uumini wa Kanisa wa mtu ikiwa mtu huyo hajapokea endaumenti. Hata hivyo, kibali cha rais wa kigingi kinahitajika kabla maamuzi hayajafika mwisho.

Wakati mwingine baraza la uumini la kata linaitishwa kwa ajili ya muumini aliyepokea endaumenti na jambo lililofanywa linaonesha kwamba uumini wake uko hatarini kuondolewa. Katika hali hizi, askofu anapeleka suala hilo kwa rais wa kigingi.

32.9.4

Rais wa Misheni

Rais wa misheni:

  • Ana mamlaka juu ya mabaraza ya uumini katika matawi na wilaya za misheni.

  • Lazima atoe kibali kabla ya rais wa wilaya au wa tawi kuitisha baraza la uumini.

  • Anaitisha baraza la uumini kama mwanamume au mwanamke ambaye amepokea endaumenti ya hekaluni yuko hatarini kuondolewa uumini wake wa Kanisa. Kama muda, au umbali unazuia hili, anaweza kumteua mmoja wa washauri wake aongoze baraza. Anateua wawili wengine wenye Ukuhani wa Melkizediki kushiriki.

  • Inapowezekana, anaitisha baraza la uumini kwa ajili ya wale ambao hawajapata endaumenti. Kama muda, au umbali unazuia hili, anaweza kuwapa mamlaka watu watatu wanaoshikilia ukuhani wa Melkedeziki kuitisha baraza. Katika hali hii, rais wa wilaya wa muumini au rais wa tawi kwa kawaida anaendesha baraza.

  • Anaweza kuitisha baraza kama muumini anakata rufaa dhidi ya uamuzi wa baraza la wilaya au la tawi.

  • Kwa kibali cha Kiongozi Mkuu Mwenye Mamlaka kutoka Idara ya Wamisionari, anaitisha baraza la uumini kama mmisionari anafanya dhambi nzito katika eneo la misheni (ona 32.9.8) Pia anapitia suala hilo pamoja na mshiriki wa Urais wa Eneo na anashauriana na rais wa kigingi cha nyumbani cha mmisionari.

  • Lazima atoe kibali kabla ya pendekezo la baraza la tawi au la wilaya la kuondoa uumini wa mtu asiye na endaumenti ni la mwisho.

Kama mmisionari anaungama dhambi nzito ambayo aliifanya kabla ya kuhudumu misheni, rais wa misheni anawasiliana na mwakilishi wake aliye kwenye eneo katika Idara ya Wamisionari kwa ajili ya mwongozo.

Wakati rais wa misheni anapoitisha baraza la uumini, anateua watu wawili wanaoshikilia ukuhani wa Melkizedeki ili kumsaidia. Ni katika hali isiyo ya kawaida pekee ndipo anapaswa kuwateua wamisionari vijana kumsaidia. Anafuata taratibu zilezile kama katika baraza la uumini la kigingi (ona 32.10). Hata hivyo, baraza kuu au baraza la wilaya halishiriki.

32.9.5

Rais wa Wilaya au Tawi katika Misheni

Rais wa Wilaya au Tawi katika misheni anaweza kuitisha baraza la uumini wakati wanaporuhusiwa na rais wa misheni. Baraza la wilaya halishiriki.

Baraza la uumini la wilaya au tawi linaweza kupendekeza kuondolewa uumini wa Kanisa wa mtu kama hajapokea endaumenti ya hekaluni. Hata hivyo, kibali cha rais wa misheni kinahitajika kabla maamuzi hayajafika mwisho.

32.9.6

Karani wa Kata au Kigingi

Karani wa Kata au Kigingi:

  • Anatunza muhtasari ulioandikwa wa baraza kadiri tu ambavyo ni muhimu kuwasilisha fomu ya Ripoti ya Uumini wa Kanisa.

  • Anatayarisha fomu kama ameombwa na kiongozi aliyeendesha baraza.

  • Hashiriki katika majadiliano au maamuzi katika baraza.

32.9.7

Ushiriki katika Hali Zisizo za Kawaida

Kama mshauri katika urais wa kigingi hawezi kushiriki katika baraza la uumini, rais wa kigingi anamwomba mshauri mkuu au kuhani mkuu mwingine kuchukua nafasi yake. Kama rais wa kigingi hawezi kushiriki, Urais wa Kwanza unaweza kuamuru mmoja wa washauri wake kusimamia badala yake.

Kama mshauri katika uaskofu hawezi kushiriki katika baraza la uumini, askofu anaweza kumwomba kuhani mkuu katika kata kuchukua nafasi yake. Kama askofu hawezi kushiriki, anapeleka suala kwa rais wa kigingi, ambaye anaitisha baraza la uumini la kigingi. Askofu anaweza asimpange mshauri kuitisha baraza la uumini.

Kama baraza la uumini linaitishwa kwa ajili ya mwanafamilia wa askofu au mmoja wa washauri wake, linaitishwa katika ngazi ya kigingi. Kama linaitishwa kwa ajili ya mwanafamilia wa mmoja wa washauri wa rais wa kigingi, rais wa kigingi anampangia kuhani mkuu mwingine kuchukua nafasi ya mshauri. Kama baraza linaitishwa kwa ajili ya mwanafamilia wa rais wa kigingi, anashauriana na Ofisi ya Urais wa Kwanza.

Kama muumini anapinga ushiriki wa askofu au washauri wake, baraza la uumini linaitishwa katika ngazi ya kigingi. Kama muumini anapinga ushiriki wa mmoja wa washauri wa rais wa kigingi, rais wa kigingi anampanga kuhani mkuu mwingine kuchukua nafasi ya mshauri. Kama muumini anapinga ushiriki wa rais wa kigingi, au kama rais wa kigingi anahisi kwamba hawezi kuleta usawa, anashauriana na Ofisi ya Urais wa Kwanza.

32.9.8

Kuamua Kiongozi Gani Anaitisha Baraza katika Hali Maalumu

Mabaraza ya uumini takriban mara zote huitishwa katika kitengo cha kijiografia cha Kanisa ambacho kina kumbukumbu ya uumini wa mtu.

Wakati mwingine baraza la uumini ni lazima kwa ajili ya mtu anayehama. Kama uhamisho ni ndani ya kigingi kile kile, rais wa kigingi anashauriana na maaskofu wa kata zote mbili na kuamua wapi litafanyika.

Kama muumini anahamia nje ya kigingi, marais wa vigingi vyote viwili wanashauriana na kuamua wapi baraza linapaswa kufanyika. Kama wanaamua kwamba linapaswa kuitishwa katika kata au kigingi cha awali, kumbukumbu ya uumini inabakizwa katika kata ile mpaka baraza linapokuwa limemalizika. Vinginevyo, kumbukumbu inahamishiwa kwenye kata mpya. Askofu au rais wa kigingi kwa siri anamfahamisha askofu wa sasa wa muumini kuhusu kwa nini baraza linahitajika.

Wakati mwingine baraza la uumini ni lazima kwa ajili ya muumini anayeishi mbali na nyumbani kwa muda. Kwa mfano, baraza linaweza kuhitajika kwa ajili ya mwanafunzi au muumini aliye jeshini. Askofu ambapo muumini anaishi kwa muda anaweza kutoa ushauri na msaada. Hata hivyo, hapaswi kuitisha baraza la uumini isipokuwa kumbukumbu ya uumini iko kwenye kitengo chake na ameshauriana na askofu wa kata ya nyumbani.

Wakati mwingine mmisionari anafanya dhambi nzito katika eneo la misheni ambayo haifichuliwi mpaka baada ya yeye kupumzishwa. Askofu na rais wa kigingi wanashauriana kuhusu nani kati yao anapaswa kuitisha baraza la uumini. Mmoja wao anashauriana na rais wa misheni wa mwanzo kabla ya kuitisha baraza.

32.10

Taratibu kwa ajili ya Mabaraza ya Uumini

32.10.1

Toa Taarifa na Fanya Matayarisho kwa ajili ya Baraza

Askofu au rais wa kigingi anatoa taarifa ya maandishi ya baraza la uumini kwa muumini ambalo litafanyika kwa niaba yake. Anasaini barua. Inajumuisha taarifa zifuatazo:

“[Uaskofu au urais wa kigingi] unaitisha baraza la uumini kwa niaba yako. Baraza litafanyika [terehe na muda] [sehemu].

