Sura ya 55
Ufunuo kuhusu Ndoa
Julai 1843
Joseph Smith alimwuliza Bwana baadhi ya maswali kuhusu ndoa. Yesu alimwambia kwamba mwanamume na mwanamke wanapaswa kufungishwa ndoa na mtu ambaye ana ukuhani. Wanapaswa kufunga ndoa hekaluni. Kama watatii amri za Mungu, watakuwa wamefunga ndoa milele.
Watu waadilifu waliofunga ndoa hekaluni wataishi katika ufalme wa selestia wa mbinguni. Watoto wao wanaomtii Mungu watakuwa wao, na watakuwa familia ya milele. Wataishi na Mungu na kuwa kama Yeye.
Yesu pia alimwambia Joseph kuhusu historia ya ndoa miongoni mwa watu Wake walioishi hapo zamani.