Mkutano Mkuu
Kuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa Wakuu
Mkutano Mkuu wa Oktoba 2020


Kuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa Wakuu

Akina kaka na dada, sasa nitawasilisha kwenu Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa Wakuu wa Kanisa kwa ajili ya kura yenu ya kuwakubali.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Russell Marion Nelson kama nabii, mwonaji, na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho; Dallin Harris Oaks kama Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza; na Henry Bennion Eyring kama Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza.

Wale wanaounga mkono wanaweza kuonesha.

Wale wanaopinga, kama wapo, wanaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Dallin H. Oaks kama Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na M. Russell Ballard kama Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

Wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: M. Russell Ballard, Jeffrey R. Holland, Dieter F. Uchtdorf, David A. Bednar, Quentin L. Cook, D. Todd Christofferson, Neil L. Andersen, Ronald A. Rasband, Gary E. Stevenson, Dale G. Renlund, Gerrit W. Gong, na Ulisses Soares.

Wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali washauri katika Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji, na wafunuzi.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Kinyume, kama kuna yeyote, kwa ishara hiyo hiyo.

Tumewapumzisha Wazee L. Whitney Clayton, Enrique R. Falabella, na Richard J. Mayness Kama Sabini Wenye Mamlaka na kuwapa hadhi hiyo wakiwa wamestaafu.

Wale ambao wangependa kuungana nasi katika kutoa shukrani kwa Ndugu hawa na familia zao kwa huduma yao kuu, tafadhali onesheni.

Tumempumzisha Mzee L. Todd Budge kama Sabini Mkuu Mwenye Mamlaka.

Wote wanaotaka kumshukuru kwa huduma yake, tafadhali fanya hivyo kwa mkono ulioinuliwa.

Tumewapumzisha Maaskofu Dean M. Davies na W. Christopher Waddell kama Washauri wa Kwanza na wa Pili, kwa mtiririko huo, katika Uaskofu Simamizi.

Wale wanaopenda kuonyesha shukrani kwa Ndugu hawa kwa huduma yao ya kujitolea, tafadhali onyesheni.

Tumewapumzisha wafuatao kama Sabini wa Maeneo: Ruben Acosta, René R. Alba, Alberto A. Alvarez, Vladimir N. Astashov, José Batalla, Bradford C. Bowen, Sergio Luis Carboni, Armando Carreón, S. Marc Clay Jr., Z. Dominique Dekaye, Osvaldo R. Dias, Michael M. Dudley, Mark P. Durham, E. Xavier Espinoza, James E. Evanson, Paschoal F. Fortunato, Sam M. Galvez, Patricio M. Giuffra, Leonard D. Greer, Daniel P. Hall, Toru Hayashi, Paul F. Hintze, Adolf J. Johansson, Wisit Khanakham, Seung Hoon Koo, Pedro X. Larreal, Johnny L. Leota, José E. Maravilla, Joel Martinez, Joaquim J. Moreira, Isaac K. Morrison, Eduardo A. Norambuena, Ferdinand P. Pangan, Jairus C. Perez, Steven M. Petersen, Jay D. Pimentel, Edvaldo B. Pinto Jr., Alexey V. Samaykin, K. David Scott, Rulon F. Stacey, Karl M. Tilleman, William R. Titera, Carlos R. Toledo, Cesar E. Villar, David T. Warner, Gary K. Wilde, na William B. Woahn.

Wale wanaopenda kuungana nasi katika kutoa shukrani kwa huduma yao nzuri, tafadhali wadhihirishe.

Mzee L. Whitney Clayton akiwa amepumzishwa kama Sabini Mkuu Mwenye Mamlaka na kupewa wadhifa huo akiwa amestaafu, pia amepumzishwa kama mshiriki wa Urais wa Sabini.

Mzee Brent H. Nielson ameitwa kama mshiriki wa Urais wa Sabini, na tunapendekeza kwamba aidhinishwe.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onyesheni.

Yeyote anayepinga, anaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tumuidhinishe Dean M. Davies kama Sabini Mkuu Mwenye Mamlaka.

Wale wanaounga mkono, tafadhali dhihirisheni.

Wanaopinga wanaweza kuonyesha vivyo hivyo.

Inapendekezwa kwamba tumuidhinishe W. Christopher Waddell kutumikia kama Mshauri wa Kwanza katika Uaskofu Simamizi and L. Todd Budge kutumikia kama Mshauri wa Pili katika Uaskofu Simamizi.

Wale wanaounga mkono, waoneshe.

Yeyote anayepinga kwa ishara hiyo hiyo.

Imependekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama Sabini wa Eneo wapya: Laurian P. Balilemwa, Jonathon W. Bunker, Enrique R. Mayorga, and Konstantin Tolomeev.

Wale wanaounga mkono wanaweza kuonesha.

Wale wanaopinga, kama wapo, wanaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali Viongozi wengine Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Maeneo, na Maafisa Wakuu wa Kanisa Kama ilivyo sasa.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Kinyume, kama kuna yeyote, kwa ishara hiyo hiyo.

Wale waliopinga mapendekezo yoyote wanapaswa kuwasiliana na rais wao wa kigingi.

Akina kaka na dada, tunatoa shukrani kwa imani na maombi yenu endelevu kwa niaba ya viongozi wa Kanisa.