Somo la Mafunzo- Nyumbani
Alma 17–24 (Kitengo cha 17)
Vifaa vya Matayarisho kwa Mwalimu wa Mafunzo -Nyumbani
Muhtasari wa Masomo ya Mafunzo- Nyumbani Kila Siku
Muhtasari ufuatao wa mafundisho na kanuni ambazo wanafunzi walijifunza waliposoma Alma 17–24 (kitengo cha 17) haijanuiwa kufundishwa kama sehemu ya somo lako. Somo unalofundisha huzingatia tu machache ya mafundisho na kanuni hizi. Fuata uvuvio wa Roho Mtakatifu unapofikiria mahitaji ya wanafunzi.
Siku ya 1 (Alma 17–18)
Kutoka kwa mfano wa Amoni, na ndugu zake wakifundisha Walamani, wanafunzi walijifunza kwamba kwa kupekua maandiko, na kuomba, na kufunga, tunaweza kupokea Roho Mtakatifu na kuwafundisha wengine kwa nguvu. Huduma ya Amoni kwa Mfalme Lamoni pia ilifundisha kipengele muhimu cha huduma ya umisionari —kwamba tunapoweka mifano mizuri, Bwana anaweza kutufanya vyombo katika mikono Yake. Wanafunzi waliweza kuona kwamba huduma ya Amoni kwa Lamoni ilitayarisha mtawala Mlamani na wengine kukubali injili. Uongofu wa mfalme Lamoni unafundisha kwamba wakati tunapoelewa haja yetu ya Mwokozi, tutakuwa na hamu ya kutubu.
Siku ya 2 (Alma 19–20)
Wanafunzi walijifunza kwamba ushuhuda na mfano wa haki wa Amoni ulisaidia kumgeuza baba yake Lamoni kwa Bwana. Walijifunza pia kwamba vitendo vyetu vya upendo vinaweza kusababisha wengine kupunguza makali ya nyoyo zao na kutafuta kujua ukweli.
Siku ya 3 (Alma 21–22)
Masimulizi ya kazi ya Haruni ya umisionari yaliwasaidia wanafunzi kuona kwamba kama kwa uaminifu tutaendelea kupitia kwa majaribio yetu, Bwana atatusaidia kufanya kazi Yake. Haruni alimsaidia baba ya Mfalme Lamoni kuelewa kwamba angeweza kupokea wokovu tu kwa njia ya kustahili ya Yesu Kristo. Kama mfalme, ni lazima tuwe radhi kuacha dhambi zetu zote ili kubadilishwa kiroho kuzaliwa na Mungu.
Siku ya 4 (Alma 23–24)
Maelfu ya Walamani waliokubali injili walionyesha kwamba uongofu ni mabadiliko ya kiroho, —kuwa mtu mpya kwa njia ya nguvu ya Mungu. Kupitia kwa mfano wa Walamani ambao walikuwa Anti-nefi-Lehi, wanafunzi walijifunza kwamba kama tukifanya yote tunayoweza kutubu, Mungu ataondoa hatia yetu na kutusaidia kubaki wasafi. Uongofu wa Walamani unaonyesha kwamba tunaweza kusaidia wengine kuwa waongofu wakati tukiwa waaminifu.
Utangulizi
Wana wanne wa Mfalme Mosia walichagua kukataa fursa na anasa nyumbani ili waweze kuhubiri injili miongoni mwa Walamani. Masimulizi ya wamisionari hawa wanne yanaonyesha jinsi wanafunzi wanaweza kujiandaa kwa ufanisi katika kufundisha injili ya Yesu Kristo kwa wengine.
Mapendekezo ya Kufundisha
Alma 17–22
Amoni na nduguze wawili wanawafundisha wafalme wawili wa Walamani
Mbele ya darasa, andika kauli ifuatayo isiyokamilika ubaoni au kwenye kipande cha karatasi: Jambo moja muhimu unaloweza kufanya ili kujiandaa kwa ajili ya wito kuhudumu [misheni] ni ku….
