Masasisho Kwenye Kozi (2024)
Masasisho ya Kozi
Kutangaza Nyenzo Zilizosasishwa za EnglishConnect
Masasisho ya kidijitali kwenye nyenzo za EnglishConnect sasa yanapatikana kwa Kiingereza kwenye app ya Maktaba ya Injili na kwenye ChurchofJesusChrist.org. Masasisho yanaakisi maboresho ili kuwasaidia wanafunzi, walimu na viongozi. Mifano inajumuisha nyenzo kwa ajili ya mazoezi ya kila siku, usaidizi wa tafsiri na kanuni za kujifunza kwa kusoma na kwa imani. Jifunze zaidi kwenye englishconnect.org/updates.
Masasisho haya yanatafsiriwa katika lugha zaidi ya 40 za nyongeza. Viongozi wa maeneo husika watafahamishwa wakati nyenzo zilizopitiwa upya za kielekroniki na zilizochapishwa zitapatikana kwa lugha yao. Waumini na wamisionari wanapaswa kuendelea kutumia matoleo ya nyenzo zilizopo kwa sasa za EnglishConnect mpaka pale matoleo yaliyosasishwa yatakapopatikana.
Pekua nyenzo mpya za EnglishConnect kwenye Maktaba ya Injili:
Matumizi ya kidijitali ya nyenzo ya wanafunzi ya EnglishConnect yanapendekezwa na unaweza kuweka oda ya nakala iliyochapishwa pale itakapokuwa inapatikana katika duka la usambazaji la mtandaoni kupitia store.ChurchofJesusChrist.org (Gospel Study > Manuals and Guides > EnglishConnect).
Walimu wanahimizwa kupitia Teacher Training Videos wakati wanapojiandaa kuongoza mazungumzo ya makundi kwa kutumia nyenzo zilizosasishwa.
Badilisha Nyenzo Hizi za Awali za EnglishConnect
Matoeleo ya awali ya nyenzo za EnglishConnect sasa yamesitishwa. Ingawa nyenzo hizi hazitumiki tena, bado unaweza kuzinunua wakati bado zikiwa zinapatikana kwenye duka la usambazaji la mtandaoni au mpaka pale nakala zilizosasishwa zitakapokuwa zikipatikana kwa ajili ya manunuzi.
Makundi yaliyopo sasa ya EnglishConnect yanaweza kuendelea kutumia matoleo ya awali ya nyenzo za EnglishConnect mpaka watakapomaliza au wanaweza kuanza kutumia matoleo yalisasishwa ya kidijitali mara tu yanapopatikana.