Somo la 36: “Jangwa Litashangilia, na Kuchanua kama Ua la Waridi”

Mafundisho na Maagano na Historia ya Kanisa: Mafundisho ya Injili Kitabu cha Kiada cha Mwalimu., 1999


Madhumuni

Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa jinsi walivyobarikiwa kwa sadaka ya Watakatifu wa mwanzo katika Bonde la Salt Lake na kuwatia moyo kufuata mfano wa waumini hawa wema.

Matayarisho

 1. 1.

  Kwa maombi jifunze Urithi Wetu, ukurasa wa 81–96.

 2. 2.

  Pitia nyenzo kwaajili ya somo hili katika Class Member Study Guide (35686). Panga njia za kurejea kwenye nyenzo wakati wa somo.

 3. 3.

  Waambie washiriki wa darasa kujiandaa kufanya muhtasari wa sehemu zifuatazo kutoka kwenye Urithi Wetu:

  1. a.

   “Mwaka wa Kwanza katika Bonde” na “Uvumbuzi” (ukurasa wa 82–84).

  2. b.

   “Wito wa Kutawala” (kurasa za 86–89).

  3. c.

   “Wamisionari Wanaitika Wito” (kurasa za 84–86).

  4. d.

   “Kazi ya Umisionari” (kurasa za 93–96).

 4. 4.

  Kama picha zifuatazo zipo, andaa kuzionyesha wakati wa somo: Hekalu la Salt Lake 62433; Picha za Sanaa za Injili 502; ukurasa wa 210 katika kitabu cha kiada hiki);); Brigham Young (Picha za Sanaa za Injili 507); na John Taylor (Picha za Sanaa za Injili 508).

Mapendekezo kwa ajili ya Kuendeleza Somo

Shughuli ya Usikivu

Kama inafaa, tumia shughuli ifuatayo au moja ya kwako mwenyewe kuanza somo.

Onyesha picha ya Hekalu la Salt Lake. Elezea kwamba chini ardhini chini ya hekalu kuna msingi imara wa vitalu vya mawe. Msingi umesaidia hekalu hili kwa zaidi ya miaka 150.

 • Kwa nini ni muhimu kwamba msingi wa jengo uwe imara na uende chini?

Elezea kwamba kama lilivyo jengo linalohitaji msingi imara, vivyo hivyo na maisha yetu. Somo hili linajadili ujenzi wa Hekalu la Salt Lake na juhudi za watangulizi kuanzisha makao yao mapya na kuieneza injili. Pia linajadili baadhi ya kanuni za msingi ambazo Watakatifu wa mwanzo walizijenga katika maisha yao na jinsi tunavyoweza kujifunza mifano yao.

Majadiliano na Matumizi

Kwa maombi chagua somo nyenzo ambalo litatimiza mahitaji ya darasa. Wahamasishe washiriki wa darasa waelezee uzoefu ambao unahusiana na majadiliano.

1. “Hapa litasimama hekalu la Mungu wetu.”

Elezea kwamba mnamo Julai 28, 1847, siku nne baada ya kuwasili katika Bonde la Salt Lake, Rais Brigham Young alisimama mahali ambapo Hekalu la Salt Lake sasa limesimama. Alipiga fimbo yake ardhini na kusema, “Hapa litasimama hekalu la Mungu wetu” (katika Wilford Woodruff, Deseret Evening News, 25 Julia, 1888, 2). Hivyo dhabihu na baraka za kujenga hekalu lingine zilianza.

Mzee John A. Widtsoe wa Akidi ya Kumi na Wawili alisema, “Watangulizi walikuwa na njaa na wamechoka; walihitaji chakula na mapumziko; jangwa lenye uadui liliwatazama usoni; hata hivyo katikati ya mahitaji kama yale ya kimwili kwanza waligeukia ujenzi wa hekalu na chakula na nguvu za kiroho” (katika Conference Report, Apr. 1943, 38).

Ndani ya wiki moja baada Rais Young kuweka alama sehemu ya hekalu, Watakatifu walianza kupima mji mpya, pamoja na hekalu likiwa katikati ya upimaji. Mpangilio wa mji uliwavutia watu kwenye hekalu.

 • Kwa nini hekalu linatakiwa kuwa kitovu cha maisha yetu leo? (Ona nukuu ifuatayo.) Tunawezaje kuliweka hekalu kuwa sehemu muhimu zaidi ya maisha yetu?

  Rais Howard W. Hunter alifundisha:

  “Sisi … sisitiza baraka binafsi za kuabudu hekaluni na utakatifu na usalama ambao unatolewa kwa wale walio ndani ya kuta tukufu. Ni nyumba ya Bwana, sehemu ya ufunuo na amani. Tunapohudhuria hekalu, tunajifunza zaidi na kwa undani umuhimu wa maisha na umuhimu wa dhabihu ya upatanisho ya Bwana Yesu Kristo. Acha tulifanye hekalu, pamoja na ibada ya hekalu na maagano ya hekalu na ndoa ya hekalu, malengo yetu ya duniani na uzoefu wa mwili wa kufa. …

  “Naomba acha maana na uzuri na amani ya hekalu kuja katika maisha yako ya kila siku moja kwa moja” (katika Conference Report, Oct. 1994, 118 au Ensign, Nov. 1994, 87–88).

