Somo la 35: Misioni ya Kuokoa

Mafundisho na Maagano na Historia ya Kanisa: Mafundisho ya Injili Kitabu cha Kiada cha Mwalimu., 1999


Madhumuni

Ni kufundisha kuhusu uokozi wa makundi ya mikokoteni ya Martin na Willie, kuonyesha kwamba injili ya Yesu Kristo ni ujumbe wa uokozi, na kuhamasisha washiriki wa darasa kusaidia kuokoa wale wenye shida.

Matayarisho

 1. 1.

  Kwa maombi jifunze maandiko yafuatayo na nyenzo nyingine:

  1. a.

   Mafundisho na Maagano 4:3–7; 18:10–16; 52:40; 81:5–6; 138:58.

  2. b.

   3 Nefi 18:31–32; Moroni 7:45–48 (maandiko ya kujaliza).

  3. c.

   Nukuu katika somo hili.

  4. d.

   Urithi Wetu, kurasa za 77–80.

 2. 2.

  Pitia nyenzo kwa ajili ya somo hili katika Class Member Study Guide (35686). Panga njia za kurejea kwenye nyenzo wakati wa somo.

 3. 3.

  Kama picha zifuatazo zipo, andaa kuzitumia wakati wa somo: Martin Handcart Co., Bitter Creek, Wyoming, 1856 (62554; Picha za Sanaa za Injili 414) na Vijana Watatu Waokoa Kuni la Mkokoteni la Martin (Picha za Sanna za Injili 415).

 4. 4.

  Kama unatumia shughuli ya usikivu, andaa kutumia picha zifuatazo katika nyongeza ya zile zilizoorodheshwa hapo juu: Kutoka (62493; Picha za Sanaa za Injili 411); Kundi la Mkokoteni (62528); na Mary Fielding and Joseph F. Smith Wakivuka Nyanda (62608).

Mapendekezo kwa ajili ya Kuendeleza Somo

Shughuli ya Usikivu

Kama inafaa, tumia shughuli ifuatayo au moja ya kwako mwenyewe kuanza somo.

Onyesha picha zilizoorodheshwa katika sehemu ya “Maandalizi,” vipengee vya 3 na 4.

 • Kwa nini ni muhimu kuendelea kurudia hadithi kuhusu uzoefu wa Watakatifu wa Siku za Mwisho watangulizi?

  Rais Gordon B. Hinckley alisema: “Hadithi za kuzingirwa kwa Watakatifu na mateso yao na kifo zitajirudia tena na tena. … Hadithi za uokozi wao zinatakiwa kurudiwa tena na tena. Zinaongea asili halisi ya injili ya Yesu Kristo” (katika Conference Report, Oct. 1996, 118–100; au Ensign, Nov. 1996, 86).

  Akirejea watangulizi Rais Hinckley pia alisema: “Siwezi kuacha kuwashukuru wao; ninatumaini nanyi hamtaacha kuwashukuru wao. Ninatumaini kwamba daima tutawakumbuka wao. … Acha tusome tena na tena, na tusome kwa watoto wetu au watoto wa watoto wetu, habari za wale walioteseka sana” (Church News, 31 July 1999, 5).

  Elezea kwamba somo hili linajadili maelezo ya mateso, kifo, na kuokoa: hadithi ya makundi ya mikokoteni ya Martin na Willie.

Majadiliano na Matumizi

Kwa maombi chagua somo nyenzo ambalo litatimiza mahitaji ya washiriki wa darasa. Wahamasishe washiriki wa darasa waelezee uzoefu ambao unahusiana na kanuni unazozifundisha.

1. Rais Brigham Young aliongoza uokozi wa makundi ya mikokoteni ya Martin na Willie.

Onyesha picha ya kundi la mikokoteni la Martin. Fupisha aya ya kwanza chini ya “Watangulizi wa Mikokoteni” kwenye ukurasa wa 77 wa Urithi Wetu. Kisha shiriki taarifa ifuatayo ya Rais Gordon B. Hinckley:

“Ninakurudisha nyuma hadi kwenye mkutano mkuu wa Oktoba 1856. Jumamosi ya mkutano ule, Franklin D. Richards na kundi la wafuasi waliwasili katika bonde. Walikuwa wamesafiri kutoka Winter Quarters na timu imara na magari ya kukokotwa na ng’ombe na waliweza kutumia muda mzuri. Kaka Richards mara moja alimtafuta Rais Young. Aliripoti kwamba kuna mamia ya wanaume na wanawake, na watoto wametawanyika njiani. … Walikuwa katika wakati mgumu. Majira ya baridi yalikuja mapema. Theruji nzito ya upepo ulikuwa ukivuma kelekea nyanda za juu. … Watu wetu walikuwa na njaa; mikokoteni yao na magari yao ya kukokotwa na ng’ombe yalikuwa yameharibika; ng’ombe wao walikuwa wanakufa. Watu wenyewe nao walikuwa wanakufa. Wote wangeangamia kama hawangeokolewa.

