Wote Wanakaribishwa. Tembelea Kanisa lililo karibu nawe.
Maswali ya Kawaida
Je, waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni Wakristo?
Ndiyo! Kama waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, tunaamini Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na Mwokozi wa Ulimwengu. Yeye anatupenda sote zaidi ya tunavyoweza kufikiria. Tunajichukulia kuwa wafuasi wa kujitolea wa Yesu. Wakati baadhi ya yale tunayoyaaminii ni ya kipekee, tunaamini kwamba kupitia maisha Yake, huduma, dhabihu, na ufufuko, Yesu Kristo hutuokoa kutoka dhambini, mateso, na kifo.
Jifunze kuhusu imani yetu.
Ibada Kanisani zikoje?
Muda wa huduma ya Kanisa hutofautiana kutoka kusanyiko mmoja hadi lingine. Hata hivyo, unaweza mara zote kutegemea huduma ya ibada moja kuu kwa ajili ya kila mtu, ikifuatiwa na madarasa kwa ajili ya watoto, vijana na watu wazima.
Huduma kwa ajili ya kila mmoja inaitwa “mkutano wa sakramenti.” Mkutano huu unajumuisha nyimbo, sala na mahubiri (au “jumbe”) zinazotolewa na waumini tofauti tofafuti wa mkusanyiko kila wiki. Lakini sehemu muhimu zaidi ya mkutano huu ni wakati tunaposhiriki sakramenti (ambayo ni sawa na komunio) ili kumkumbuka Mwokozi.
Jifunze zaidi kuhusu huduma za Jumapili au tafuta kanisa karibu nawe .
Je,kwa nini Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho lina mahekalu?
Kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho, hekalu ni tofauti na majengo mengine ya Kanisa. Hekalu ni mahali ambapo Watakatifu wa Siku za Mwisho hupokea maelekezo maalumu kuhusu Mungu na Yesu Kristo. Hekaluni, waumini wanafanya maagano ya milele (au ahadi) na Mungu. Hii inajumuisha ahadi za kutii amri, kuishi injili ya Yesu Kristo, kuwa mwaminifu katika ndoa, na kusaidia kutunzana kwa kushiriki kile tulichonacho.
Pia, kwa sababu tunaamini familia ni za milele, kazi nyingi zinazofanywa ndani ya mahekalu ni kufanya mahusiano ya familia kuwa imara zaidi. Ndoa katika hekalu zinafanywa ili kudumu milele, sio tu “mpaka kifo kitakapotutenganisha.” Wazazi na watoto wanakuwa familia za milele katika mahekalu. Mababu wanaweza pia kupokea baraka zote za hekaluni ikiwa mtu atafanya ibada takatifu kwa niaba yao na wao kukubali tendo hilo la huduma. Mahekalu ni sehemu zenye shughuli nyingi!
Kitabu cha Mormoni ni nini?
Kitabu cha Mormoni ni kitabu cha maandiko yenye mwongozo wa kiungu ambayo hutufundisha kuhusu Mungu na Yesu Kristo. Hutusaidia kupokea mwongozo kwa ajili ya maisha yetu binafsi na kinaweza kutusaidia kuhisi kuwa karibu zaidi na Yesu Kristo. Nini chanzo cha jina hilo? Mamia ya miaka iliyopita, nabii wa kale aliyeitwa Mormoni alikusanya kumbukumbu ya watu wake. Walikabiliana na changamoto nyingi sawa na zile tulizonazo leo. Na kama vile sisi, walipata nguvu wakati walipomgeukia Yesu Kristo. Pata utambulisho wa Kitabu cha Mormoni kupitia wamisionari.
Kitabu cha Mormoni kimekusudiwa kusomwa sambamba na Biblia kama ushuhuda mwingine wa Yesu Kristo na huduma yake kama Mwokozi na Mkombozi wa ulimwengu. Kwa pamoja, Biblia na Kitabu cha Mormoni hutoa uelewa zaidi wa upendo mkuu wa Mungu kwa ajili yetu sote na huweza kutusaidia tusonge karibu Naye.
Jifunze zaidi kuhusujinsi Biblia na Kitabu cha Mormoni hufanya kazi pamoja.
Je, mnaamini katika Biblia?
Ndiyo. Biblia ni neno la Mungu, juzuu takatifu ya maandiko, na kufuata mafundisho yake huleta shangwe katika maisha yetu. Pamoja na Biblia, pia tunapata mwongozo wa kiungu katika vitabu vingine vya maandiko vya kipekee kwa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Vyote hufanya kazi pamoja kutufundisha kweli muhimu kuhusu Mungu na Yesu Kristo.
Jifunze zaidi kuhusu imani yetu katika Biblia.
Songa karibu na Mungu. Kutana na wamisionari.
Kutana mtandaoni au ana kwa ana. Tutajibu maswali yako na kukutambulisha kwenye jumuiya ya kanisa kwenye eneo lako.
Jumuiya ya Kiimani yenye fokasi kwa Yesu Kristo
Pata habari za hivi karibuni kutoka Kanisani.
Mambo mazuri yanatokea ulimwenguni kote. Pata habari za sasa juu ya miradi ya Kanisa, matukio, juhudi za kimisaada kwenye majanga na zaidi.