Maktaba
Somo la 100: Alma 43–44


Somo la 100

Alma 43–44

Utangulizi

Wakati Alma na wanawe wakiendelea kuhubiri injili, Wazoramu walijiunga na jeshi la Walamani kuwashambulia Wanefi. Kapteni Moroni alidhihirisha imani na busara katika kuwaongoza Wanefi kujilinda dhidi jeshi la Walamani. Ijapokua walizidiwa kwa idadi, maandalizi ya wanajeshi Wanefi na imani yao katika Yesu Kristo iliwasaidia vitani. Walamani walipoona walikuwa dhahiri wanashindwa, walifanya agano la amani na kuondoka kutoka kwa nchi hiyo kwa kipindi fulani.

Mapendekezo ya Kufundisha

Alma 43

Maandalizi na mikakati ya Kapteni Moroni ilisaidia kushinda mbinu za jeshi la Walamani

Waalike wanafunzi waandike kwenye daftari au shajara za kujifunza maandiko orodha ya mipango, malengo na hamu zao za siku za usoni. Wanapoandika, wakumbushe wafikirie kuhusu malengo na hamu zao za kiroho kama vile kuhudumu misheni, kufungishwa hekaluni na kulea familia. Kabla ya darasa, unaweza kuandika orodha kama hiyo ya malengo na hamu yako mwenyewe ya siku za usoni. Unaweza kushirikisha baadhi ya mipango na hamu zako kama mifano ili kuwasaidia wanafunzi kuanza kuandika.

Baada ya wanafunzi kuandika orodha yao, waalike kutambua hamu na malengo wanahisi Shetani hatataka wao wayatimize. Alika wanafunzi wachache kushiriki malengo waliyoyatambua. Waombe waelezee kwa nini Shetani hatotaka wao wayatimize malengo hayo. Unaweza pia kuwauliza kwa nini wanahisi kwa nguvu kuhusu kutimiza hayo malengo. Pendekeza kuwa somo la Alma 43–44 linaweza kusaidia kuonyesha jinsi tunavyoweza kutimiza malengo yetu maadilifu licha ya juhudi za uharibifu za adui.

Fanya muhtasari wa Alma 43:1–4 kwa kuelezea kuwa licha ya juhudi za Alma kuwarudisha tena Wazoramu katika Kanisa, wengi wao walijiunga na Walamani na kujitayarisha kuwavamia Wanefi. Waliungana pia na Waamaleki, ambao, kama Wazoramu walikuwa kwa wakati mmoja Wanefi lakini walikuwa wamepotoka kutoka kwenye kweli.

Mualike mwanafunzi asome Alma 43:5–8 kwa sauti. Omba darasa lifuatilie likitafuta mipango au “ mbinu” za kiongozi Mlamani, Zerahemna.

Eleze kuwa tunapojifunza masimulizi ya vita vya kimwili katika Kitabu cha Mormoni, tunaweza kufananisha na mapigano ya kiroho tunayokabiliana nayo.

  • Mbinu za Zerahemna dhidi ya Wanefi zinaweza vipi kuwa kama mbinu alizonazo Shetani?

Mualike mwanafunzi asome Alma 43:9–12 kwa sauti. Uliza darasa litambue mbinu za Wanefi.

  • Mbinu za Wanefi zilikuwa ni nini?

Waalike wanafunzi wasome Alma 43:16–19 kimya. Waalike wakitafute kile Moroni, kapteni mkuu wa Wanefi, alikifanya kuwaandaa watu kulinda nchi yao na familia zao.

  • Ni vitu gani halisi ambavyo Wanefi walifanya ili kujiandaa kwa shambulizi la Walamani?

Mualike mwanafunzi asome Alma 43:20–22 kwa sauti, na omba darasa litafute majibu ya Walamani kwa maandalizi ya Wanefi.

  • Kwa nini Walamani waliondoa shambulizi lao ijapokuwa walikuwa wengi kushinda Wanefi?

  • Tunaweza kujifunza nini kutoka tukio hili kuhusu kujilinda sisi wenyewe dhidi ya mbinu za Shetani?

Waalike wanafunzi wasomeAlma 43:23–24 kimya wakitafuta kile Moroni alifanya alipokuwa hana uhakika jinsi adui yake alivyopanga kufanya shambulio lingine.

  • Kwa nini Moroni aliwatuma wajumbe kuzungumza na Alma?