Alika wanafunzi wachache waeleze jinsi ilivyokuwa walipomwona mwanafamilia au rafiki akirudi kutoka kuhudumu kwa uaminifu misheni ya muda kamili. Kisha waulize wanafunzi: Jinsi gani mtu huyo alikuwa tofauti baada ya misheni wake? Unafikiri nini kilisababisha mabadiliko haya?
Waulize wanafunzi ni kwa jinsi gani wanaweza kukamilisha taarifa iliyopo ubaoni. Baada ya wanafunzi kujibu, shiriki nao jinsi Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alivyokamilisha taarifa: “Jambo moja muhimu unaloweza kufanya ili kujiandaa kwa ajili ya wito kutumikia [misheni] ni kuwa mmisionari muda mrefu kabla ya kwenda misheni” (Becoming a Missionary, Ensign or Liahona, Nov. 2005, 45).
Uliza: Ni katika njia gani wavulana na waischana wanafuata ushauri wa Mzee Bednar na kuwa wamisionari kabla ya wao kutumikia misheni za muda kamili?
Shiriki kauli ifuatayo ya Rais Thomas S. Monson:
“Huduma ya umisionari ni jukumu la ukuhani—, sharti ambalo Bwana anatarajia kutoka kwetu sisi ambao tumepewa mengi sana. Wavulana, nawasihi mjitayarishe kwa huduma kama mmisionari. Jiwekeni wasafi na halisi na wastahiki kumwakilisha Bwana. Dumisha afya na nguvu zako” Soma maandiko. Pale ambapo inapatikana, shiriki katika seminari na chuo. Jizoeshe na kitabu cha maelekezo cha misionari Hubiri Injili Yangu.
Neno kwenu kina dada vijana: “Ingawa hamna majukumu ya ukuhani sawa na waliyonayo wavulana kuhudumu kama wamisionari wa muda kamili pia mnatoa mchango muhimu kama wamisionari, na tunakaribisha huduma yenu.” (As We Meet Together Again, Ensign or Liahona, Nov. 2010, 6).
Andika yafuatayo ubaoni: Bwana atatubariki kwa Roho Mtakatifu na nguvu ya kufundisha neno lake tunapo
Gawa darasa katika vikundi vinne. Pangia kila kundi moja ya vifungu vifuatavyo vya maandiko: Alma 17:1–4; Alma 17:9–13; Alma 17:19–25; 18:1–9; Alma 17:26–30. (Rekebisha shughuli hii kama una darasa ndogo.)
Waalike wanafunzi wasome vifungu walivyopangiwa kimya, wakitafuta kile wana wa Mosia walichofanya ambacho kiliwabariki kwa Roho na kwa nguvu walipokuwa wakifundisha injili. Eleza kwamba wakati wanafunzi wakishakamilisha, waulize washiriki kile walichogundua na jinsi watakavyoweza kukamilisha sentensi ubaoni.
Baada ya muda wa kutosha, alika mtu kutoka kila kundi kueleza kile wana wa Mosia walichofanya na jinsi washiriki wa kundi wangekamilisha kanuni iliyopo ubaoni. Majibu ya wanafunzi yanaweza kujumuisha yafuatayo: kupekua maandiko, kufunga na kuomba, kuwa na subira, kuweka mfano mzuri, uaminifu kwa Bwana, kutumikia wengine kwa dhati, na kuwapenda wengine kama ndugu na dada zetu. Wanafunzi wanaposhiriki majibu yao, yaorodheshe ubaoni. Waulize wanafunzi waeleze jinsi kila kitendo au tabia inavyoweza kusaidia mtu binafsi kushiriki injili kwa ufanisi zaidi.
Kama wowote wa mwanafunzi wako wangeongolewa katika injili baada ya kufundishwa na wamisionari wa muda wote, unaweza ukawataka washiriki jinsi walivyojisikia walipokuwa wakijifunza injili.