“Nafikiri Rais Young hakulala usiku ule. Nafikiri maono ya watu fukara, wenye baridi, wanaokufa walipanga msululu kwenye fikra zake. Asubuhi iliyofuata alikuja kwenye tabenakulo ambalo lilikuwa limesimama katika mraba huu. Aliwaambia watu:

“‘Sasa nitawapa watu hawa somo na maandiko kwa ajili ya Wazee ambao wataongea. … Ni hii. … Ndugu na dada zetu wengi wapo kwenye uwanda wakiwa na mikokoteni, na huenda wengi sasa wapo maili mia saba toka mahali hapa, na lazima waletwe hapa, lazima tutume msaada kwao. Maandishi yatakuwa, “kuwaleta hapa. …

“‘Hiyo ni dini yangu; hiyo ni amri ya Roho Mtakatifu ambayo ninayo. Ni kuwaokoa watu. …

“‘Nitawaita Maaskofu siku hii ya leo. Sitasubiri hadi kesho, wala siku inayofuata, kwa timu ya nyumbu 60 shupavu na magari 12 au 15 ya kukokotwa. Sitaki kutuma ng’ombe. Ninataka farasi na nyumbu wazuri. Wapo katika mipaka hii, na lazima tuwapate. Pia tani 12 za unga na waendeshaji wazuri wa farasi 40, mbali na wale wanaoongoza timu. …

“‘Nitawaambieni wote kwamba imani yenu, dini, kazi yenu ya dini, katu haitaokoa hata nafsi moja kati yenu katika Ufalme wa Selestia wa Mungu wetu, pasipo ninyi kutekeleza kanuni kama hizi ninazokufundisheni hivi sasa. Enendeni na mkawalete wale watu walio nyandani sasa’ (katika LeRoy R. Hafen na Ann W. Hafen, Handcarts to Zion [1960], 120–21).

“Mchana ule, chakula, vitanda, na nguo kwa idadi kubwa vilikuwa vimekusanywa na wanawake. Asubuhi iliyofuata, farasi waliandaliwa na mikokoteni ilitengenezwa na kupakiwa. Asubuhi iliyofuata, … timu za nyumbu 16 ziliondoka na kuelekea upande wa mashariki. Hadi kufikia mwisho wa Oktoba palikuwa na timu 250 barabarani ili kutoa msaada” (katika Conference Report, Oct. 1996, 117–18; au Ensign, Nov. 1996, 85–86).

Onyesha kwamba makundi ya mikokoteni ya Martin na Willie yalifanya yote yaliyowezekana kufika Bonde la Salt Lake, lakini walishindwa kuendelea zaidi. Walihitaji kuokolewa. Bila makundi ya uokozi, wote wangekufa.

 • Umeshapata uzoefu gani ambao umeweza kuokolewa? Ulijisikia vipi wakati ulipokuwa unahitaji msaada? Ulijisikia vipi wakati mtu alipokuja kukupa msaada?

 • Ni jinsi gani Watakatifu katika makundi ya mikokoteni walivyojisikia wakati makundi ya uokozi yalipowafikia?

Rais Hinckley alishiriki taarifa hii ya uokozi:

“Ilikuwa katika … hali ya kutisha na kukata tamaa—njaa, kuchoka, nguo zao nyepesi na chakavu—kwamba [makundi ya mikokoteni] yalipatikana na kundi la kuokoa. Pindi waokoaji walivyojitokeza upeo wa magharibi wakikatiza kwenye theruji, walionekana kama malaika wa rehema. Na hakika walikuwa. Wahamiaji waliozingirwa walishangilia kwa furaha, baadhi yao. Wengine, walikuwa wadhaifu kushangilia, walilia na kulia na kulia.

“Sasa palikuwa na chakula cha kula na wengine nguo zenye joto. Lakini mateso yalikuwa hawajaisha, wala hayawezi kwisha katika maisha haya. Viungo vilikuwa vimeganda, na mwili uliokosa damu wenye ngozi iliyokauka toka kwenye mifupa.