“Baraza hili litazingatia [fanya muhtasari wa mwenendo mbaya kwa ujumla, lakini usitoe maelezo ya kina au ushahidi].

“Unaalikwa kuhudhuria baraza ili kutoa majibu yako. Unaweza kutoa maelezo kwa maandishi kutoka kwa watu ambao wanaweza kutoa taarifa husika. Unaweza kuwaalika watu hao kuzungumza kwenye baraza kwa niaba yako kama wameidhinishwa mapema na rais wa kigingi au askofu. Unaweza pia kuwaalika [rais wa Muungano wa Usaidizi au rais wa akidi ya wazee] wawepo na kutoa msaada.

“Yoyote anayehudhuria lazima awe tayari kukubaliana na asili ya heshima ya baraza, ikiwa ni pamoja na taratibu zake na usiri. Mshauri wa kisheria na watetezi zaidi ya wale waliotajwa hapo juu hawatakiwi kuwepo.”

Ibara ya mwisho inaweza kujumuisha hisia ya upendo, matumaini, na wasiwasi.

Mwongozo kuhusu ni nani mtu anaweza kumwalika kuzungumza kwenye baraza umetolewa katika 32.10.3. Namba 4.

Kama barua haiwezi kuwasilishwa na mtu binafsi, inaweza kutumwa kwa rejista au barua halali, pamoja na ombi la stakabadhi ya urejeshaji.

Askofu au rais wa kigingi anapanga baraza la uumini kwenye muda ambao unafaa kwa mtu. Pia anahakikisha kwamba pamekuwa na muda wa kupata maelezo kutoka kwa wahanga wa tabia mbaya kama wanapenda kuyatoa (ona 32.10.2).

Askofu au rais wa kigingi anamtayarisha muumini kwa ajili ya baraza kwa kumweleza azma na taratibu zake. Pia anaelezea maamuzi ambayo baraza linaweza kufikia na matokeo yake. Kama muumini ameungama, kiongozi anaelezea kwamba ungamo litahitajika kutumika katika baraza la uumini.

32.10.2

Pata Maelezo kutoka kwa Wahanga

Wakati muumini wa Kanisa ni mhanga (kama vile kwa kujamiiana kwa maharimu, uyanyasaji wa watoto, unyanyasaji wa mke au mume, au udanganyifu), askofu au rais wa kigingi anawasiliana na askofu au rais wa kigingi wa sasa wa mtu yule. Viongozi hawa wanaamua ikiwa itasaidia kumpa mhanga fursa ya kutoa maelezo ya maandishi kuhusu tabia mbaya na madhara yake. Maelezo haya yanaweza kusomwa katika baraza la uumini (ona 32.10.3, namba 3). Viongozi wa Kanisa hawana mamlaka kuanzisha mawasiliano na wahanga ambao sio waumini wa Kanisa.

Mkutano wowote na mhanga kwa ajili ya azma hii unaitishwa na askofu au rais wake wa kigingi wa sasa. Kama mhanga anatoa maelezo, kiongozi huyu anayapeleka kwa askofu au rais wa kigingi ambaye anaitisha baraza la uumini. Viongozi lazima wachukue tahadhari kubwa kuepuka kiwewe zaidi.

Uchunguzi wowote kuhusu mhanga ambaye yupo chini ya miaka 18 unafanywa kupitia wazazi au walezi halali wa mtoto, isipokuwa tu kama kufanya hivyo kunaweza kumweka mhanga hatarini.

Kwa maelezo kuhusu maaskofu na marais wa vigingi kupokea mwongozo katika mambo ya unyanyasaji, ona 32.4.5 na 38.6.2.1.

32.10.3

Endesha Baraza

Punde kabla baraza halijaanza, askofu au rais wa kigingi anawaeleza washiriki ambao baraza ni kwa ajili yao na kuhusu tabia mbaya iliyoripotiwa. Kama ni lazima, anaelezea taratibu za baraza.

Mtu, kama yupo, kisha anakaribishwa ndani ya chumba. Kama askofu amealikwa kuhudhuria baraza la uumini la kigingi, yeye pia anaalikwa ndani ya chumba wakati huu. Kama mtu alimwalika rais wa Muungano wa Usaidizi wa kata au rais wa akidi ya wazee kuwepo na kutoa utetezi, yeye pia anakaribishwa ndani ya chumba.

Askofu au rais wa kigingi anaongoza baraza kwa roho ya upendo, kama ilivyoainishwa hapo chini.

  1. Anamwalika mtu kutoa sala ya ufunguzi.

  2. Anaeleza tabia mbaya iliyoripotiwa. Anampa mtu (kama yupo) fursa ya kuthibitisha, kukana, au kufafanua maelezo haya.

  3. Kama muumini anathibitisha tabia mbaya, askofu au rais wa kigingi anaendelea kwenye namba 5 hapo chini. Kama muumini akikana, askofu au rais wa kigingi anawasilisha taarifa kuhusu hilo. Hii inaweza kujumuisha kuonesha nyaraka za kuaminika na kusoma kwa sauti maelezo yoyote ya kimaandishi kutoka kwa wahanga (ona 32.10.2). Kama anasoma maelezo kama hayo, analinda utambulisho wa mhanga.

  4. Kama muumini akikataa tabia mbaya, anaweza kutoa taarifa kwenye baraza. Hii inaweza kuwa taarifa ya maandishi. Au muumini anaweza kuomba watu ambao wanaweza kutoa taarifa husika kuzungumza kwenye baraza, mmoja baada ya mwingine. Watu kama hao wanapaswa kuwa waumini wa Kanisa isipokuwa kama askofu au rais wa kigingi ameamua mapema kwamba asiye muumini anaweza kuhudhuria. Wanasubiri katika chumba tofauti hadi pale wanapoombwa kuzungumza. Kila mtu anaondoka kutoka chumba cha baraza wakati anapomaliza. Lazima wawe tayari kukubaliana na asili ya heshima ya baraza ikiwa ni pamoja na taratibu zake na usiri. Waumini hawapaswi kuwa na mshauri wa kisheria. Wala hawawezi kuwa na mashabiki zaidi ya wale waliotajwa katika ibara ya pili katika sehemu hii.

  5. Askofu au rais wa kigingi anaweza kumuuliza muumini maswali kwa njia ya upole na kwa heshima. Anaweza pia kuwauliza maswali watu wengine ambao muumini amewaomba watoe taarifa. Washauri katika uaskofu au urais wa kigingi wanaweza pia kuuliza maswali. Maswali yoyote yanapaswa kuwa mafupi na yenye ukomo kwenye kweli muhimu.

  6. Baada ya taarifa zote husika kutolewa, askofu au rais wa kigingi anamruhusu muumini kutoka kwenye chumba. Karani pia anaruhusiwa, isipokuwa kama baraza kuu limeshiriki katika baraza la uumini la Kigingi. Kama askofu wa muumini yupo kwa ajili ya baraza la uumini la kigingi, anaruhusiwa kuondoka. Kama rais wa Muungano wa Usaidizi au rais wa akidi ya wazee anahudhuria kutoa msaada, yeye pia anaruhusiwa.

  7. Askofu au rais wa kigingi anaomba maoni au utambuzi kutoka kwa washauri wake. Kama baraza kuu limeshiriki katika baraza la uumini la kigingi, anaomba maoni yao na utambuzi.

  8. Pamoja na washauri wake, askofu au rais wa kigingi kwa maombi wanaomba mapenzi ya Bwana kuhusu mada. Rais wa kigingi na washauri wake pekee au askofu na washauri wake pekee wanapaswa kuwa ndani ya chumba wakati huu. Kama baraza la uumini la kigingi linajumuisha baraza kuu, urais wa kigingi kwa kawaida unakwenda kwenye ofisi ya rais wa kigingi.

