Somo la 34: Imani katika Kila Hatua

Mafundisho na Maagano na Historia ya Kanisa: Mafundisho ya Injili Kitabu cha Kiada cha Mwalimu., 1999


Madhumuni

Ni kuwasaidia wanafunzi kuelewa jinsi safari ya watangulizi kwenda bonde la Salt Lake inafanana na safari yetu kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni na kuwasaidia wanafunzi kushukuru kwa ajili dhabihu iliyofanywa na watangulizi.

Matayarisho

  1. 1.

    Kwa maombi jifunze maandiko yafuatayo na nyenzo zingine:

    1. a.

      Mafundisho na Maagano 136.

    2. b.

      Urithi Wetu, kurasa 71–77,

  2. 2.

    Hakiki nyenzo kwa somo hili katika mwongozo wa mafunzo kwa wanafunzi (35686). Panga njia za kurejea kwenye nyenzo wakati wa somo.

  3. 3.

    Waambie wanafunzi kujitayarisha kufupisha sehemu zifuatazo katika Urithi Wetu:

    1. a.

      “Makazi ya majira ya baridi” (kurasa 71–72)

    2. b.

      “Watakatifu wa Brooklyn” (kurasa 74–75)

    3. c.

      “Mkusanyiko unaendelea” (kurasa 75–76)

    4. d.

      “Hapa ni sehemu sahihi” (kurasa 76–77)

  4. 4.

    Kama picha zifuatazo zipo, jitayarishe kuzitumia wakati wa somo: Mary Fielding na Joseph F. Smith wakivuka nyanda (62608; Picha za Sanaa za Injili 412) na Watangulizi wanawasili kwa meli katika ghuba ya San Francisco (Picha za Sanaa za Injili 421).

Mapendekezo kwa maendelezo ya somo

Shughuli ya Usikivu

Kama inafaa, tumia utendaji ufuatao au mojawapo ya utendaji wako kuanza somo.

Andika nchi ya ahadi kwenye ubao. Eleza kwamba mara nyingi kwenye maandiko Bwana ameongoza makundi ya watu kutoka kule walikokuwa wanaishi kwenda “nchi ya ahadi.” Maandiko mara nyingi yameita sehemu kama hii nchi iliyochaguliwa, au nchi ya amani, au nchi ya urithi (1 Nefi 2:20; M&M 45:66; 103:11)

  • Unaweza kutaja makundi yoyote toka kwenye maandiko ambayo yaliongozwa kwenye safari kwenda nchi ya ahadi? (Andika majibu ya wanafunzi ubaoni. Majibu yanaweza kuwa Wayaredi, familia ya Lehi, wana wa Israeli katika Agano la Kale, na Brigham Young na watangulizi.)

Eleza kwamba maisha yetu ya hapa duniani ni kama safari kwenda “nchi ya ahadi” ya ufalme wa selestia. Akizungumzia juu ya watangulizi walio weka msingi wa kipindi hiki cha maongozi ya Mungu, Mzee M. Russell Ballard wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema:

“Safari zao zinafanana na za kwetu. Kuna masomo kwetu sisi katika kila hatua waliyochukua—masomo ya upendo, ujasiri, bidii, uvumilivu, na zaidi ya yote imani (katika taarifa ya Mkutano Mkuu, Apr. 1997, 81: au Ensign, Mei 1997, 59).

Somo hili linazungumzia mojawapo ya safari kubwa sana katika historia—safari kubwa na ngumu ya watangulizi kwenda Bonde la Salt Lake. Wakati wa somo, waalike wanafunzi kufananisha safari ya Watangulizi na safari yao wenyewe kuelekea maisha ya milele.

Mazungumzo na matumizi

Kwa maombi chagua nyenzo ya somo ambayo itakidhi vizuri mahitaji ya wanafunzi. Watie moyo wanafunzi kushiriki uzoefu ambao unahusiana na kanuni za kimaandiko.

1. Bwana aliwaelekeza watakatifu kuhusu matayarisho yao kimwili kwa ajili ya kwa safari yao.

Mwambie mwanafunzi aliyepangiwa kufanya muhtasari wa maelezo ya Watakatifu katika Makazi ya Majira ya Baridi kutoka Urithi wetu, kurasa 71–72.