“Mikokoteni ilitelekzwa, na waliopona walijazana kwenye magari ya kukokotwa ya waokoaji. Safari ndefu mbaya ya maili mia tatu, mia nne, hata mia tano kati yao na bonde hili ilikuwa ni ya polepole na ya kuchosha kwa sababu ya tufani. Mnamo Novemba 30, magari yakuvutwa 104, yaliyojaa binadamu wanaotaabika, yalifika katika Bonde la Salt Lake. Neno la matarajio ya kuwasili kwao liliwafikia. Ilikuwa Jumapili, na tena Watakatifu walikusanyika katika Tabenakulo. Brigham Young alisimama mbele ya umati na kusema:

“‘Mara baada ya mkutano huu kwisha ninataka ndugu na dada kurudi nyumbani kwao. …

“‘Mkutano wa mchano utaondolewa, kwani nawataka akina dada … kuandaa kuwapa wale waliowasili kitu cha kula, na kuwaosha na kuwauguza. …

“‘Wengine mtawakuta miguu yao iliganda hadi kwenye visigino; wengine waliganda kwenye magoti na wengine mikono yao iliganda … ; tunataka ninyi kuwapokea kama vile watoto wenu wenyewe, na kuwa na hisia ileile kwa ajili yao’ (imedondolewa katika Hafen, Handcarts to Zion, p. 139)” (katika Conference Report, Oct. 1991, 76–77; au Ensign, Nov. 1991, 54).

 • Nini kinachokupendeza kuhusu juhudi za kuwaokoa watangulizi wa mikokoteni?

2. Bwana anatuokoa sisi kupitia dhabihu Yake ya Upatanisho.

Eleza kwamba injili ya Yesu Kristo ni ujumbe wa uokozi. Katika hotuba ya mkutano, baada ya kushiriki hadithi ya uokozi wa makundi ya mikokoteni, Rais Gordon B. Hinckley alishuhudia juu ya kazi ya uokozi ya Mwokozi.

“Ni kwa sababu ya dhabihu ya ukombozi iliyohemshwa na Mwokozi wa ulimwengu kwamba mpango mkuu wa injili ya milele unapatikana kwetu, kwa masharti ambayo wale wanaokufa katika Bwana hawataonja kifo bali watapata nafasi ya kuendelea kwenda selestia na utukufu wa milele.

“Katika kukosa kwetu msaada, Anakuwa Mwokozi wetu, akituokoa toka kwenye laana na kutleta katika uzima wa milele.

“Katika wakati wa kukata tamaa, katika misimu ya upweke na hofu, Yeye yupo pale kwenye upeo wa macho kuwaletea msaada na faraja na uhakika na imani. Yeye ni Mfalme wetu, Mtoaji wetu, Bwana wetu na Mungu wetu” (katika Conference Report, Oct. 1991, 78; au Ensign, Nov. 1991, 54).

 • Ni kwa njia gani tunahitaji kuokolewa na Mwokozi? Kwa nini Mwokozi ameweza kutuokoa sisi? (Ona Alma 7:11–13; M&M 18:11–12.) Tunapaswa kufanya nini ili kupokea ahadi Yake ya uokozi?

3. Kama Watakatifu wa siku za mwisho, tunatakiwa kuwaokoa wale wenye shida.

Onyesha picha ya vijana watatu wakiwaokoa watangulizi wa mikokoteni. Kisha soma hadithi ifuatayo aliyoshiriki Rais Thomas S. Monson:

“Acha kwa muda tuungane na Kapteni Edward Martin na kundi la mikokoteni aliyoiongoza. Wakati tunapohisi uchungu wa njaa ambao waliuona au uzoefu wa baridi kali ambayo iliingia kwenye miili yao iliyochoka, tutatoka kwenye ziara yetu kwa uelewa bora wa ugumu waliopata, ujasiri ulioonyeshwa, na imani kutimia. Tutashuhudia kwa macho yaliyojaa machozi jibu la kuvutia la swali ‘Mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?’

“‘Mikokoteni iliondoka Novemba 3 na kufika mto [Sweetwater], uliojaa barafu iliyokuwa ikielea. Kuvuka kulihitaji ujasiri na ushupavu zaidi, ilionekana, kuliko asili ya mwanadamu ingeweza kafaa. Wanawake walirudi nyuma na wanaume walilia. Baadhi walipita, lakini wengine hawakuweza kujaribu.