  9. Askofu au rais wa kigingi anawaeleza washauri wake juu ya uamuzi wake na anawaomba wauidhinishe. Kama baraza la uumini la kigingi linajumuisha baraza kuu, urais wa kigingi unarudi chumbani na kuliomba baraza kuu kuuidhinisha. Kama mshauri au mshauri mkuu ana wazo tofauti, askofu au rais wa kigingi anasikiliza na kutafuta kutatua tofauti. Jukumu kwa ajili ya maamuzi liko mikononi mwa afisa kiongozi.

  10. Anamrudisha mtu chumbani. Kama karani aliruhusiwa, anarudishwa pia ndani ya chumba. Kama askofu wa muumini yupo kwa ajili ya baraza la uumini la kigingi, pia anaalikwa ndani ya chumba. Kama rais wa Muungano wa Usaidizi au rais wa akidi ya wazee anahudhuria kutoa msaada, wao pia wanakaribishwa tena.

  11. Askofu au rais wa kigingi anashiriki maamuzi ya baraza katika roho ya upendo. Kama uamuzi ni kuzuia rasmi fursa za uumini wa Kanisa au kuondoa uumini, anaelezea masharti (ona 32.11.3 na 32.11.4). Pia anaelezea jinsi ya kushinda vizuizi na anatoa maelekezo mengine na ushauri. Askofu au rais wa kigingi anaweza kuahirisha baraza kwa muda kutafuta mwongozo au taarifa zaidi kabla kufanya uamuzi. Katika hali kama hiyo, anaelezea haya.

  12. Anaelezea haki ya mtu kukata rufaa (ona 32.13)

  13. Anamwalika mtu kutoa sala ya kufunga.

Iwe mtu yupo au la, askofu au rais wa kigingi anamfahamisha juu ya uamuzi kama ilivyoelezwa katika 32.12.1.

Hakuna mshiriki katika baraza la uumini anaruhusiwa kurekodi sauti, video au rekodi ya maandishi. Karani anaweza kuandika muhtasari kwa kusudi la kutayarisha Ripoti ya Baraza la Uumini la Kanisa. Hata hivyo, muhtasari huo usiwe wa neno kwa neno au nakala. Baada ya ripoti kuandaliwa, mara moja anaharibu mihutasari yote.

32.11

Maamuzi kutoka Mabaraza ya Uumini

Maamuzi kutoka mabaraza ya Uumini yanapaswa kuelekwezwa na Roho. Yanapaswa kuonesha upendo na matumaini yanayotolewa na Mwokozi kwa wale wanaotubu. Maamuzi yanayowezekana yameelezwa hapo chini. Wakati wa kufanya maamuzi haya, viongozi wanazingatia mazingira ambayo yameainishwa katika 32.7.

Baada ya baraza lolote la uumini, askofu au rais wa kigingi mara moja anapeleka fomu ya Ripoti ya Baraza la Uumini la Kanisa kupitia LCR (ona 32.14.1).

Maamuzi yanayowezekana kutoka mabaraza ya uumini yameainishwa katika sehemu zifuatazo.

32.11.1

Anabaki katika Msimamo Mzuri

Katika baadhi ya hali, mtu anaweza kuwa hana hatia na anabaki katika msimamo mzuri. Katika baadhi ya hali, mtu anaweza kuwa amefanya dhambi, ametubu kwa dhati, na kuwa katika msimamo mzuri. Askofu au rais wa kigingi anaweza kutoa ushauri na tahadhari kuhusu vitendo vya baadaye. Baada ya baraza, anaendelea kutoa msaada kama inavyohitajika.

Picha
mume na mke wakiwa wamekaa pamoja

32.11.2

Ushauri Binafsi pamoja na Askofu au Rais wa Kigingi

Katika baadhi ya mabaraza ya uumini, viongozi wanaweza kuamua kwamba muumini hayupo katika msimamo mzuri—lakini vizuizi rasmi vya uumini havihitajiki. Katika hali hizi, baraza linaweza kuamua kwamba mtu anapaswa kupokea ushauri binafsi na marekebisho kutoka kwa askofu au rais wa kigingi. Ushauri huu unaweza kujumuisha vizuizi visivyo rasmi vya uumini kama ilivyoainishwa katika 32.8.3.

Ushauri binafsi na vizuizi visivyo rasmi sio vya hiari pale ambapo baraza limeitishwa kwa ajili ya dhambi zilizoorodheshwa katika 32.6.1.

32.11.3

Vizuizi Rasmi vya Uumini

Katika baadhi ya mabaraza ya uumini, viongozi wanaweza kuamua kwamba ni vyema kuzuia rasmi fursa za uumini wa kanisa wa mtu kwa muda. Vizuizi rasmi vinaweza kufaa kwa zote isipokuwa dhambi nzito au hali nzito, ambazo uumini utaweza kuondolewa (ona 32.11.4).

Wale walio na vizuizi rasmi vya uumini bado ni waumini wa Kanisa. Hata hivyo, fursa zao za uumini wa Kanisa zimezuiliwa kama ifuatavyo:

  • Hawataweza kuingia hekaluni. Hata hivyo, wanaweza kuendelea kuvaa gamenti ya hekaluni kama wamepata endaumenti. Kama muumini ana kibali cha hekaluni, kiongozi anakifuta kwenye LCR.

  • Hawawezi kutumia ukuhani.

  • Hawawezi kupokea sakramenti au kushiriki katika kuwakubali maafisa wa Kanisa.

  • Hawawezi kuhubiri, kutoa somo, au kusali katika mipangilio ya Kanisa. Wala hawawezi kuhudumu katika wito wa Kanisa.

Wanahimizwa kuhudhuria mikutano ya Kanisa na shughuli kama tabia zao ni nzuri. Pia wanahimizwa kulipa zaka na matoleo.

Askofu au rais wa kigingi anaweza kuongeza masharti mengine, kama vile kukaa mbali na zana za ponografia na vishawishi vingine viovu. Mara zote anaongeza masharti chanya. Haya yanaweza kujumuisha uhudhuriaji Kanisani kila mara, sala za kila mara, na kusoma maandiko na nyenzo zingine za Kanisa.

Kama fursa za mtu za uumini wa Kanisa zimezuiliwa rasmi, hiyo inaandikwa kwenye kumbukumbu ya uumini.

Muda wa zuio rasmi kwa kawaida ni angalau mwaka mmoja na unaweza kuwa zaidi ya hapo. Wakati muumini anapoonesha maendeleo kwenye toba ya kweli, askofu au rais wa kigingi anaitisha baraza lingine kuzingatia kuondoa vizuizi (ona 32.16.1). Kama muumini anaendelea katika tabia ya dhambi, kiongozi anaweza kuitisha baraza lingine kuzingatia hatua zingine.

32.11.4

Uondoaji wa Uumini

Katika baadhi ya mabaraza ya uumini, viongozi wanaweza kuamua kwamba ni vyema kuondoa uumini wa Kanisa wa mtu kwa muda (ona Mosia 26:36; Alma 6:3; Moroni 6:7; Mafundisho na Maagano 20:83).

Kuondoa uumini wa Kanisa wa mtu kunatakiwa kwa mauaji (kama ilivyofafanuliwa katika 32.6.1.1) na` ndoa ya mitala (kama ilivyoelezwa katika 32.6.1.2). Mara zote kunahitajika kwenye kujamiiana kwa maharimu kama iliyoelezwa katika 32.6.1.2 na 38.6.10.

Kama inavyoongozwa na Roho, kuondoa uumini wa mtu kunaweza pia kuwa lazima kama ifuatavyo:

  • Kwa wale ambao tabia zao zinawafanya kuwa tishio kubwa kwa wengine.

  • Kwa wale waliofanya hasa dhambi zenye athari nzito.

  • Kwa wale ambao hawaoneshi toba ya dhambi nzito (ona mazingatio katika 32.7).

  • Kwa wale wanaofanya dhambi nzito ambazo zina madhara kwa Kanisa.

Baraza la uumini la kata, tawi au wilaya linaweza kupendekeza kuondoa uumini wa Kanisa kutoka kwa mtu ambaye hajapokea endaumenti ya hekaluni. Hata hivyo, kibali cha rais wa kigingi au misheni ni lazima kabla ya uamuzi wa mwisho.

