Mkutano Mkuu
Kwa Umoja wa Kihisia Tunapata Nguvu pamoja na Mungu
Mkutano Mkuu wa Oktoba 2020


Kwa Umoja wa Kihisia Tunapata Nguvu pamoja na Mungu

Tutafutapo umoja wa kihisia, tunaita nguvu za Mungu ili kufanya juhudi zetu kuwa kamili zaidi.

Mama yake Gordon alimwambia Gordon kwamba kama angemaliza kazi zake, angemtengenezea keki Aina aipendayo zaidi. Kwa ajili yake pekee. Gordon alienda kufanya kazi ya kukamilisha kazi hizo, na mama yake akaandaa keki. Dada yake mkubwa Kathy alikuja nyumbani na rafiki. Aliona keki hiyo na akauliza ikiwa yeye na rafiki yake wangeweza kupata kipande.

“Hapana,” Gordon alisema, “ni keki yangu. Mama aliniokea, na ilibidi niifanyie kazi kuipata ”

Kathy hakupendezwa kwa hilo toka kwa kaka yake mdogo. Alikuwa mwenye kujipenda sana na asiye na ukarimu. Angewezaje kuwa na hiki chote mwenyewe?

Saa baadaye wakati Kathy alipofungua mlango wa gari kumpeleka rafiki yake nyumbani, pale kwenye kiti kulikuwa na karatasi nyepesi mbili zilizokunjwa vizuri, nyuma mbili zilikuwa zimewekwa juu, na vipande viwili vya keki kwenye sahani. Kathy alisimulia hadithi hii kwenye mazishi ya Gordon kuonyesha jinsi alivyokuwa tayari kubadilika na kuonyesha fadhila kwa wale ambao hawakustahili kila wakati.

Mnamo 1842, Watakatifu walikuwa wakifanya kazi kwa bidii kujenga Hekalu la Nauvoo. Baada ya kuanzishwa kwa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama mwezi Machi, Nabii Joseph mara nyingi alikuja kwenye mikutano yao kuwaandaa kwa maagano matakatifu, ya kuwa na umoja ambayo wangefanya hivi karibuni hekaluni.

Mnamo Juni 9, Nabii “alisema alikuwa anaenda kuhubiri rehema [.] Ikiwa Yesu Kristo na [malaika] watatupinga kwa mambo ya kipuuzi, sisi tutakuwaje? Lazima tuwe wenye rehema na tupuuze vitu vidogo.” Rais Smith aliendelea, “Inanisikitisha kwamba hakuna ushirika mkamilifu zaidi—ikiwa mshiriki mmoja anateseka wote wanatakiwa kuhisi—kwa umoja wa kihisia tunapata nguvu pamoja na Mungu” 1

Sentensi hiyo ndogo ilinishitua kama radi. Kwa umoja wa kihisia tunapata nguvu pamoja na Mungu. Ulimwengu huu sio vile ningetaka uwe. Kuna mambo mengi nataka kushawishi na kufanya kuwa bora. Na kusema ukweli, kuna upinzani mwingi kwa kile ninachotumainia , na wakati mwingine ninahisi sina nguvu. Hivi karibuni, nimekuwa nikijiuliza maswali ya kuchunguza: Ninawezaje kuelewa watu walio karibu nami vizuri? Je, Nitawezaje kuunda “umoja wa kihisia” wakati vyote huonekana vya kitofauti? Je, Ni nguvu gani kutoka kwa Mungu ninayoweza kupata ikiwa nimeunganishwa zaidi na wengine? Kutoka kwenye kuchunguza nafsi yangu, nina mapendekezo matatu. Labda yatakusaidia pia.

Kuwa na Rehema

Yakobo 2:17 inasema, “Fikirieni [kaka na dada] zenu jinsi mnavyojifikiria nyinyi wenyewe, na mfanye urafiki na wote na muwe wakarimu katika utajiri wenu, ili nao wawe matajiri kama nyinyi.” Acha tubadilishe neno utajiri kwa rehema—muwe wakarimu katika rehema yenu ili nao wawe matajiri kama nyinyi.”

Mara nyingi tunafikiria utajiri katika suala la chakula au pesa, lakini labda tunachohitaji zaidi katika kuhudumia kwetu ni rehema.