“‘Wavulana watatu wa umri wa miaka kumi na nane waliotoka kundi la msaada walikuja kuokoa; na kwa mshangao wa wote walioona, walimbeba karibu kila mtu ambaye hakujiweza wa kundi la mkokoteni kuwavusha ngambo ya mto wenye theruji. Uchovu ulikuwa wa ajabu, na ulionekana kuwa mkubwa, kwamba miaka ya baadaye wale wavulana wote walikufa kutokana na ile shida. Wakati Rais Young aliposikia tendo hili la kishujaa, alilia kama mtoto, na baadaye alitangaza waziwazi, “Tendo lile pekee litahakikisha C. Allen Huntington, George W. Grant, na David P. Kimball wokovu wa milele katika Ufalme wa Mungu wa Selestia, ulimwengu usio na mwisho”’ (LeRoy R. Hafen and Ann W. Hafen, Handcart to Zion [Glendale, California: The Arthur H. Clark Company, 1960], pp. 132–33).

“Huduma yetu kwa wengine inaweza isiwe kubwa, lakini inaweza kuimarisha roho, kuivisha miili iliyo na baridi, kuwalisha watu wenye njaa, kuifariji mioyo yenye huzuni, na kuiinua kwa urefu mpya nafsi zenye thamani” (katika Conference Report, Apr. 1990, 61–62; au Ensign, May 1990, 46–47).

Sisitiza kwamba kama waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, tuna kazi ya kuokoa. “Kazi yetu katika maisha, kama wafuasi wa Bwana Yesu Kristo,” alisema Rais Gordon B. Hinckley, “lazima iwe kazi ya kuokoa” (katika Conference Report, Oct. 1991, 78; au Ensign, Nov. 1991, 59). Kama vile Rais Monson alivyosema, huduma yetu huenda isiwe kubwa kama dhabihu iliyofanywa na vijana wale watatu katika historia. Hata hivyo, tunaweza kusaidia kuokoa wanafamilia, marafiki, na wengine kupitia juhudi zetu rahisi za kila siku za upendo, kuhudumu, na kuwafundisha.

 • Je, ni mambo gani dhahiri ambayo tunatakiwa kuyafanya ili kuwaokoa wale wenye shida? (Andika majibu ya washiriki wa darasa kwenye ubao. Kama sehemu ya majadiliano, shiriki nukuu ifuatayo.)

  Akirejea kwa mateso ya makundi ya mikokoteni ya Martin na Willie, Rais Hinckley alisema:

  “Ninafufaha kwamba siku zile za watangulizi zimepita. Ninashukuru kwamba hatuna ndugu na dada waliokwama kwenye theruji, wakiganda na kufa, wakati wakijaribu kuja hapa, kwenye Sayuni yao katika milima. Lakini kuna watu, sio wachache, ambao hali zao ni mbaya na ambao wanalia kwa ajili ya msaada na faraja.

  “Kuna wengi ambao wana njaa na fukara ulimwenguni kote ambao wanahitaji msaada. … Jukumu letu ni kubwa na takatifu ili kuwafikia na kuwasaidia, kuwainua, kuwalisha kama wana njaa, kuzistawisha roho zao kama wana kiu ya ukweli na haki.

  “Kuna vijana wengi ambao wanazurura bila sababu na kufuata njia za madawa, genge, tabia mbaya, na kundi zima la shida zinazotokana na mambo haya. Kuna wajane ambao wanahitaji sauti za kirafiki na roho anayependa kujali ambaye anaongea upendo. Kuna wale ambao wakati fulani walikuwa na joto katika imani, lakini imani zao zimekuwa baridi. Wengi wao wanatamani kurudi lakini hawaujui hasa jinsi ya kufanya hivyo. Wanahitaji mikono ya urafiki ili kuweza kuwafikia. Kwa juhudi kidogo, wengi wao wanaweza kurudishwa tena kula katika meza ya Bwana.

  “Ndugu na dada zangu, ningetumaini, ningeomba kwamba kila mmoja wetu … Angeamua kuwatafuta wale wanaohitaji msaada, wale waliokata tamaa na hali ngumu, na kuwainua katika roho wa upendo hadi kwenye kumbatio la Kanisa, ambako mikono imara na mioyo ya upendo itawapa joto, wafariji, kuwaidhinisha, na kuwaweka kwenye njia ya furaha na maisha mazuri” (katika Conference Report, Oct. 1996, 118; au Ensign, Nov. 1996, 86).

Waambie washiriki wa darasa kusoma maandiko yafuatayo, wakiangalia ushauri wa nini tunaweza kufanya ili kuwaokoa wale wenye shida. Tumia maswali kuhamasisha mjadala na matumizi.

 1. a.