Wale ambao uumini wao wa Kanisa umeondolewa hawawezi kufurahia fursa yoyote ya uumini.

  • Hawataweza kuingia hekaluni au kuvaa gamenti ya hekaluni. Kama mtu ana kibali cha hekaluni, kiongozi anakifuta kwenye LCR.

  • Hawawezi kutumia ukuhani.

  • Hawawezi kupokea sakramenti au kushiriki katika kuwakubali maafisa wa Kanisa.

  • Hawawezi kuhubiri, kutoa somo, au sala katika mipangilio ya Kanisa au kuongoza shughuli katika Kanisa. Wala hawawezi kuhudumu katika wito wa Kanisa.

  • Hawawezi kulipa zaka na matoleo.

Wanahimizwa kuhudhuria mikutano ya Kanisa na shughuli kama tabia zao ni nzuri.

Wale ambao uumini wao wa Kanisa umeondolewa wanaweza kufikiriwa kurudishwa tena kwa kubatizwa na kuthibitishwa. Kwa kawaida, wanahitaji kwanza kuonesha toba ya kweli kwa angalau mwaka mmoja. Askofu au rais wa kigingi anaitisha baraza lingine la uumini kuzingatia kuingizwa tena (ona 32.16.1).

Maamuzi ya Baraza la Uumini na Matokeo

Uamuzi

Matokeo

Uamuzi

Anabaki katika Msimamo Mzuri (ona 32.11.1)

Matokeo

  • Hakuna

Uamuzi

Ushauri Binafsi pamoja na Askofu au Rais wa Kigingi (Ona 32. 11.2)

Matokeo

  • Kunaweza kuwa na baadhi ya fursa za uumini zimezuiliwa bila kuwa rasmi.

  • Vizuizi kwa kawaida ni chini ya mwaka mmoja; katika hali isiyo ya kawaida, vinaweza kuwa vya muda mrefu.

  • Vizuizi visivyo rasmi vinaondolewa baada toba ya kweli.

  • Kitendo hakirekodiwi kwenye kumbukumbu ya uumini.

Uamuzi

Vizuizi Rasmi vya Uumini (ona 32.11.3)

Matokeo

  • Fursa za uumini zinazuiliwa rasmi.

  • Vizuizi kwa kawaida ni angalau mwaka mmoja na vinaweza kuwa vya muda mrefu.

  • Kitendo kinarekodiwa kwenye kumbukumbu ya uumini.

  • Vizuizi rasmi vinaondolewa baada ya toba ya kweli, baraza la uumini, na kama ni lazima, kibali cha Urais wa Kwanza.

  • Kiashiria cha kumbukumbu ya uumini kinaondolewa kama vizuizi vimeondolewa baada ya baraza la uumini (isipokuwa ufafanuzi unatakiwa; ona 32.14.5).

Uamuzi

Uondoaji wa Uumini (ona 32.11.4)

Matokeo

  • Ibada zote zinatenguliwa.

  • Fursa zote za uumini zinaondolewa, kwa kawaida, kwa angalau mwaka mmoja.

  • Mtu anastahili kurudishwa kwa kubatizwa na kuthibitishwa tu baada ya toba ya kweli, baraza la uumini, na kama ni lazima, kibali cha Urais wa Kwanza.

  • Mtu aliyepata endaumenti hapo zamani anakuwa mwenye kustahili kupokea urejesho wa baraka kwa kibali cha Urais wa Kwanza pekee na baada ya angalau mwaka mmoja mzima tangu kurudishwa (ona 32.17.2).

  • Kwa mtu aliyepata endaumenti hapo awali, “Urejesho wa Baraka Unahitajika” kiashirio kinaondolewa kutoka kumbukumbu ya uumini baada tu ya ibada kufanyika (ufafamuzi uliohitajika unabaki; ona 32.14.5).

32.11.5

Maswali kuhusu Kuamua Mambo Magumu

Maaskofu wanaelekeza maswali kuhusu miongozo ya kitabu cha maelezo kwa ajili ya mabaraza ya uumini kwa rais wa kigingi.

Kuhusu mambo magumu, rais wa kigingi anaweza kuomba ushauri kutoka Sabini wa Eneo lake. Rais wa kigingi lazima ashauriane na Urais wa Eneo juu ya mambo yaliyoainishwa katika 32.6.3. Hata hivyo, rais wa kigingi hapaswi kumuuliza Sabini wa Eneo au Kiongozi Mkuu Mwenye Mamlaka jinsi ya kuamua mambo magumu. Rais wa kigingi anaamua kama baraza linapaswa kuitishwa kuzungumzia tabia. Kama baraza linakutana, rais wa kigingi au askofu anaamua matokeo.

32.11.6

Mamlaka ya Urais wa Kwanza

Urais wa Kwanza una mamlaka ya mwisho juu ya vizuizi vyote vya uumini wa Kanisa na uondoaji.

32.12

Taarifa na Matangazo

Maamuzi ya baraza la uumini yanawasilishwa kwa mtu—na kwa wengine kama ni lazima—kama ilivyoelezwa hapo chini.

32.12.1

Kumtaarifu Mtu juu ya Uamuzi

Askofu au rais wa kigingi kwa kawaida anamwambia mtu matokeo ya baraza wakati linapomalizika. Hata hivyo, anaweza kuahirisha baraza kwa muda kutafuta mwongozo zaidi au taarifa kabla ya kufanya maamuzi.

Baraza la uumini la kata, tawi au wilaya linaweza kupendekeza kuondoa uumini wa Kanisa kutoka kwa mtu ambaye hajapokea endaumenti ya hekaluni. Hata hivyo, kibali cha rais wa kigingi au misheni ni lazima kabla ya uamuzi wa mwisho.

Askofu au rais wa kigingi anaelezea athari za maamuzi kama yalivyoainishwa katika 32.11. Kwa kawaida pia anatoa ushauri juu ya masharti ya toba ili vizuizi viweze kuondolewa au mtu aweze kurudishwa Kanisani.

Askofu au rais wa kigingi papo hapo anampa mtu notisi ya maandishi ya uamuzi na athari zake. Notisi hii ina malelezo ya jumla kwamba kitendo kilifanyika kama mjibizo wa tabia iliyo kinyume na sheria na taratibu za Kanisa. Inaweza pia kujumuisha ushauri kuhusu kutolewa kwa vizuizi vya uumini au kurudishwa Kanisani. Inapaswa kumtaarifu mtu kwamba anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi (ona 32.13).

Kama mtu haudhurii baraza, notisi ya maandishi inaweza kutosha kumtaarifu juu ya maamuzi. Askofu au rais wa kigingi anaweza pia kukutana na mtu.

Askofu au rais wa kigingi hampi mtu nakala ya fomu ya Ripoti ya Baraza la Uumini la Kanisa.

32.12.2

Kuwajulisha Wengine kuhusu Uamuzi

Kama askofu au rais wa kigingi anatoa vizuizi visivyo rasmi vya fursa za uumini wa mtu katika ushauri binafsi, kwa kawaida hamtaarifu yoyote yule (ona 32.8.3). Hata hivyo, viongozi hawa wanawasiliana wao kwa wao kuhusu vizuizi visivyo rasmi pale wanapowasaidia waumini.

Kama fursa za uumini za mtu zimezuiliwa isivyo rasmi au zimeondolewa katika baraza la uumini, askofu au rais wa kigingi anawasilisha maamuzi kwa wale tu wanaohitaji kujua. Miongozo ifuatayo inatumika.

  • Anazingatia mahitaji ya wahanga na wanaoweza kuwa wahanga na hisia za familia ya mtu.

  • Hazungumzii uamuzi kama mtu anaukatia rufaa. Hata hivyo, anaweza kuzungumzia kwamba unakatiwa rufaa kama anahisi ni lazima kuwalinda wanaoweza kuwa wahanga. Anaweza pia kuuzungumzia ili kusaidia uponyaji wa mhanga (japokuwa hataji jina la mhanga) au kulinda uadilifu wa Kanisa.