Onyesha picha ya Hekalu la Salt Lake. Elezea kwamba uchimbaji kwa ajili ya msingi mkubwa ulifanywa kwa mkono, ukihitaji maelfu ya masaa ya kazi. Jiwe kuu la pembeni liliwekwa tarehe 6 Aprili 1853. Baada ya miaka michache ya kazi ya msingi, Watakatifu walisimama kufanyakazi kwa sababu ya tatizo na serikali ya Marekani. Rais wa Marekani alisikia habari za uongo kwamba Watakatifu walikuwa wanagoma dhidi ya serikali, hivyo akatuma jeshi kwenda Bonde la Salt Lake. Katika majibu, Rais Young aliwaambia Watakatifu kufukia msingi kwa udongo ionekane kama uwanja wa kawaida.

Wakati Watakatifu baadaye walipoondoa udongo kwenye msingi wa mawe, waligundua nyufa kwenye mawe. Waliondoa jiwe la mchanga na kuweka matofali ya matale. Rais Young alisisitiza kwamba ni vifaa bora pekee na ufunidistadi ndio utumike katika ujenzi wa hekalu. Alisema:

“Nataka kuona hekalu linajengwa kwa njia ambayo litahimili hadi Milenia. Hili siyo hekalu pekee tutakalojenga; yatakuwa mamia ya haya yamejengwa na kuwekwa wakfu na Bwana. … Na wakati Milenia imepita, … ninataka hekalu lile libaki limesimama kama jengo la ukumbusho la kujivunia la imani yetu, uvumilivu na sekta ya Watakatifu wa Mungu katika milima, katika karne ya kumi na tisa” (Discourses of Brigham Young, sel. John A. Widtsoe [1941], 395).

Iliwachukua miaka kwa Watakatifu kuchimba, kusafirisha, na kuchonga matofali ya tamale. Katika kipindi hiki, walipata shida ya kuendelea kuishi, wakiwa wamepoteza mazao yao kwa vitu vya asili, kwa kuhudumu misioni mbali, na kukubali wito wa kuondoka nyumbani mwao na kuanzisha jamii sehemu za mashambani. Pamoja na changamoto hizi nyingi, Watakatifu walivumilia, na kwa msaada wa Bwana walishinda. Hekalu la Salt Lake liliwekwa wakfu mwaka 1893, miaka 40 baada ya kuwekwa kwa jiwe kuu la pembeni.

 • Tunaweza kujifunza nini kutokana na uvumilivu wa Watakatifu wakiwa wanajenga Hekalu la Salt Lake? Ni vipi mfano wa uvumilivu wa Watakatifu unatusaidia sisi?

  Wakati Jeffrey R. Holland alipokuwa rais wa Chuo Kikuu cha Brigham Young, alifananisha ujenzi wa maisha yetu na ujenzi wa Hekalu la Salt Lake:

  “Mwanasayansi mwenye sifa wa Kimarekani alifananisha [Hekalu la Salt Lake] kama ‘ukumbusho wa uvumilivu wa Mormoni.’ Na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Damu, kazi, machozi, na jasho. Vitu vizuri daima vina thamani kuvimalizia. ‘Je, hamjui kuwa ninyi ni hekalu la Mungu?’ (1 Wakorintho 3:16.) Kwa uhakika zaidi sisi ndio Kadiri kazi na jitihada zinavyoweza kuonekana, ni lazima tuendelee kuchagiza na kuweka mawe ambayo yatafanya mafanikio yetu kuwa mazuri na sherehe kubwa ya kuvutia. Lazima tuchukue faida ya kila nafasi ili kujifunza na kukua, kuota ndoto na kuona maono, kutenda kuelekea kuelewa kwao, kusubiri kwa uvumilivu wakati tunapokuwa hatuna chaguo lingine, tuegemee upanga wetu na tupumzike kwa muda, lakini kusimama na kupambana tena. … Tunajenga msingi wa kazi kubwa—yetu ya baadaye isiyotabarika” (However Long and Hard the Road [1985], 127).

Hekalu la Salt Lake

Hekalu la Salt Lake Liliwekwa wakfu mwaka 1893, hekalu hili lilichukua miaka 40 kujenga.

2. Watakatifu walikuwa na utii walipokuwa wakitafuta na kuanzisha makao kwenye Bonde la Salt Lake na maeneo yaliyozunguka.

Elezea kwamba Watakatifu walikumbana na changamoto kubwa walipoanza jukumu la kuweka makao kwenye Bonde la Salt Lake na maeneo yaliyozunguka. Muombe mshiriki wa darasa aliyeandaliwa kufupisha sehemu “The First Year in the Valley” and “Explorations” from Urithi Wetu, kurasa za 82–84.

 • Ni tabia gani ziliwasaidia Watakatifu kushinda matatizo waliyokumbana nayo kipindi cha mwaka wa kwanza katika Bonde la Salt Lake? Ni hali gani katika maisha yetu ya leo inaweza kuhitaji sifa hizo hizo?