Wakumbushe wanafunzi kwamba baada ya Amoni kulilinda kundi la mifugo ya mfalme, Mfalme Lamoni alishangazwa na nguvu za Amoni na vilevile utii na uaminifu wake katika kutimiza amri za mfalme (ona Alma 18:8–10). Lamoni alikuwa tayari kusikiliza ujumbe wa Amoni ambao alikuwa amekuja kushiriki naye. Waalike wanafunzi kuchukua zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 18:24–29. Uliza darasa litafute jinsi Amoni alivyojengea kwa ufahamu wa Lamoni juu ya Mungu ili aweze kumwandaa Lamoni kuelewa mafundisho ya kweli.
Waulize wanafunzi maswali yafuatayo:
-
Kama ungekuwa na mazungumzo kuhusu Mungu na rafiki wa imani ingine, ungewezaje kutumia imani mnazoshiriki nyote, kama Amoni alivyofanya? Juhudi hii inawezaje kumsaidia rafiki yako?
-
Mada gani nyingine za injili mgezugumza na marafiki zako kufungua fursa ya kushiriki injili pamoja nao?
Wakumbushe wanafunzi kwamba Mfalme Lamoni alikuwa msikivu kwa injili ya Yesu Kristo, kama alivyofanya baba yake. Muulize mwanafunzi mmoja asome kwa sauti Alma 18:39–41— majibu ya Lamon kwa kujifunza kuhusu Yesu Kristo. Muulize mwanafunzi mwingine asome Alma 22:14–18— majibu ya babake Lamoni. Alika darasani lifuatilie katika maandiko yao na litafuta majibu yanayofanana katika watu hawa.
Uliza: Je! Watu wote wawili walitaka kufanya nini wakati walipojifunza kuhusu Yesu Kristo?
Eleza kwamba Lamoni na baba yake waliguswa na Roho kwa njia ya mafundisho ya wamisionari. Kwa hivyo, walitaka baraka za injili na walikuwa radhi kuacha dhambi zao na kutubu. Wakumbushe wanafunzi ukweli waliojifunza juma hili: Ni lazima tuwe radhi kuziacha dhambi zetu zote ili tubadilishwe kiroho na kuzaliwa kwa Mungu.
Mualike mwanafunzi asome kwa sauti taarifa ya Mzee Dallin H. Oaks inayopatikana katika mwongozo wao wa kujifunza: “Injili ya Yesu Kristo inatupa changamoto kubadilika. Tubuni ni ujumbe wa kila mara, na kutubu ina maana ya kuacha matendo yetu yote ya — kibinafsi, familia, kabila, na kitaifa — ambayo ni kinyume na amri za Mungu. Madhumuni ya injili ni kugeuza viumbe vya kawaida na kuwa raia wa selestia, na hiyo inahitaji mabadiliko” (Repentance and Change, Ensign au Liahona, Nov. 2003, 37).
Waalike wanafunzi kufikiria kuhusu maisha yao na kufikiria kama wanahitaji kuacha dhambi yoyote ili kubadilishwa kiroho kama vile Lamoni na baba yake walivyobadilishwa. Hitimisha kwa kushirikiana himizo lako na ushuhuda kwamba tukiwa radhi kuacha dhambi zetu, Bwana atatusaidia kubadilika na kukua.
Kitengo Kinachofuata (Alma 25–32)
Waulize wanafunzi kufikiria swali hili: Ungeweza kusema nini kwa mtu ambaye ni mpinga Kristo? Katika kitengo cha pili, wanafunzi watajifunza jinsi Alma alishughulikia maswali na kejeli ya Korihori, ambaye alikuwa mpinga Kristo. Kwa nyongeza, watajifunza zaidi kuhusu imani kama wanavyosoma kuhusu jinsi Alma na wengine walivyofanya kazi ya kufundisha Wazoramu waliokengeuka, ambao walikuwa kuzipotosha njia za Bwana.