  • Kama itahitajika, askofu anazungumzia uamuzi kwa imani kwa washiriki wa baraza la kata. Hii ni kuwafahamisha viongozi ambao wanaweza kufikiria kwamba mtu yule anaweza kupatikana kwa ajili ya wito, kufundisha masomo, au kutoa sala au mahubiri. Pia ni kuwatia moyo viongozi kutoa uangalizi na msaada kwa muumini na familia yake.

  • Kwa kibali kutoka kwa rais wa kigingi, askofu anaweza kuzungumzia uamuzi kwenye mikutano ya akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi wa kata yake ikiwa hali inahusisha:

    • Tabia hatarishi ambayo inaweza kutishia wengine.

    • Kufundisha mafundisho ya uongo au aina zingine za ukengeufu.

    • Dhambi za dhahiri kama vile kutekeleza ndoa za mitala au kutumia mafundisho ya madhehebu kuvutia ufuasi.

    • Kupinga hadharani matendo au mafundisho ya viongozi wakuu au wa maeneo husika wa Kanisa.

  • Katika hali kama hizo, rais wa kigingi anaweza pia kuhitaji kuruhusu mawasiliano kwa waumini wa kata zingine katika kigingi.

  • Katika baadhi ya hali, askofu au rais wa kigingi anaweza kuhisi itaweza kuwa msaada kuwafahamisha baadhi au wahanga wote na familia zao kwamba baraza la uumini limeitishwa kwa ajili ya mtu yule. Anafanya hivi kupitia askofu wao au rais wa kigingi.

  • Kama miendendo hatarishi ya mtu inawaweka wengine kwenye hatari, askofu au rais wa kigingi anaweza kutoa maonyo ili kusaidia kuwalinda wengine. Hatoi taarifa za siri na hafanyi ufafanuzi.

  • Katika hali zingine zote, askofu au rais wa kigingi anaweka ukomo kwenye mawasiliano yoyote kwa kutoa maelezo ya jumla. Kwa ufupi anasema kwamba fursa za mtu za uumini wa Kanisa zimezuiliwa au zimeondolewa kwa sababu ya tabia ambayo ni kinyume na sheria na utaratibu wa Kanisa. Anawaomba wale waliopo kutokuijadili. Hawaombi kura ya kukubali.

  • Kama muumini yupo kwenye msimamo mzuri baada ya baraza la uumini (ona 32.11.1), askofu au rais wa kigingi anaweza kuzungumzia hilo ili kuondoa uvumi.

32.12.3

Kuzungumzia Kujiuzulu kwa Uumini

Katika baadhi ya hali, askofu anaweza kuhitaji kuzungumza kwamba mtu amejiuzulu uumini wake katika Kanisa (ona 32.14.9). Askofu hatoi maelezo mengine yoyote.

32.13

Kukata Rufaa Kwenye Uamuzi

Muumini anaweza kukata rufaa ya uamuzi wa baraza la uumini la kata kwa rais wa kigingi ndani ya siku 30. Rais wa kigingi anaitisha baraza la uumini la kigingi ili kuzingatia rufaa. Anaweza pia kumwomba askofu kuitisha tena baraza na kuzingatia upya uamuzi, hasa kama kuna taarifa mpya.

Muumini anaweza kukata rufaa ya uamuzi wa baraza la uumini la kata kwa kuandika barua kwa Urais wa Kwanza ndani ya siku 30. Muumini anatoa barua kwa rais wa kigingi ili aipeleke kwa Urais wa Kwanza.

Katika misheni, muumini anaweza kukata rufaa ya uamuzi wa baraza la uumini la tawi au wilaya kwa rais wa misheni ndani ya siku 30. Rais wa misheni anaitisha baraza la uumini kuzingatia rufaa. Kama muda au umbali unamzuia kufanya hili, anafuata maelekezo katika 32.9.4.

Kama rais wa misheni aliongoza baraza, muumini anaweza kukata rufaa ya uamuzi kwa kuandika barua kwa Urais wa Kwanza ndani ya siku 30. Muumini anatoa barua kwa rais wa misheni ili aipeleke kwa Urais wa Kwanza.

Mtu anayekata rufaa ya uamuzi anaeleza bayana kwa maandishi madai ya makosa au kukosekana kwa haki katika taratibu au uamuzi.

Kama baraza la uumini linaitishwa kuzingatia rufaa, moja ya maamuzi mawili yanawezekana:

  • Wacha uamuzi wa kwanza usimame.

  • Rekebisha uamuzi wa kwanza.

Maamuzi ya Urais wa Kwanza ni ya mwisho na hayawezi kukatiwa rufaa tena.

32.14

Ripoti na Kumbukumbu za Uumini

32.14.1

Ripoti za Baraza la Uumini la Kanisa

Baada ya baraza lolote la uumini, askofu au rais wa kigingi mara moja anapeleka fomu ya Ripoti ya Baraza la Uumini wa Kanisa kupitia LCR. Anaweza kumwomba karani kutayarisha ripoti. Anahakikisha kwamba hakuna nakala halisi au nakala ya kielektroniki ya fomu inabakizwa mahali pale. Pia anahakikisha kwamba mihutasari yoyote iliyotumika kutayarisha ripoti mara moja inaharibiwa.

32.14.2

Vizuizi Rasmi vya Uumini wa Kanisa

Vizuizi rasmi vya Uumini wa Kanisa vinaandikwa kwenye kumbukumbu za mtu za uumini. Makao makuu ya Kanisa yanatengeneza taarifa hii baada kupokea Ripoti ya Baraza la Uumini la Kanisa. Wakati muumini anapokuwa ametubu, kiongozi lazima aitishe baraza lingine ili kuzingatia kuondoa vizuizi hivi (ona 32.16.1).

32.14.3

Rekodi baada ya Uumini wa Kanisa wa mtu Kuondolewa

Kama uumini wa Kanisa wa mtu umeondolewa, makao makuu ya Kanisa yanaondoa kumbukumbu ya uumini baada ya kupokea Taarifa ya Baraza la Uumini la Kanisa. Kama mtu anatamani, viongozi wanamsaidia kujitayarisha kurudishwa Kanisani kupitia ubatizo na uthibitisho (ona 32.16.1).

32.14.4

Kumbukumbu baada ya Kurudishwa Kanisani

Baada ya mtu kurudishwa Kanisa, askofu anapeleka fomu ya Ripoti ya Baraza la Uumini la Kanisa. Cheti cha Ubatizo na Uthibitisho hakitengenezwi. Bali, ubatizo na uthibitisho vinarekodiwa kwenye fomu ya Ripoti ya Baraza la Uumini la Kanisa.

Kama muumini hakupokea endaumenti, makao makuu ya Kanisa yanatoa kumbukumbu ya uumini ambayo inaonesha tarehe ya ubatizo wake wa kwanza na ibada zingine. Rekodi haifanyi marejeleo kwa upotevu wa uumini wa Kanisa.

Kama muumini alipokea endaumenti, makao makuu ya Kanisa yanasasisha kumbukumbu ya uumini kuonesha tarehe mpya ya ubatizo na uthibitisho Rekodi hii pia inajumuisha ujumbe “Urejesho wa Baraka Unahitajika.” Baada ya baraka za muumini kurejeshwa (ona 32.17.2), kumbukumbu ya uumini inasasishwa kuonesha tarehe za ubatizo wa kwanza na ibada zingine. Haifanyi marejeleo kwa upotevu wa uumini wa Kanisa.

32.14.5

Kumbukumbu za Uumini zenye Ufafanuzi

Kama ilivyoruhusiwa na Urais wa Kwanza, makao makuu ya Kanisa yanafafanua kumbukumbu za uumini za mtu katika hali yoyote iliyoorodheshwa hapo chini.

  1. Askofu au rais wa kigingi anawasilisha Ripoti ya fomu ya Baraza la Uumini la Kanisa ikionesha kwamba uumini wa mtu ulikuwa umezuiliwa rasmi au kuondolewa kwa sababu ya mwenendo ufuatao:

    1. Kujamiiana kwa maharimu (kujamiiana kwa ndugu wa karibu)

    2. Unyanyasaji wa kijinsia wa mtoto au kijana, udhalimu wa kijinsia wa mtoto au kijana, au unyanyasaji mkubwa wa kimwili au kihisia wa mtoto au kijana.