  M&M 4:3–7; Moroni 7:45–48. Ni jinsi gani tabia zilizoorodheshwa katika aya hizi zinaweza kutusaidia sisi kuwaokoa wale wenye shida?

 2. b.

  M&M 18:10–16. Ni nafasi zipi tulizonazo za kufundisha injili na kuwaongoza wengine kwenye toba?

 3. c.

  M&M 52:40. Je, tunawezaje kuwasaidia “maskini na wenye shida, wagonjwa na wanaoteseka”? Kwa nini sisi siyo wanafunzi wa Mwokozi kama hatuwasaidii walio na shida?

 4. d.

  M&M 81:5–6. Ina maana gani “kuinua juu mikono iliyolegea, na kuyaimarisha magoti yaliyo dhaifu”? Inawezekana vipi amri hii ifanye kazi kwenye mahitaji ya kiroho na pia kimwili?

 5. e.

  M&M 138:58. Ni jinsi gani tunawaokoa watu kupitia kazi ya hekalu?

 6. f.

  3 Nefi 18:31–32. Tunaweza kufanya nini ili kuendelea kuhudumia wale walioanguka?

 • Waombe washiriki wa darasa kutafakari kuokolewa kwa makundi ya mikokoteni ya Martin na Willie. Tunapojitahidi kuwaokoa wengine, tunaweza kujifunza nini kutoka kwa mifano ya Rais Brigham Young na Watakatifu walioyaokoa makundi ya mikokoteni yaliyokwama? (Majibu yanaweza kujumuisha kwamba tusicheleweshe juhudi zetu, kwamba mara nyingi tunatakiwa kuweka kando matatizo yetu ili kuwasaidia wengine, na kwamba tunatakiwa kuonyesha imani.)

Hitimisho

Wahimize washiriki wa darasa kutafuta njia za kutumia kanuni zilizojadiliwa katika somo hili. Sisitiza kwamba tunapojitahidi kuwasaidia wale walio na shida ya kuokolewa, hatutakiwi kukata tumaini. Lazima tuondokane na ubinafsi, na lazima tuwafikie kwa upendo. Ukiongozwa na Roho wa Bwana, shuhudia kweli zilizojadiliwa wakati wa somo.

Mawazo ya Ziada ya Kufundishia

Unaweza ukataka kutumia moja au zaidi ya mawazo yafuatayo ili kuongeza muhtasari wa somo uliopendekezwa.

1. “Tulimtambua [Mungu] katika mateso yetu”

Waambie washiriki wa darasa kushiriki hadithi ya Nellie Pucell kutoka kwenye Urithi Wetu, kurasa za 77–78. Mualike mshiriki mwingine wa darasa kujiandaa kushiriki hadithi ya mtu ambaye alishuhudia kwamba yeye na watangulizi wengine wa mkokoteni “walimtambua [Mungu] katika mateso [yao]” (Urithi Wetu ukurasa wa 78).

 • Tunaweza kujifunza nini katika hadithi hizi? Umewezaje kuona kwamba tunaweza kumjua vizuri Mungu tunapovumilia mateso?

Kama sehemu ya majadiliano haya, unaweza kutaka washiriki wa darasa kusoma M&M 122:5–8.

2. “Kama ulimwengu utaokolewa, tunatakiwa kufanya hivyo”

Kusisitiza jukumu la kuwaokoa wale wenye shida, shiriki taarifa ifuatayo ya Rais Gordon B. Hinckley:

“Ujumbe wetu ni muhimu sana, wakati unaacha kufikiri kwamba wokovu, ni wokovu wa milele, upo mabegani mwa Kanisa hili. Wakati yote yakiwa yamesemwa na kwisha, kama ulimwengu utaokolewa, tunatakiwa kufanya hivyo. Hakuna kwa kukimbilia kutoka hapo. Hakuna watu wengine katika historia ya ulimwengu wamepokea amri kama hii ambayo sisi tumepokea. Tunawajibika kwa ajili ya wote walioishi juu ya dunia. Hiyo inajumuisha historia yetu ya familia na kazi ya hekalu. Tunawajibika kwa ajili ya wote wanaoishi juu ya dunia, na kwamba inahusu kazi yetu ya umisionari. Na tutawajibika kwa ajili ya wote watakaoishi juu ya dunia” (Church News, 3 July 1999, 3).

3. “Walijaribu Mambo Yote” maonyesho ya video

Kama video ya Mafundisho kutoka Mafundisho na Maagano na Historia ya Kanisa (53933) inapatikana, fikiria kuonyesha “Walijaribu Mambo Yote,” yenye dakika–nne.