Maandiko Matakatifu
1 Nefi 2


Mlango wa 2

Lehi anachukua jamii yake nyikani kando ya Bahari ya Shamu—Wanaacha mali yao—Lehi anamtolea Bwana dhabihu na anawafundisha wanawe kuweka amri—Lamani na Lemueli wananungʼunika dhidi ya baba yao—Nefi ni mtiifu na anasali kwa imani; Bwana anamzungumzia na anachaguliwa kuwaongoza kaka zake. Karibia mwaka wa 600 K.K.

1 Kwani tazama, ikawa kuwa Bwana alimzungumzia baba yangu, ndiyo, hata katika ndoto, na akamwambia: Umebarikiwa ewe Lehi, kwa sababu ya vitu ambavyo umetenda; na kwa sababu umekuwa mwaminifu na kuwatangazia hawa watu vile vitu nilivyokuamrisha, tazama, wanakutafuta awatoe uhai wako.

2 Na ikawa kwamba Bwana aakamwamrisha baba yangu, hata kwenye bndoto, kuwa caichukue jamii yake na aelekee nyikani.

3 Na ikawa kwamba alikuwa amtiifu kwa neno la Bwana, kwa hivyo alitenda kulingana na yale Bwana aliyomwamuru.

4 Na ikawa kwamba akatoka na kuelekea nyikani. Na akaacha nyumba yake, na nchi yake ya urithi, na dhahabu yake, na fedha yake, na vitu vyake vya thamani, na hakubeba chochote, isipokuwa jamii yake, na maakuli, pamoja na mahema, na aakaelekea nyikani.

5 Na akashuka mipakani karibu na ufuko wa aBahari ya Shamu; na akasafiri nyikani mipakani ambayo imekaribia Bahari ya Shamu; na akasafiri nyikani na jamii yake, ambayo ilikuwa ni mama yangu, Saria, na kaka zangu wakubwa ambao walikuwa ni bLamani, Lemueli, na Samu.

6 Na ikawa kwamba baada ya yeye kusafiri nyikani kwa siku tatu, alipiga hema lake abondeni kando ya mto wa maji.

7 Na ikawa kwamba alijenga amadhabahu ya bmawe, na akamtolea Bwana dhabihu, na ckumshukuru Bwana Mungu wetu.

8 Na ikawa kwamba aliuita ule mto, Lamani, na ulitiririka ukielekea Bahari ya Shamu; na bonde lilikuwa mipakani karibu na kinywa cha huo mto.

9 Na wakati baba yangu alipoona kwamba maji ya ule mto yalitiririka kwenye chemchemi ya Bahari ya Shamu, alimzungumzia Lamani, na kusema: Ee kwamba uwe kama mto huu, daima ukitiririka kwenye chemchemi ya haki yote!

10 Na pia akamzungumzia Lemueli: Ee kwamba uwe kama bonde hili, imara na thabiti, na asiyetingishika kwa kuweka amri za Bwana!

11 Sasa aliyazungumza haya kwa sababu ya ugumu wa Lamani na Lemueli; kwani tazama awalinungʼunika kwa vitu vingi dhidi ya bbaba yao, kwa sababu alikuwa ni mtu wa cmaono, na alikuwa amewatoa kutoka nchi ya Yerusalemu, kuacha nchi yao ya urithi, na dhahabu zao, na fedha zao, na vitu vyao vya thamani, kuangamia nyikani. Na wakasema alikuwa ametenda haya kwa sababu ya mafikira ya ujinga moyoni mwake.

12 Na hivyo ndivyo Lamani na Lemueli, wakiwa wakubwa, walivyonungʼunika dhidi ya baba yao. Na walinungʼunika kwa sababu ahawakujua matendo ya yule Mungu aliyewaumba.

13 Wala hawakuamini kuwa Yerusalemu, mji ule mkuu, aungeangamizwa kulingana na maneno ya manabii. Na walikuwa kama Wayahudi waliokuwa Yerusalemu, ambao walimtafuta baba yangu wakitaka kumtoa uhai wake.

14 Na ikawa kwamba baba yangu akawazungumzia katika bonde la Lemueli, akwa nguvu, akiwa amejazwa na Roho, hadi miili yao bikatetemeka mbele yake. Na aliwafadhaisha, kwamba hawakunena lolote kinyume chake; kwa hivyo, wakatenda alivyowaamrisha.

15 Na baba yangu aliishi kwenye hema.

16 Na ikawa kwamba mimi, Nefi, nikiwa mdogo, ingawa nilikuwa na mwili mkubwa, na pia nikiwa na hamu ya kujua asiri za Mungu, kwa hivyo, nikamlilia Bwana; na tazama bakanijia mimi, na cakanigusa moyo wangu kwamba dnikaamini maneno yote ambayo ebaba yangu alikuwa amezungumza; kwa hivyo, mimi sikumwasi kama kaka zangu.

17 Na nikazungumza na Samu, nikimjulisha vile vitu ambavyo Bwana alikuwa amenidhihirishia kwa Roho Mtakatifu. Na ikawa kwamba aliamini maneno yangu.

18 Lakini, tazama, Lamani na Lemueli hawakusikiza maneno yangu; na nikiwa animehuzunishwa na ugumu wa mioyo yao nikamlilia Bwana kwa niaba yao.

19 Na ikawa kwamba Bwana akanizungumzia, akisema: Umebarikiwa ewe, Nefi, kwa sababu ya aimani yako, maana umenitafuta kwa bidii, kwa unyenyekevu wa moyo.

20 Na kadiri utakavyozishika amri zangu, wewe autafanikiwa, na utaongozwa kwa bnchi ya ahadi; ndiyo, hata nchi ambayo nimekutayarishia wewe; ndiyo nchi ambayo ni bora kuzidi nchi zingine.

21 Na kadiri kaka zako watakavyokuasi wewe, awatatengwa mbali na Bwana.

22 Na kadiri utakavyo weka amri zangu, wewe utakuwa amtawala na mwalimu wa kaka zako.

23 Kwani tazama, katika siku ile watakaponiasi, anitawalaani hata na laana kali, na hawatakuwa na uwezo juu ya uzao wako ijapokuwa pia nao waniasi.

24 Na kama wataniasi, watakuwa amjeledi kwa uzao wako, kwa bkuwavuruga wakumbuke njia zangu.