    3. Kujihusisha na ponografia ya mtoto kama ilivyoainishwa katika 38.6.6

    4. Ndoa ya mitala

    5. Tabia ya Unyanyasaji wa kutumia nguvu kijinsia kwa watu wazima.

    6. Ubadilishaji wa jinsia—vitendo vya maabadiliko kwenda kinyume cha jinsia ya kibaolojia ya mtu wakati wa kuzaliwa. (ona 38.6.23)

    7. Ubadhirifu wa fedha za Kanisa au kuiba mali za Kanisa

    8. Matumizi mabaya ya ustawi wa Kanisa

    9. Tabia za kutisha (kama vile kijinsia, kinguvu, au kifedha) au tabia ambazo zina madhara kwa Kanisa

  2. Askofu au rais wa kigingi anapeleka taarifa ya maandishi kwamba mtu yule:

    1. Amekubali au ametiwa hatiana kwa kosa linalohusu moja ya matendo yaliyoorodheshwa hapo juu.

    2. Amekutwa anastahili kuwajibishwa kisheria katika kitendo cha madai ya udanganyifu au vitendo vingine vya kuvunja sheria vinavyohusisha moja ya matendo yaliyoorodheshwa hapo juu.

Wakati askofu anapopokea kumbukumbu ya uumini iliyofafanuliwa, anafuata maelekezo katika ufafanuzi.

Ni Urais wa Kwanza pekee unaoweza kuruhusu kuondoa ufafanuzi kutoka kwenye kumbukumbu ya uumini. Ili kupendekeza kuondoa ufafanuzi, rais wa kigingi: anatumia LCR. Ofisi ya Urais wa Kwanza inamjulisha kama pendekezo limekubaliwa ama la.

32.14.6

Kutoa Taarifa ya Wizi wa Fedha za Kanisa

Kama uumini wa mtu umezuiliwa au umeondolewa kwa sababu za ubadhirifu wa fedha za Kanisa, askofu au rais wa kigingi anautolea taarifa kama ilivyoainishwa katika 34.9.5.

32.14.7

Hamisha Vizuizi kwenye Kumbukumbu za Uumini

Wakati mwingine muumini wa Kanisa anahama wakati kitendo cha uumini au masuala mengine mazito yakisubiri uamuzi. Wakati mwingine askofu anahitaji kushiriki taarifa na askofu mpya kabla ya kuhamisha kumbukumbu ya uumini kwenda kitengo kipya. Katika maswala haya, askofu (au karani kama ameruhusiwa) anaweza kuweka kizuizi cha kuhamisha kwenye kumbukumbu ya uumini. Kumbukumbu zinabaki katika kitengo mpaka askofu (au karani kama ameruhusiwa) anapoondoa kizuizi. Hii inatoa fursa kwa ajili ya askofu kuzungumzia wasiwasi na taarifa.

32.14.8

Taarifa za Wale Ambao Wamefungwa Jela

Baadhi ya waumini wametiwa hatiani kwa makosa ya jinai na wamefungwa jela. Askofu au rais wa kigingi wa kitengo ambapo mtu aliishi wakati kosa lilipofanyika anaendelea na kitendo chochote cha muhimu kwa ajili ya vizuizi rasmi vya uumini au kuondoa. Kama fursa za uumini zilikuwa zimezuiliwa, kiongozi (au karani kama ameruhusiwa) anapeleka kumbukumbu ya uumini kwenye kitengo ambacho kinahusika na mahali ambapo mtu amefungwa jela. Kama uumini ulikuwa umeondolewa, askofu au rais wa kigingi anawasiliana na kuongozi wa kitengo kile. (Ona 32.15.)

32.14.9

Maombi ya Kujiuzulu Uumini

Kama muumini anaomba kujiuzulu uumini wake katika Kanisa, askofu anamfikia kuona kama yupo tayari kujadili dukuduku na kujaribu kuzitatua. Askofu pamoja na muumini wanaweza pia kushauriana na rais wa kigingi. Kiongozi anahakikisha kwamba muumini anaelewa matokeo yafuatayo ya kujiuzulu uumini wa Kanisa:

  • Kunabatilisha ibada zote.

  • Kunaondoa haki zote za uumini.

  • Kurudishwa kwa ubatizo na kuthibitishwa kunaweza kutokea tu baada ya usaili wa kina na katika hali nyingi, baada ya baraza la uumini (ona 32.16.2).

  • Mtu aliyepokea endaumenti hapo kabla anastahili kupokea urejesho wa ukuhani na baraka za hekaluni kwa idhini ya Urais wa Kwanza pekee na baada ya angalau mwaka mmoja tangu kurejeshwa tena (ona 32.17.2).

Kama muumini bado anataka kujiuzulu uumini wa Kanisa, anampa askofu maombi ya kujiuzulu yaliyo katika maandishi na yaliyosainiwa. Askofu anapeleka maombi kwa rais wa kigingi kupitia LCR. Rais wa kigingi kisha anapitia upya na kuwasilisha maombi kupitia mfumo huo. Viongozi wanapaswa kufanyia kazi maombi kwa haraka.

Mtu pia anaweza kujiuzulu uumini kwa kupeleka maombi yaliyothibitishwa na kusainiwa kwenye makao makuu ya Kanisa.

Mtoto mdogo chini ya kiaka 18 anayetaka kujiuzulu uumini wake wa Kanisa anafuata taratibu zilezile kama mtu mzima, isipokuwa kwa jambo moja: ombi linapaswa kusainiwa na mtoto mwenyewe (kama umri wake ni zaidi ya miaka 8) na kusainiwa na mzazi au wazazi au mlezi au walezi ambao wana wajibu kisheria kwa mtoto huyo.

Kama muumini anayejiuzulu uumini anatishia kitendo cha kisheria dhidi ya Kanisa au viongozi wake, rais wa kigingi anafuata maelekezo katika 38.8.24.

Ombi la kujiuzulu uumini linapaswa kushughulikiwa hata kama viongozi wa ukuhani wana taarifa kuhusu dhambi nzito. Taarifa yoyote kuhusu dhambi ambazo hazikutatuliwa inaandikwa wakati ombi linapokuwa limepelekwa kupitia Leader and Clerk Resources. Hii inawaruhusu viongozi wa ukuhani kutatua masuala kama hayo hapo baadae kama mtu anaomba kurudishwa tena ndani ya Kanisa (ona 32.16.2).

Kiongozi wa ukuhani hapaswi kupendekeza kujiuzulu uumini wa Kanisa ili kuepuka kuitisha baraza la uumini.

Viongozi wanaendelea kuwahudumia wale wanaojiuzulu uumini wao isipokuwa pale wanapoomba kutokuwa na mawasiliano.


KURUDISHA FURSA ZA UUMINI WA KANISA


Kama fursa za uumini wa Kanisa wa mtu zimezuiliwa au kuondolewa, viongozi wanashirikiana, wanashauriana, na kumsaidia mtu kadiri anavyoruhusu. Sehemu hii inaelezea jinsi fursa hizo zinavyoweza kurejeshwa.

32.15

Endelea Kuhudumia

Wajibu wa askofu au rais wa kigingi kama mwamuzi wa wote haukomi wakati muumini anapokuwa amepokea vizuizi vya uumini au uumini wake wa Kanisa kuondolewa. Anaendelea kuhudumia, kadiri mtu huyo anayoruhusu, ili mtu huyo aweze tena kufurahia baraka za uumini wa Kanisa. Askofu mara kwa mara anakutana na mtu huyo na, wakati inapokuwa yenye msaada au yenye kufaa anakutana na, mke au mume wake. Mwokozi aliwafundisha Wanefi:

“Walakini, hamtamtupa nje ya … mahali penu pa kuabudu, kwani kwa hawa mtaendelea kuwahudumia; kwani hamjui lakini watarudi na kutubu, na kuja kwangu kwa moyo wa lengo moja, na nitawaponya; na ndipo mtakuwa njia ya kuwaletea wokovu” (3 Nefi 18:32).