  • Watakatifu katika Winter Quarters waliteseka sana na magonjwa na shida zingine, hata hivyo waliendelea kufanya kazi na kufanya matayarisho ya safari yao. Ni kwa njia gani wao na wengine walibarikiwa kwa kuendelea na dhamira yao? (Majibu yanaweza kuwa kwamba matayarisho yao yalifanya safari yao kuwa rahisi zaidi na kuwasaidia wale watakaokuja baada yao.) Umebarikiwa vipi kwa kuhifadhi katika muda wa matatizo? Jinsi gani kuhifadhi katika muda wa matatizo kunawasaidia wale wanaokuja baada yetu?

Eleza kwamba katika Winter Quarters mnamo Januari 1847, Rais Brigham Young alipokea ufunuo kuhusu safari ya kuelekea magharibi ya Watakatifu. Ufunuo huu umeandikwa katika M&M 136.

  • Ni maelekezo gani Bwana aliwapa Watakatifu kuhusu matayarisho kwa safari yao? (Soma mistari ifuatayo pamoja na wanafunzi: na tambua maelekezo katika kila fungu la maneno. Chagua baadhi ya maswali kusaidia wanafunzi kujadili na kutumia maelekezo haya.)

    1. a.

      M&M 136:2. (Fanya “agano na ahadi kutii amri zote na sheria za Bwana.”) Kwa nini maelekezo haya ni muhimu kwa Watakatifu? Tunawezaje kutumia ushauri huu katika safari yetu?

    2. b.

      M&M 136:3. (Anzisha makundi ya watu chini ya maelekezo ya Akidi ya Wale Kumi na Wawili, pamoja na rais na washauri wawili na pamoja na makapteni kwa mamia, hamsini hamsini, na kumi kumi.) Jinsi gani utaratibu huu ni sawa na njia kata na vigingi vimeratibiwa?

    3. c.

      M&M 136:5. (“Wacha kila kikundi kijiandalie chenyewe na vyote …anavyoweza.”) Kwa nini ni muhimu kwamba tujitahidi kujitegemea?

    4. d.

      M&M 136:6. (“Jitayarishe kwa hao wanaotembea [waliobaki nyuma].) Ni matayarisho gani waliyoyafanya Watakatifu kwa hao wataobaki nyuma? (Ona M&M 136:7, 9.) Jinsi gani maelekezo haya yanatumika kwetu?

    5. e.

      M&M 136:8. (Kuwatunza “maskini, wajane, [na] wasio na Baba.”) Tunawezaje kutekeleza majukumu haya leo?

    6. f.

      M&M 136:10. (“Acheni kila mtu atumie uwezo wake wote na mali yake kuwapeleka watu hawa … kigingi cha Sayuni.”) Jinsi gani maelekezo haya yanatumika kwetu?

2. Bwana aliwaelekeza watakatifu kuhusu tabia zao.

Fundisha na jadili M&M 136:17–33. Eleza kwamba zaidi ya kuwapa maelekezo juu ya matayarisho ya kimwili, Bwana aliwapa watakatifu maelekezo kuhusu mambo ya kiroho na tabia yao wao kwa wao.

  • Ni maelekezo gani Bwana aliwapa Watakatifu kuhusu jinsi watakavyojiongoza wenyewe? (Soma mistari ifuatayo pamoja na wanafunzi: na tambua maelekezo katika kila fungu la maneno. Chagua baadhi ya maswali kuwasaidia wanafunzi kujadili na kutumia maelekezo haya.)

    1. a.

      M&M 136:19. “Na kama mtu yeyote atatafuta kujijenga mwenyewe, na hatafuti ushauri wangu, hatakuwa na uwezo”) Kwa nini unyenyekevu utakuwa muhimu kwa Watakatifu kwenye safari yao? Jinsi gani watu wakati mwingine wanataka kujijenga juu wenyewe? Tunawezaje kwa ukamilifu zaidi kutaka utukufu wa Bwana badala ya wetu wenyewe?

    2. b.

      M&M 136:21. (“Kujitenga wenyewe kutoka uovu na kuchukuwa jina la Bwana kwa njia isiyofaa.” Ona pia Alma 20:7.) Kwa nini ni muhimu kwamba tulichukuwe jina la Bwana kwa heshima kuu?

