Kwa ajili ya Watoto Wakubwa
Huduma Rahisi
-
Toa tabasamu kwa kila watu unaowaona.
-
Andika barua kwa mmisionari.
-
Imba wimbo wa kumchamngamsha mtu.
Upishi na gazeti la Rafiki
Napenda kuandaa mapishi kutoka kwenye gazeti la Rafiki! Moja ya malengo yangu kwa ajili ya programu ya Watoto na Vijana ni kujifunza jinsi ya kupika. Inaburudisha sana kufuatilia mapishi na pia ni matamu sana. Mimi ninajifunza mbinu mpya za kupika.
David A., umri miaka 9, Utah, Marekani
Dokezo la Maandalizi ya Hekaluni
Andika wimbo au shairi kuhusu hekalu, au chora picha ya moja lililo karibu na kwenu.
Changamoto ya Sanaa
Jaza nafasi hii kwa mitindo mingi kadiri uwezavyo.
Maneno ya Kuvutia
“Furahini siku zote, na toeni shukrani katika kila kitu.” Mafundisho na Maagano 98:1