  • Mfano wa Moroni unaweza kutufundisha nini kuhusu jinsi tunavyoweza kujitayarisha kiroho dhidi ya adui? (Wasaidie wanafunzi kutambua kanuni ifuatayo: Kama tukitafuta na kufuata ushauri wa kinabii, tutaweza vizuri zaidi kujilinda dhidi ya adui.)

Kwa ufupi fanya muhtasari wa Alma 43:25–43 kwa kuelezea kwamba Moroni alitumia ufahamu ambao alipata kutoka kwa Nabii. Aliligawa jeshi lake katika sehemu mbili. Baadhi ya wanajeshi walikaa katika mji wa Jershoni na kuwalinda watu wa Amoni. Jeshi lililobakia lilikwenda katika nchi ya Manti. Moroni alituma wapelelezi kutafuta wapi walikuwepo Walamani, na alikuwa na wanajeshi wengine waliojificha katika njia ambayo Walamani wangepitia. Walamani walipokaribia, wanajeshi Wanefi waliwazingira. Walamani walipoona kuwa wamezungukwa, walipigana vikali. Wengi wa Wanefi walikufa, lakini Walamani hata walipata waadhiriwa zaidi.

Waalike baadhi ya wanafunzi wachukue zamu kusoma kwa sauti kutoka Alma 43:43–54. Uliza darasa litafute tofauti kati ya motisha na chanzo cha nguvu za Walamani na motisha na chanzo cha nguvu za Wanefi.

  • Umegundua nini kuhusu sababu za Walamani za kwenda vitani? Umegundua nini kuhusu sababu za Wanefi za kwenda vitani? Chanzo cha nguvu za Wanefi kilitofautiana vipi na kile chanzo cha nguvu za Walamani? Kama inahitajika, sisitiza kwamba wakati Walamani walipigana kwa sababu ya chuki na hasira, Wanefi walivutiwa na sababu bora zaidi [ona Alma 43:45–47]. Walimlilia Bwana kwa msaada, na Yeye aliwaimarisha [ona Alma 43:49–50].)

  • Tunaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa Moroni na jeshi lake cha kutusaidia kupigana dhidi ya adui?

Waalike wanafunzi waandike majibu yao kwa swali hili. Kisha waombe wao washiriki kile walichoandika. Wanaweza kutaja baadhi ya kanuni zifuatazo:

Na tunapoomba msaada katika kutimiza mipango yetu ya haki na haja adilifu, Mungu atatusaidia kuyatimiza.

Tunaongozwa na nia bora kuliko hao wanaoukataa ukweli.

Bwana atatusaidia kutimiza wajibu wetu kulinda familia zetu, uhuru wetu, na dini yetu.

Waalike wanafunzi waelezee kuhusu wakati ambapo walipata msaada wa Bwana katika kutimiza malengo mema. Fikiria kushirikisha uzoefu wako mwenyewe. Shuhudia uwezo wa Bwana wa kutusaidia kutimiza mbinu njema. Waalike wanafunzi waweka malengo mema kama sehemu endelevu ya maombi yao.

Alma 44

Kapteni Moroni anawaamuru Walamani kufanya agano la amani

Mualike mvulana ambaye yupo radhi kusoma kwa sauti aje mbele ya chumba na maandiko yake. Kumbusha darasa kwamba wakati kapteni Moroni alipoona hofu kubwa ya Walamani, aliamrisha watu wake kuacha kupigana (ona Alma 43:54). Acha yule mvulana asome maneno ya Moroni katika Alma 44:1–6. Omba darasa lisikilize maelezo ya Moroni kuhusu ushindi wa Wanefi.

  • Moroni alitaka Zerahemna kuelewa nini kuhusu chanzo cha nguvu za Wanefi kwenye vita? Alitoa nini kwa Walamani? (Alisema kwamba Wanefi wasingewadhuru tena kama wangeweka silaha zao chini na kuingia kwenye agano la amani.)

  • Tunaweza kujifunza ukweli gani kutoka katika Alma 44:4–6 ambacho kinaweza kutusaida kwenye vita vyetu vya kiroho. (Wanafunzi wanaweza kushiriki kanuni kadhaa, baadhi yake tayari zimekwishapitiwa kwenye somo hili. Hakikisha watajumuisha ukweli unaofuata: Bwana atatuimarisha na kutuhifadhi kulingana na imani yetu Kwake. Unaweza ukitaka kupendekeza kwamba wanafunzi waweke alama kwenye maneno katika aya hizi yanayofundisha ukweli huu.)

Mualike mwanafunzi asome kwa sauti ushauri ufuatao kwa vijana wa Kanisa, kutoka kwa Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Unaweza ukitaka kutoa nakala kwa kila mwanafunzi.