Rais wangu mwenyewe wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama hivi karibuni alisema: “Jambo ambalo mimi… ninakuahidi… wewe ni kwamba nitalinda jina lako. … Nitakuona kwa jinsi ulivyo katika ubora wako. … Sitasema kamwe chochote juu yako ambacho sio cha ukarimu, ambacho hakitakuinua. Ninakuomba unifanyie vivyo hivyo kwa sababu ninaogopa, kusema ukweli, juu ya kukukatisha tamaa. …

Joseph Smith aliwaambia akina dada siku hiyo ya Juni mnamo 1842:

“Wakati watu wanadhihirisha wema na upendo mdogo kwangu, Ee ni nguvu kiasi gani huja kutokana na hilo katika akili yangu. …

“… Tunapomkaribia zaidi Baba yetu wa mbinguni, ndivyo tunavyopaswa kuangalia kwa huruma juu ya nafsi zinazoangamia—[tunahisi kuwa tunataka] kuwabeba mabegani mwetu, na kuweka dhambi zao migongoni mwetu. [Hotuba yangu imekusudiwa kwa ajili ya] Jamii hii yote—ikiwa ungependa Mungu awarehemu, kuweni na rehema ninyi kwa ninyi.” 2

Hili lilikuwa shauri haswa kwa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama. Tusihukumiane au kuacha maneno yetu yaumize. Acha tuhifadhi majina ya kila mmoja na tutoe zawadi ya rehema. 3

Tengeneza Mashua Yako ibembee

Mnamo 1936, timu isiyojulikana ya kupiga makasia kutoka Chuo Kikuu cha Washington ilisafiri kwenda Ujerumani kushiriki Michezo ya Olimpiki. ilikuwa ni katika vina vya kuhofisha sana. Hawa walikuwa wavulana wa tabaka la wafanya kazi ambao miji yao midogo ya uchimbaji madini na isiyo ya kifahari walichangia kiasi kidogo kidogo ili kwamba waweze kusafiri kwenda Berlin. Kila hali ya mashindano ilionekana kubanwa dhidi yao, lakini kitu kilitokea kwenye mashindano. Kwenye ulimwengu wa kupiga makasia wanakiita “bembea.” Sikiliza maelezo haya kulingana na kitabu The Boys in the Boat:

Kuna jambo ambalo wakati mwingine hufanyika ambapo ni ngumu kufanikiwa na ni ngumu kufafanua. Linaitwa “bembea.” Inatokea tu wakati wote wanapiga makasia kwa umoja kamili kwamba hakuna hatua hata moja ambayo haiko katika uwiano.

Wapiga makasia lazima watawale kwa ari katika uhuru na wakati huo huo kushikilia kiukweli uwezo wao binafsi. Mbio hazishindwi na viumbe baki. Makundi mazuri yanafanya kazi kwa ushirikiano—-mtu wa kuongoza, mtu wa kushikilia akiba, mtu wa kupigana vita, mtu wa kuleta amani. Hakuna mpiga makasia aliye na thamani kubwa kuliko mwingine, wote ni rasilimali kwenye boti, lakini ili wapige makasia vizuri, lazima kila mmoja azingatie mahitaji na uwezo wa wengine—mtu mwenye mkono mfupi anaongeza juhudi kidogo, mwenye mkono mrefu anavuta zaidi kidogo.

Tofauti zinaweza kugeuzwa kuwa faida badala ya hasara. Ni kwa hivyo tu itaonekana kwamba boti inajisukuma yenyewe. Ni kwa hivyo tu maumivu yatafungua njia kuelekea furaha. “kubembea” kuzuri huwa kama ushairi. 4

Kinyume na vizuizi vikubwa, timu hii ilipata kubembea na ikashinda. Dhahabu ya Olimpiki ilikuwa ya kufurahisha, lakini umoja ambao kila mpiga makasia alipata siku hiyo ulikuwa wakati mtakatifu ambao ulikaa nao maisha yao yote.

Ondoa Maovu Kulingana na vile Mema Yanavyoweza Kukua

Kwenye mfano mzuri katika Yakobo 5, Bwana wa shamba la mizabibu alipanda mti mzuri kwenye ardhi nzuri, lakini ukaharibika kwa muda na ukazaa matunda ya mwituni. Bwana wa shamba la mizabibu anasema mara nane: “inanihuzunisha kwamba nitaupoteza mti huu;”

Lakini, tazama, yule mtumishi akamwambia Bwana wa shamba: “Uache kwa muda mdogo zaidi. Na Bwana akasema: Ndiyo, nitauacha kwa muda mdogo zaidi.” 5

Halafu yanakuja maagizo ambayo yanaweza kutumiwa kwetu sote tunaojaribu kupalilia na kupata matunda mazuri katika mashamba yetu madogo ya mizabibu: “mtafyeka iliyo miovu kulingana na vile iliyo mizuri itakavyomea,” 6

Umoja haufanyiki kama kiini macho; inalazimu kazi. Hakuna mpangilio, wakati mwingine si ya kupendeza, na hufanyika hatua kwa hatua tunapofyeka iliyo miovu kulingana na vile mizuri itakavyomea.