Mara tu uumini wa mtu unapokuwa umezuiliwa au kuondolewa ni wakati mgumu na wa hisia kali kwa familia yake. Viongozi wanapaswa kuwa wenye hisia kwa mahitaji haya na wawahimize na kuwasaidi wanafamilia.

Askofu anahakikisha kwamba waumini wanaojali wanapangwa kumhudumia mtu ambaye uumini wake wa Kanisa umezuiliwa au kuondolewa, kadiri mtu anavyoruhusu. Wanahudumu pia kwa wanafamilia wengine. Watu binafsi chini ya vizuizi vya uumini wanaweza kunufaika kutokana na kushiriki katika kuweka pamoja majina kwa ajili ya kazi ya hekalu (ona 25.4.3).

Kama mtu anahama kutoka kwenye kata, askofu anamfahamisha askofu mpya na anamuelezea nini bado kinatakiwa kutokea kabla ya vizuizi vya uumini wa Kanisa kuweza kuondolewa. Kama uumini wa mtu uliondolewa kutoka Kanisani au mtu alijiuzulu uumini, askofu anafanya mawasiliano kama haya kama mtu amekubali kusaidiwa na viongozi wa Kanisa.

32.16

Kuondoa Vizuizi Rasmi au Kurudishwa Kanisani

32.16.1

Mabaraza ya Uumini ili Kuondoa Vizuizi Rasmi au Kumrudisha tena Mtu

Wakati fursa za uumini zimezuiwa au kuondolewa katika baraza la uumini, baraza lingine lazima liitishwe ili kuzingatia kuondoa vizuizi au kumrudisha tena mtu Kanisani. Baraza hili linapaswa pia kuwa na kiwango sawa cha mamlaka (au ya juu zaidi) kama baraza la mwanzo. Kwa mfano, kama rais wa kigingi au misheni alisimamia baraza la mwanzo, rais wa kigingi au misheni anasimamia baraza la kuzingatia kuondoa vizuizi au kumrudusha tena mtu.

Askofu au rais wa kigingi wa sasa anaitisha baraza. Kwanza anahakikisha kwamba mtu ametubu na yupo tayari na anastahili kufurahia baraka za uumini wa Kanisa.

Wale ambao uumini wao wa Kanisa ulikuwa umezuiliwa rasmi kwa kawaida wanahitaji kuonesha toba ya kweli kwa angalau mwaka mmoja kabla zingatio halijatolewa kwa ajili ya kuondoa vizuizi. Wale ambao uumini wao wa Kanisa ulikuwa umeondolewa daima wanahitaji kuonesha toba ya kweli kwa angalau mwaka mmoja kabla hawajaweza kufikiriwa kwa ajili ya kurudishwa tena. Kwa muumini ambaye alishikilia nafasi mashuhuri ya Kanisa katika wakati wa dhambi nzito, muda kwa kawaida ni mrefu zaidi (ona 32.6.1.4).

Baraza la kuzingatia kuondoa vizuizi au kumrudisha tena mtu Kanisani linafuata mwongozo uleule kama mabaraza mengine ya uumini. Askofu anahitaji idhini kutoka kwa rais wa kigingi ili kuitisha baraza. Katika misheni, rais wa tawi au vilaya anahitaji idhini kutoka kwa rais wa misheni.

Miongozo ifuatayo inatumika wakati kwa kufanya baraza la uumini kuzingatia kuondoa vizuizi vya uumini wa Kanisa au kumrudisha tena mtu Kanisani. Sio miongozo yote hii inaweza kutumika katika kila suala.

  1. Rejea upya baraza la mwanzo la uumini. Askofu au rais wa kigingi anarejea upya fomu ya Ripoti ya Baraza la Uumini la Kanisa. Anaomba nakala kupitia LCR. Baada ya kupitia fomu, anaweza kuwasiliana na askofu au rais wa kigingi ambapo baraza la kwanza lilifanyika kutafuta ufafanuzi.

  2. Anamfanyia mtu usaili. Askofu au rais wa kigingi anamfanyia mtu usaili wa kina kuona uimara wa imani yake katika Yesu Kristo na kiwango cha toba yake. Pia anaamua kama mtu ametimiza masharti yaliyoainishwa katika tendo la mwanzo.

  3. Anaamua hali ya jinai au tendo la mahakama ya kiraia. Wakati mwingine mtu anakuwa amekiri au ametiwa hatiani kwa jinai. Wakati mwingine mtu anakuwa amekutwa kuwa anawajibika kisheria katika kitendo cha kiraia cha udanganyifu au vitendo vingine haramu. Katika hali hizi, kiongozi kwa kawaida haitishi baraza mpaka mtu anapokuwa amekamilisha masharti yote ya kifungo chochote, utaratibu, au hukumu iliyotolewa na mamlaka za kisheria. Masharti haya yanaweza kujumuisha kifungo jela, matazamio, kuachiwa, na faini, au kurejesha. Upekee unahitaji idhini ya Urais wa Kwanza kabla ya kuitisha baraza la uumini. Upekee huu unaweza kujumuisha mtu aliyekamilisha mahitaji ya kisheria na ameonesha toba ya kweli lakini yupo kwenye matazamio ya maisha yote au ana faini kubwa.

  4. Wasiliana na viongozi wa ukuhani wa wahanga. Askofu au rais wa kigingi anawasiliana na akofu wa sasa au rais wa kigingi wa sasa wa mhanga yoyote (ona 32.10.2).

  5. Anatoa taarifa ya baraza. Anamtaarifu mtu juu ya tarehe, muda, na mahali baraza litakapofanyika.

  6. Anaendesha Baraza. Anaendesha baraza kulingana na miongozo katika 32.10.3. Anamwuliza mtu nini amefanya ili kutubu. Pia anamwuliza kuhusu msimamo wake kwa Yesu Kristo na kwa Kanisa. Wakati masuala yote yanayohusika yanapokuwa yametolewa, anamruhusu muumini kutoka nje. Pamoja na washauri wake, anasali ili kuzingatia ni hatua ipi ya kuchukua. Maamuzi matatu yanayowezekana ni:

    1. Kuendeleza vizuizi vya uumini wa Kanisa au kuondoa uumini

    2. Kuondoa vizuizi au kuruhusu kurejeshwa tena.

    3. Kupendekeza kwa Urais wa Kwanza kwamba vizuizi viondolewe au kurejeshwa kuruhusiwe (kama ni lazima kulingana na “Omba Idhini ya Urais wa Kwanza” hapa chini).

  7. Shiriki Uamuzi. Baada ya baraza kufanya uamuzi, afisa kiongozi anaushiriki na mtu huyo. Kama idhini kutoka Urais wa kwanza ni lazima, anaeleza kwamba uamuzi ni pendelezo kwa urais wa Kwanza.

  8. Anapeleka ripoti. Askofu au rais wa kigingi anawasilisha fomu ya Ripoti ya Baraza la Uumini la Kanisa kupitia LCR. Anaweza kumwomba karani kutayarisha ripoti hii. Anahakikisha kwamba hakuna nakala ya karatasi au nakala ya kielektroniki inabakizwa mahali pale. Pia anahakikisha kwamba mihutasari yoyote iliotumika kutayarisha ripoti inaharibiwa haraka.

  9. Anaomba Idhini ya Urais wa Kwanza (kama ni lazima). Katika hali zifuatazo, idhini ya Urais wa Kwanza ni lazima ili kuondoa vizuizi rasmi au kumrudisha tena mtu Kanisani. Idhini hii inahitajika hata kama tabia ilitokea baada ya uumini wa Kanisa kuzuiliwa rasmi au kuondolewa.