Rais Boyd K. Packer

“Vijana wa leo wanalelewa kwenye himaya ya adui lililo na viwango vya maadili vinavyodorora. Lakini kama mtumishi wa Bwana, ni naahidi kwamba mtalindwa na kukingwa kutokana na mashambulizi ya adui kama mtatii uvuvio ambao unaletwa na Roho Mtakatifu.

“Valieni kwa staha; ongeeni kwa adabu; sikiliza muziki uinuao. Epukeni uasherati na vitendo vinavyoshusha hadhi. Chukua hatua ya maisha yako na jiamrishe kuwa shujaa. Kwa sababu tunakutegemea sana wewe, utabarikiwa sana. Haupo mbali machoni pa Baba yako wa Mbinguni mwenye upendo” (“Ushauri kwa Vijana),” Ensign au Liahona, Nov. 2011, 18).

  • Katika maneno ya Rais Packer, nini kinachokuvutia zaidi? Kwa nini?”

Fanya muhtasri Alma 44:7–10 kwa kuelezea kuwa Zerahemna alitangaza kwamba yeye na watu wake hawakuamini kwamba Wanefi waliimarishwa na Mungu. Alijitolea kuhakikisha Walamani wanasalimisha silaha zao, lakini alikataa kuweka agano la amani Mualike mwanafunzi aliyesoma Alma 44:1–6 asome kwa sauti jibu alilotoa Moroni kwa Zerahemna, ambalo linapatikana katika Alma 44:11. Uliza darasa:

  • Unadhani kulikua na umuhimu gani kwa Moroni kuhakikisha wanaweka agano la amani na Walamani?

Fanya muhtasari Alma 44:12–20 kwa kuelezea kwamba wakati wengi wa Walamani walifanya agano la amani, Zerahemna aliwakusanya watu wake waliosalia kushindana na jeshi la Moroni. Na Wanefi walipoanza kuwaua, Zerahemna aliona maangamizo yao yaliyokuwa karibu sana na akaahidi kuingia kwenye agano la amani.

Shuhudia juu ya mkono wa ulinzi wa Bwana katika maisha ya wale wenye imani Kwake. Wahimize wanafunzi kupigana kishujaa kwa malengo yao ya haki na haja na kuamini katika ahadi za Mungu za kutusaidia, na kutunza, na kutulinda, almradi tuna imani na Yeye (Alma 44:4).

Tangazo na Habari za Usuli

Alma 36:3 Vita tunayopigana ilianza katika maisha kabla ya hapa duniani

Rais Gordon B. Hinckley alizungumzia uhalisia wa vita tuliyoingia kabla ya dunia kuanza.

“Kuna vita ambayo imeendelea kabla ya dunia kuumbwa na ambayo inaonekana itaendelea kwa muda mrefu ujao.

“Vita hiyo ….ni vita kati ya ukweli na makosa, kati ya uhuru na shuruti, kati ya wafuasi wa Kristo na wale waliomkataa Yeye. Maadui Zake wametumia kila mbinu kwenye huo mgongano.

“Ni kama ilivyokuwa mwanzoni. Waathiriwa wanaoanguka ni tunu kama wale ambao walioanguka hapo awali. Ni mapigano yanayoendelea.

vita inaendelea. “Vita inaendelea Inapiganwa katika maisha yetu wenyewe, usiku na mchana, katika nyumba zetu, katika kazi zetu, katika vyama vyetu vya shule; inapiganwa kwenye masuala ya mapenzi na heshima, ya utiifu na uaminifu, ya utiifu na uadilifu. Sote tunahusika navyo. Tunashinda, na siku za usoni hazijapata kuwa na mwanga zaidi ya sasa (The War We Are Winning, Ensign, Nov. 1986, 42, 44–45).

Alma 43:9, 45. Linda na imarisha familia

Dada Virginia U. Jensen wa Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama alirejelea onyo katika tangazo kuhusu familia “ Kuwa kuvunjika kwa familia kutawaletea watu binafsi, jamii na mataifa maafa yaliyotabiriwa na manabii wa kale na wale wa kisasa (Familia: Tangazo kwa Ulimwengu, Ensign au Liahona, Nov. 2010, 129). Dada Jensen alisema hivi: Ndugu na kina dada, tumo katikati ya uhalisi huo wakati huu. Ni wajibu wetu wote kulinda na kuimarisha familia (Come, Listen to a Prophet’s Voice, Ensign, Nov. 1998, 13–14).