    3. c.

      M&M 136:23–24. (“Acheni kubishana wenyewe kwa wenyewe; acheni kusemeana uovu wenyewe kwa wenyewe. … na acheni maneno yenu yawe ya kuadilishana.”) Jinsi gani mabishano na kusemeana uovu yanatuzuia kama watu? Tunawezaje kushinda mabishano kati yetu? Tunaweza kufanya nini ili tuadilishane?

    4. d.

      M&M 136:25–26. (Rudisha vitu ulivyoazima au kupoteza.)

    5. e.

      M&M 136:27. (“Kuwa mwenye bidii katika kuhifadhi kile ulichonacho.”) Unafikiri inamaanisha nini kuwa “mtumishi mwenye busara? Jinsi gani utumishi wetu juu ya mali zetu za kimwili unaweza kuathiri raha yetu ya kiroho?

Katika M&M 136:28, Bwana anatoa maelekezo juu ya burudani ya kufaa. Akizungumza juu ya swala hili, Mzee David O. McKay alifundisha:

“Kwenye uwanda, baada ya kutembea kutwa mzima, magari ya kukokotwa yalivutwa kwenye mduara, na mtu mwenye fidla alichukua sehemu yake karibu na moto wa kuota na pale kwenye uwanda mpana Watangulizi shupavu waliungana katika dansi, wakiifungua kwa sala, nakushiriki katika burudani ambayo ulikuza roho ya injili. … Rais Brigham Young … aliwahi husema, kwa kweli: ‘mazingira ya dansi yalikuwa kwamba kama mzee yoyote akiitwa kutoka kwanye dansi kwenda kuhudumia mtu, mgonjwa, aliondoka na roho ileile ambayo angeondoka nayo kutoka kwenye mkutano wa akidi ya wazee’” (katika Taarifa ya Mkutano Mkuu, Apr. 1920, 117.)

  • Tunawezaje kutumia ushauri huu?

  • Bwana aliwaelekeza Watakatifu kufanya nini ili kujifunza busara? (Ona M&M 136:32–33.) Katika njia zipi umegundua maelekezo haya kuwa ni ya kweli katika maisha yako?

3. Chini ya maelekezo ya Rais Brigham Young, watakatifu walisafiri kwenda katika Bonde la Salt Lake.

Rejea kwa ramani 3 kwenye ukurasa 278 katika kitabu hiki cha kiada na ukurasa 31 ndani ya Class Member Study Guide. Eleza kwamba miaka miwili kabla Nabii Joseph Smith hajafa, alitabiri kwamba “Watakatifu wangeendelea kuteseka zaidi na mateso na wangefurushwa kwenda Rocky Mountains” na kwamba baadhi yao “wataishi na kwenda kusaidia katika kufanya makazi na kujenga majiji na kuwaona Watakatifu wanakuwa watu wenye nguvu katikati ya Rocky Mountains” (Mafundisho ya Nabii Joseph Smith, sel. Joseph Fielding Smith [1976], 255). Katika kutimiza utabiri, kiasi cha Waumini wa Kanisa 70,000 kutoka ulimwenguni kote walifanya safari ndefu na ngumu kwenda Utah kati ya miaka 1847 na 1869.

Magari ya kukokotwa yaliyo funikwa

Kuondoka kwenda Magharibi. Mnamo tarehe 4 Februari 1846 magari ya kwanza ya kukokotwa yalivuka Mto Mississippi kuanza safari ndefu na ngumu ya kihistoria kwenda magharibi.

Onesha picha za Mary Fielding Smith na Joseph F. Smith na ya Watakatifu wakiwasili San Francisco. Eleza kwamba kuna hadithi nyingi za imani na ujasiri kama Watakatifu waliosafiri kwenda Utah.

