Rafiki
Salama katika Moto
Oktoba 2026


“Salama katika Moto,” Rafiki, Okt. 2026, 46–48.

Ujumbe wa Kila Mwezi wa Rafiki, Oktoba 2026

Salama katika Moto

Kielelezo cha Mfalme Nebukadreza

Mfalme Nebukadreza alitengeneza sanamu kubwa ya dhahabu na kuwalazimisha watu wake waiabudu. Ikiwa wangekataa, wangetupwa kwenye tanuru la moto.

Kielelezo cha Shadraka, Meshaki, na Abednego na askari

Shadraka, Meshaki, na Abednego walimpenda Mungu na hawangemwabudu mungu wa uongo wa mfalme.

Kielelezo cha marafiki wakizungumza na mfalme

Marafiki watatu walimwambia mfalme kwamba wangemwabudu Mungu pekee. Waliamini Mungu angeweza kuwalinda. Lakini hata ikiwa Yeye asingewaokoa, wangesimamia kile walichokiamini.

Kielelezo cha Shadraka, Meshaki, na Abednego katika tanuru

Mfalme alikasirika. Alisababisha watupwe ndani ya tanuru la moto. Lakini mfalme alipotazama ndani ya tanuru, alishangazwa kuona kiumbe wa mbinguni ndani ya moto akiwa na wanaume watatu.

Kielelezo cha mfalme akimwangalia Shadraka, Meshaki, na Abednego wakitoka nje ya tanuru

Mfalme aliwaita Shadraka, Meshaki, na Abednego, na walitoka nje ya tanuru. Moto haukuwadhuru au hata kuchoma nguo zao.

Kielelezo cha Shadraka, Meshaki, na Abednego wakitembea na kuzungumza na mfalme

Shadraka, Meshaki, na Abednego walitii amri za Mungu, hata wakati maisha yao yalipokuwa hatarini. Mfano wao ulimsaidia mfalme kuamini katika Mungu.

Ukurasa wa Kupaka Rangi

Manabii Wameitwa Kunena Maneno ya Bwana.

Ukurasa wa PDF wa kupaka rangi wa manabii wa Kibiblia

Vielelezo na Audrey Day. Vinaweza kunakiliwa kwa matumizi ya Kanisa pekee.

Ni kwa jinsi gani wewe unamfuata nabii?