 • Je, Watakatifu walibarikiwa vipi wakati wa kipindi chao cha shida? Je, Bwana amekubariki vipi katika kipindi chako cha shida?

Muombe mshiriki wa darasa aliyeandaliwa kufupisha sehemu Wito wa Kutawala, kutoka Urithi Wetu, kurasa za 86–89.

 • Ni nini kinachokufurahisha kuhusu hadithi za Charles Lowell Walker and Charles C. Rich?

Elezea kwamba ndugu hawa wawili na familia zao ni mfano mzuri wa utiifu. Moja ya mafundisho makubwa ya historia ya Kanisa ni kwamba tutabarikiwa tunapomtii Bwana na kuwafuata manabii Wake. Mafundisho na Maagano pia yana mafundisho mengi kuhusu baraka za utiifu. Soma maandiko yafuatayo pamoja na washiriki wa darasa. Jadili kila fungu linafundisha nini kuhusu utii, kama inavyoonyesha chini.

 1. a.

  M&M 58:2–4. Kama tunatii amri na “tunakuwa waaminifu katika dhiki,” sisi “tutavikwa taji pamoja na utukufu mwingi.”)

 2. b.

  M&M 64:33–34. (Wale ambao wapotayari na watiifu watabarikiwa katika nchi ya Sayuni katika siku za mwisho.)

 3. c.

  M&M 82:10. (Bwana anafungwa wakati tukifanya asemayo. Atatubariki tunapotii amri Zake.)

 4. d.

  M&M 93:1. (Wale wanaotubu, kuja kwa Mwokozi, na kutii amri Zake watauona uso Wake.)

 5. e.

  M&M 130:19–21. (Mtu anayepata maarifa na akili zaidi kwa njia ya juhudi na utii katika maisha haya atakuwa na faida katika ulimwengu ujao. Tunapata baraka kwa kutii sheria za Mungu.)

 • Ni uzoefu gani ambao unaweza kushiriki vizuri ambao umekufundisha wewe umuhimu wa utiifu? Japokuwa hatujaitwa kutawala maeneo mapya, ni kwa njia zipi tunaombwa kumtii nabii leo? Unanakuwa na hisia gani unapokuwa mtiifu kwa mapenzi ya Mungu?

3. Wamisionari walitoa dhabihu ili kufundisha injili ulimwenguni kote.

Elezea kwamba wakati Watakatifu walipoweka makao katika Bonde la Salt Lake, Rais Brigham Young aliwaita wamisionari wengi ili kuhudumu ulimwenguni kote. Muombe mshiriki wa darasa aliyeandaliwa kufupisha sehemu Missionaries Answer the Call kutoka Urithi Wetu, kurasa za 84–86.

 • Ni katika maeneo gani ya dunia ambayo Watakatifu walifundisha injili wakati Rais Brigham Young akiliongoza Kanisa? Ni dhabihu gani ambazo Watakatifu wa mwanzo walizifanya ili kushiriki injili pamoja na watu wa duniani kote?

 • Jinsi gani imani na maombi ya Mzee Lorenzo Snow yalisaidia kufungua mioyo ya watu huko Italia katika ujumbe wa injili?

 • Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na mifano ya Mzee Edward Stevenson? Elizabeth na Charles Wood? Mzee Joseph F. Smith

Rais Brigham Young aliliongoza Kanisa kwa miaka 33. Baada ya Rais Young kufariki mwaka 1877, John Taylor aliliongoza Kanisa kwa miaka mitatu kama Rais wa Akidi ya Kumi na Wawili na kisha akasimikwa kama Rais wa Kanisa mnamo Oktoba 10, 1880 (Urithi Wetu, ukurasa wa 93).

Elezea kwamba chini ya uongozi wa Rais Taylor, Watakatifu waliendelea kuhubiri injili duniani kote. Muombe mshiriki wa darasa aliyeandaliwa kufupisha sehemu “Kazi ya Umisionari” kutoka Urithi Wetu, kurasa za 93–96.

 • Ni katika maeneo gani ya dunia ambayo Watakatifu walihubiri injili wakati Rais John Taylor akiliongoza Kanisa?

 • Jinsi gani Milton Trejo aliongoza katika maisha yake ili kuweza kushiriki katika kuujenga ufalme wa Mungu? Jinsi gani tunaweza kujiandaa vizuri sisi wenyewe ili kuujenga ufalme wa Mungu?

 • Je! Tunaweza kujifunza nini kutokana na hadithi ya Mzee Thomas Biesinger? Mzee Kimo Pelio na Samuela Manoa? Mzee na Dada Dean? Jonathan na Kitty Napela?

Hitimisho

Onyesha kwamba katika Bonde la Salt Lake, watakatifu walijenga msingi imara kwaajili ya hekalu la Bwana na kwaajili ya maisha yao. Watie moyo washiriki wa darasa kufuata mfano wa Watakatifu wa kale wa imani, uvumilivu, utii, na tamanio la kushiriki injili. Ukiongozwa na Roho wa Bwana, shuhudia kweli zilizojadiliwa wakati wa somo.