    1. Mauaji

    2. Kujamiiana kwa maharimu (kujamiiana kwa ndugu wa karibu)

    3. Unyanyasaji wa kijinsia wa mtoto au kijana, udhalimu wa kijinsia wa mtoto au kijana, au unyanyasaji mkubwa wa kimwili au unyanyasaji wa kihisia wa mtoto au kijana na mtu mzima au na kijana ambaye ni mkubwa kwa miaka kadhaa

    4. Kujihusisha na ponografia ya mtoto wakati kuna hatia kisheria

    5. Ukengeufu

    6. Ndoa ya mitala

    7. Kufanya dhambi nzito wakati unashikilia nafasi maarufu ya Kanisa

    8. Ubadilishaji wa jinsia—vitendo vya mabadiliko kwenda kinyume cha jinsia ya kibaiolojia ya mtu wakati wa kuzaliwa (ona 38.6.23)

    9. Kufanya ubadhirifu wa fedha za Kanisa au mali za Kanisa.

  10. Toa taarifa ya maandishi ya uamuzi. Askofu au rais wa kigingi anahakikisha kwamba mtu anapokea mara moja notisi ya maandishi ya uamuzi na athari zake.

  11. Batiza na thibitisha. Kama uumini wa Kanisa wa mtu ulikuwa umeondolewa katika baraza la mwanzo, lazima yeye abatizwe na kuthibitishwa tena. Kama idhini ya Urais wa Kwanza ni lazima, ibada hizi zinaweza kufanywa tu baada ya idhini hii kupokelewa. Cheti cha Ubatizo na Uthibitisho hakitengenezwi (ona 32.14.4).

32.16.2

Kurudishwa tena baada ya Kujiuzulu Uumini wa Kanisa

Kama mtu anajiuzulu rasmi uumini wa Kanisa, yeye lazima abatizwe na kuthibitishwa ili aweze kuruhusiwa tena Kanisani. Kwa watu wazima, kurudishwa tena kwa kawaida hakuzingatiwi mpaka angalau baada ya mwaka mmoja baada ya kujiuzulu uumini.

Wakati mtu anapoomba kurudishwa tena, askofu au rais wa kigingi anapata nakala au fomu ya Ripoti ya Tendo la Utawala ambayo inaambatana na lile ombi la kujiuzulu. Anaweza kupata hii kupitia LCR.

Askofu au rais wa kigingi kisha anamfanyia usaili mtu kwa kina. Anauliza kuhusu sababu ya ombi la kwanza na tamanio la kurudishwa tena. Katika roho ya upendo, anauliza kuhusu dhambi nzito ambazo mtu yawezakuwa amezifanya kabla au baada ya kujiuzulu uumini. Kiongozi haendelei na kurudisha tena mpaka pale anapokuwa ameridhika kwamba mtu ametubu na yu tayari na anastahili kufurahia baraka za uumini wa Kanisa.

Miongozo kwa ajili ya kuruhusu tena baada ya kujiuzulu inafuata:

  • Baraza la uumini linaitishwa kama uumini wa mtu ulizuiliwa rasmi wakati wa muda wa kujiuzulu.

  • Baraza la uumini linaitishwa kama mtu alifanya dhambi nzito, ikijumuisha ukengeufu, kabla ya kujiuzulu uumini.

Katika hali zingine, baraza la uumini haliitishwi isipokuwa kama askofu au rais wa kigingi anaamua kwamba litahitajika.

Wakati baraza la uumini ni lazima kwa ajili ya mtu ambaye amepokea endaumenti ya hekaluni, rais wa kingingi analiitisha. Wakati baraza ni la lazima kwa ajili ya mtu ambaye hakupokea endaumenti, askofu analiitisha, kwa kibali kutoka kwa rais wa kigingi.

Kama mtu alijihusisha na tabia yoyote katika 32.16.1, nambari 9, ama kabla au baada ya kujiuzulu uumini wa Kanisa, idhini ya Urais wa Kwanza inahitajika kwa ajili ya kurudishwa tena. Kama mtu alijihusisha na tabia yoyote katika 32.14.5, nambari 1, ama kabla au baada ya kujiuzulu uumini, ufafanuzi utafanywa kwenye kumbukumbu ya uumini.

Mtu anayeomba kurudishwa tena lazima akidhi sifa sawa na zile za wengine waliobatizwa. Wakati askofu au rais wa kigingi anapokuwa ameridhika kwamba mtu anastahili na ni mkweli katika kutaka kurudishwa tena, mtu anaweza kubatizwa na kuthibitishwa. Cheti cha Ubatizo na Uthibitisho hakitengenezwi (ona 32.14.4).

32.17

Shughuli za Kanisa, Utawazo, na Urejesho wa Baraka baada ya Kurudishwa tena.

32.17.1

Shughuli za Kanisa na Utawazo

Chati ifuatayo inaonesha kiwango kinachofaa cha shughuli za Kanisa kwa ajili ya mtu ambaye amerudishwa tena kwa ubatizo na uthibitisho.

Hakupokea Endaumenti Hapo Mwanzo

Alipokea Endaumenti Hapo Mwanzo

Walishikilia Ukuhani Hapo Mwanzo

Hakupokea Endaumenti Hapo Mwanzo

  • Mara tu baada ya ubatizo na uthibitisho, ukuhani unaweza kutunukiwa kwao na kutawazwa kwenye ofisi ya ukuhani waliokuwa nao wakati uumini wao wa Kanisa ulipoondolewa au kujiuzulu. Kura ya kukubali haihitajiki.

  • Wanaweza kupewa kibali cha hekaluni chenye matumizi yenye ukomo.

Alipokea Endaumenti Hapo Mwanzo

  • Wanaweza wasitawazwe kwenye ofisi yoyote ya ukuhani. Wakati ukuhani wao na baraka za hekaluni zinapokuwa zimerejeshwa, ofisi yao ya zamani ya ukuhani itarejeshwa kama ilivyoainishwa katika 32.17.2. Hawawezi kufanya ibada mpaka muda huo.

  • Wanaweza kushiriki katika shughuli yoyote ya Kanisa ambayo inaruhusiwa kwa muumini ambaye hajapokea endaumenti ambaye hana ukuhani.

  • Hawawezi kuvaa gamenti ya hekaluni au kupokea aina yoyote ya kibali cha hekaluni mpaka baraka zao zirejeshwe.

Waumini wengine

Hakupokea Endaumenti Hapo Mwanzo

  • Wanaweza kushiriki katika shughuli za Kanisa kama waongofu wapya wanavyofanya.

  • Wanaweza kupewa kibali cha hekaluni chenye matumizi yenye ukomo.

Alipokea Endaumenti Hapo Mwanzo

  • Wanaweza kushiriki katika shughuli yoyote ya Kanisa ambayo inaruhusiwa kwa muumini ambaye hajapokea endaumenti ambaye hana ukuhani.

  • Hawawezi kuvaa gamenti ya hekaluni au kupokea aina yoyote ya kibali cha hekaluni mpaka baraka zao zirejeshwe (ona 32.17.2).

32.17.2

Urejesho wa Baraka

Watu waliopokea endaumenti ya hekaluni hapo mwanzo na walirudishwa tena kwa ubatizo na uthibitisho wanaweza kupokea ukuhani wao na baraka za hekaluni kupitia ibada ya urejesho wa baraka pekee (ona Mafundisho na Maagano 109:21). Hawatawazwi tena kwenye ofisi ya ukuhani au kupokea tena endaumenti. Baraka hizi zinarejeshwa kupitia ibada. Akina kaka wanarejeshwa kwenye ukuhani wao wa zamani, isipokuwa kwa ofisi ya Sabini, askofu, au patriaki.

Urais wa Kwanza pekee unaweza kuidhinisha utoaji wa ibada ya urejesho wa baraka. Hawatashughulikia maombi kwa ajili ya ibada hii mapema zaidi ya mwaka mmoja baada ya mtu kurudishwa tena kwa ubatizo na uthibitisho. Askofu au rais wa kigingi anaomba urejesho wa baraka kupitia LCR.

Kama Urais wa Kwanza unaidhinisha urejesho wa baraka, wanampangia Kiongozi Mkuu mwenye Mamlaka au rais wa kigingi kumfanyia usaili mtu huyo. Kama mtu huyo anastahili, kiongozi huyu anafanya ibada ili kurejesha baraka za mtu huyo.

Kwa maelezo kuhusu kumbukumbu ya uumini na urejesho wa baraka, ona 32.14.4.

Picha
mwanamume akishiriki sakramenti