Watake wanafunzi wailopangwa watayarishe muhtasari sehemu zifuatazo kutoka Urithi Wetu: ” (Watakatifu wa Brooklyn” kurasa 74–75, “Mkusanyiko Unaendelea” kurasa 75–76, na “Hapa Ndipo” (kurasa 76–77). Kama muda unaruhusu, unaweza kutaka kueleza hadithi zingine za kuvutia za watangulizi (ona wazo la kwanza la ziada la kufundishia kama mfano.) Ungeweza pia kuwaalika wanafunzi kuelezea hadithi za watangulizi ambazo zinawavutia. Hadithi hizi za watangulizi zinaweza pia kutoka vipindi vingine katika historia ya Kanisa na kutoka nchi zingine ambako Kanisa limeanzishwa.

  • Unahisi vipi unapofikiria urithi wa imani na dhabihu ambazo watangulizi na Watakatifu wengine wametuachia? Ni kina nani ndiyo watangulizi wa Kanisa katika eneo llako? Tunawezaje kuwapa aina kama hii ya urithi hao ambao watatufuata?

  • Ni masomo gani tunaweza kujifunza kutoka kwa safari ndefu ngumu ya watangulizi ya kutusaidia kwenye safari yetu kurudi kwenye uwepo wa Mungu? (Baada ya wanafunzi wamekuwa na nafasi ya kujibu, soma maelezo yafuatayo kutoka kwa Mzee M. Russell Ballard.)

    “Maisha sio siku zote rahisi. Sehemu fulani katika safari yetu tunaweza kujisikia sawa kama watangulizi walivyojisikia walipovuka Iowa—kwenye matope hadi magotini mwetu, kulazimika kuzika baadhi ya ndoto zetu kandokando mwa njia. Sisi wote tunakabiliana na milima ya mawe, pamoja na upepo kwenye nyuso zetu na majira ya baridi yakija hivi karibuni tu. Wakati mwingine inaonekana kama vile hakuna mwisho kwa vumbi ambalo linauma macho yetu na kufifisha uwezo wetu wa kuona. Kingo kali za kukata tamaa na pingamizi vimejitokeza kutoka kwenye madhari kupunguza mwendo wetu. … Mara chache tunafika juu ya moja ya kilele cha maisha, kama watangulizi walivyofanya, ila kuona vilele zaidi vya milima mbele, virefu zaidi na vyenye changamoto zaidi kuliko kile tulichokipita. Kufyonza hazina zisizoonekana za imani na uvumilivu, sisi, kama walivyofanya watangulizi wetu, kidogo wakati wote mbele kuelekea siku ile wakati sauti zetu ziweze kuungana pamoja na hizo za watangulizi wote waliovumilia katika imani, wakiimba, ‘Yote ni sawa! Yote ni sawa!” (Katika Tarifa ya Mkutano Mkuu, Apr.1997, 82; au Ensign, May 1997, 61).

Hitimisho

Sisitiza kwamba katika njia nyingi safari yetu kuelekea uzima wa milele ni sawasawa na safari ya watangulizi kuvuka Amerika. Watangulizi walivuka nyanda kwa dhabihu binafsi kubwa na mara nyingi katika shida kali. Kuonesha imani kubwa, ujasiri, na uvumilivu waliweka mfano kwa ajili yetu tuufuate.

Eleza kwamba hii ni siku yetu katika historia ya ufalme wa Mungu duniani. Watangulizi waliweka msingi, lakini sasa ni juu yetu kukamilisha kazi. Kama Rais James F. Faust alivyoshuhudia, “Imani katika kila hatua ya baadae itatimiza ufunuo wa kinabii kuhusu majaliwa ya utukufu ya Kanisa hili” (katika Taarifa ya Mkutano Mkuu, Okt. 1997, 58; au Ensign, Nov.1997, 42).

Mzee M. Russell Ballard alisema: “Sisi ni warithi wa urithi mkubwa sana. Sasa ni heshima yetu na majukumu yetu kuwa sehemu ya tamthilia inayoendelea ya Urejesho, na kuna hadithi kubwa na za majisifu za imani zitakazoandikwa katika siku yetu. Itahitaji kila sehemu ya nguvu zetu, hekima, na nguvu kushinda vikwazo ambavyo vitatukabili. Lakini hata hiyo haitatosha. Tutajifunza, kama walivyofanya mababu zetu, kwamba ni katika imani tu—imani ya kweli, kwa roho yote, ilyopimwa na kujaribiwa—kwamba tutapata usalama na kujiamini tutapotembea katika njia zetu za hatari kupitia maisha” (katika taarifa ya Mkutano Mkuu, Apr. 1997, 83: au Ensign, Mei 1997, 61).

