Rafiki
Isaya Nabii
Desemba 2026


“Isaya Nabii,” Rafiki, Des. 2026, 46–47.

Ujumbe wa kila mwezi wa Rafiki, Desemba 2026

Isaya Nabii

Kielelezo cha Isaya akimwona Bwana katika ono

Siku moja hekaluni, Bwana alimwita Isaya kuwa nabii. Isaya aliwapenda watu na akawafundisha kuhusu kuja kwa Kristo.

Kielelezo cha Isaya akitoa unabii kuhusu kuzaliwa kwa Yesu Kristo

Isaya alijifunza kwamba Yesu Kristo angekuja siku moja kuwaokoa watu Wake kutokana na dhambi. Lakini sio kila mtu angemtambua Yeye kama Mwokozi wao. Isaya alihuzunika sana kwa sababu alijua kuwa watu wengi hawangeamini katika Yesu Kristo.

Kielelezo cha Isaya akiandika kuhusu Ujio wa Pili wa Yesu Kristo

Isaya pia alitoa unabii juu ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Siku moja Yeyey atarudi tena na kuwa Mfalme wa dunia yote. Yeye atarudi tena na kukamilisha mpango wa Baba Yake kwa kuleta ukarimu na amani milele. Isaya alisema kila mmoja angejua kuwa Yesu Kristo ni Mwokozi wao.

Ukurasa wa Kupaka Rangi

Yesu Kristo alizaliwa Bethlehemu.

Ukurasa wa kupaka rangi wa PDF wa Yusufu akimwongoza punda pamoja na Mariamu akiwa juu yake

Vielelezo na Audrey Day. Vinaweza kunakiliwa kwa matumizi ya Kanisa pekee.

Je, wewe unasherehekeaje kuzaliwa kwa Mwokozi?