Hatuko peke yetu katika juhudi zetu za kuunda umoja. Yakobo 5 inaendelea, “Na ikawa kwamba watumishi walienda na kutumikia kwa nguvu zao; na Bwana wa shamba alifanya kazi pamoja nao.” 7

Kila mmoja wetu atakuwa na uzoefu wa kuumiza sana, mambo ambayo hayapaswi kutokea kamwe. Kila mmoja wetu pia, kwa nyakati tofauti, ataruhusu kiburi na majivuno kuharibu matunda tunayozaa. Lakini Yesu Kristo ndiye Mwokozi wetu katika mambo yote. Nguvu zake zinafika chini kabisa na kwa uhakika ziko kwetu wakati tunapomwita. Sisi sote tunaomba rehema kwa dhambi na kutofaulu kwetu. Yeye huitoa bila malipo. Na anatuuliza kama tunaweza kutoa rehema hiyo na uelewa huo kwa kila mmoja wetu.

Yesu alisema wazi: “muwe na umoja; na kama hamna umoja ninyi siyo wangu.” 8 Lakini ikiwa sisi ni wamoja—ikiwa tunaweza kubakiza kipande cha keki yetu au kuweka talanta zetu binafsi ili boti iweze kubembea kwa umoja mkamilifu—basi sisi ni Wake. Na atasaidia kufyeka iliyo miovu kulingana na vile mizuri itakavyomea.

Ahadi za Kinabii

Labda bado hatuwezi kuwa mahali tunapotaka kuwa, na hatuko sasa pale ambapo tutakuwa. Ninaamini mabadiliko tunayotafuta ndani yetu na katika vikundi tunavyohusika yatakuja kwa uchache kwa kuhamasishana na kwa wingi kwa kila siku kujaribu kuelewana kila mmoja wetu. Kwa nini? Kwa sababu tunajenga Sayuni—“Watu wa moyo mmoja na wazo moja” 9

Kama wanawake wa agano, tuna ushawishi mpana. Ushawishi huo hutumiwa wakati wa kila siku wakati tunaposoma na rafiki, kuwalaza watoto kitandani, kuzungumza na mwenzetu kwenye basi, kuandaa uwasilishaji na mwenzako. Tunayo nguvu ya kuondoa ubaguzi na kujenga umoja.

Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama na Wasichana si madarasa tu. Yanaweza pia kuwa uzoefu usiosahaulika ambapo wanawake tofauti sana wote huingia kwenye boti moja na safu hadi tutakapopata kubembeakwetu. Ninatoa mwaliko huu: kuwa sehemu ya nguvu ya pamoja inayobadilisha ulimwengu kwa wema. Jukumu letu la agano ni kuhudumu, kuinua mikono ambayo inaning’inia, kuweka watu wanaohangaika migongoni mwetu au mikononi mwetu na kuwabeba. Si vigumu kujua nini cha kufanya, lakini mara nyingi huenda kinyume na masilahi yetu ya ubinafsi na ni lazima tujaribu. Wanawake wa Kanisa hili wana uwezo usio na kikomo wa kubadilisha jamii. Nina imani kamili ya kiroho kwamba, tunapotafuta umoja wa kihisia, tunaita nguvu za Mungu ili kufanya juhudi zetu kuwa kamili zaidi.

Wakati Kanisa lilipokumbuka ufunuo wa 1978 juu ya ukuhani, Rais Russell M. Nelson alitoa baraka kubwa ya kinabii: “Ni sala yangu na baraka ninazoacha juu ya wale wote ambao wanasikiliza kwamba tuweze kushinda mzigo wowote wa udanganyifu na kutembea kwa haki na Mungu—na kila mmoja wetu—katika amani timilifu na usawa.” 10

Ninaomba tutumie baraka hii ya kinabii na tutumie juhudi zetu binafsi na za pamoja ili kuongeza umoja ulimwenguni. Ninaacha ushuhuda wangu katika maneno ya sala ya Bwana Yesu Kristo ya unyenyekevu, isiyopitwa na wakati: “ili wote wawe kitu kimoja. Baba wewe ulivyo ndani yangu nami ndani yako. ili wawe kitu kimoja ili wote wawe kitu kimoja ndani yetu.” 11 Katika Jina la Yesu Kristo, amina.