Toa ushuhuda kwamba njia nyingi ambazo kwanzo watangulizi walishauriwa ziko katika M&M 136 kujitayarisha kwa safari yao zinatumika pia kwenye safari yetu. Watie moyo wanafunzi kuonesha shukrani za kwa watangulizi kwa kuendeleza urithi wao wa imani.

Mawazo ya Kufundishia ya Ziada

Unaweza kutaka kutumia moja au mawazo yote yafuatayo kuongeza muhtasari wa somo uliopendekezwa.

1. Dabihu zilizofanywa na watangulizi

Kwa kuongezea kwenye utabiri ambao Watakatifu wengi wangeishi na kuwa watu maarufu katika Rocky Mountalns, Joseph Smith alitabiri mateso yao. Asema kwamba baadhi “wangeuwawa na watesi wetu au kupoteza maisha yao katika matokeo ya baridi kali au magonjwa” (Mafundisho ya Nabii Joseph Smith, 255).

Shiriki maelezo ya yafuatayo yaliyohusishwa na Mzee Thomas S. Monson alipokuwa anahudumia katika Akidi ya Wale Kumi na Wawili:

“Watangulizi wa Mormoni kwa mamia waliteseka na kufa kutokana na magonjwa, baridi kali, au njaa. Kulikuwa na baadhi ambao, kwa kukosa magari ya kukokota na makundi kwa uhalisia walitembea maili 1,300 kuvuka nyanda na kupitia milimani, wakisukuma na kuvuta mikokoteni. Katika makundi haya, mmoja kati ya sita yaliangamia.

“Kwa wengi, safari haikuanza katika Nauvoo, Kirtland, Magharibi ya mbali, au New York bali mbali nchini Uingereza, Scotland, Scandinavia, au Ujerumani. … Kati ya usalama wa nyumbani na ahadi ya Sayuni palisimama maji danganyifu na ya kutisha ya bahari kuu ya Atlantiki. Ni nani anayeweza kueleza hofu iliyoshika moyo wa binadamu wakati huo wa mivuko ya hatari? Wakishawishiwa na minong’ono ya kimya ya Roho, ikiidhinishwa na imani rahisi lakini ya kudumu, walimwamini Mungu na kuanza safari yao. …

Wakiwa kwenye mojawapo ya vyombo, [meli] vile vilivyojaa kupita kiasi vya miaka ya zamani walikuwa mababu wa mababu zangu, familia yao ndogo, na mali zao chache. Mawimbi yalikuwa makubwa mno, safari ndefu mno, makazi yaliyobanana. mno Mary mdogo sana [binti yao] siku zote amekuwa mwembamba, lakini sasa kila siku ipitayo, mama yake mwenye wasiwasi alijua dogo alikuwa anaonekana hususani dhaifu. Alikuwa amepatwa ugonjwa mbaya.… Siku hadi siku wazazi wenye wasiwasi waliangalia kwa makini nchi kavu, lakini hapakuwa na nchi kavu. Sasa Mary hakuweza kusimama. … Mwisho ulikaribia. Mary mdogo kwa amani alipita upande wa pili hili pazia la majonzi.

“Wakati familia na marafiki walipokusanyika juu ya staha iliyowazi, nahodha wa meli aliongoza huduma, na mwili ule mdogo wa thamani uliowekwa kwa upendo katika turubai lililojaa machozi, ulikabidhiwa bahari yenye hasira. Baba jasiri, katika sauti ya mhemuko iliyojaa kwikwi, alimfariji mama mwombolezaji, akirudia, ‘Bwana alitoa, na Bwana ametwa; jina la Bwana libarikiwe. Tutamwona Mary wetu tena” (katika Taarifa ya Mkutano Mkuu, Apr. 1967, 55–56 au Improvement Era, June 1967, 55).

2. “Imani katika kila hatua” onesho la video

Kama kanda ya video Mafundisho kutoka Mafundisho na Maagano na Historia ya Kanisa (53933) ipo, fikiria kuonesha “Imani katika kila hatua,” kipande cha dakika 16.